settings icon
share icon
Swali

Je, ni namna gani mvutio wa umbo ni muhimu wakati wa kutafuta mke?

Jibu


Hakuna shaka kwamba Mungu aliumba wanaume na wanawake kuvutina kimwili. Sehemu ya ngono katika ndoa ni muhimu kwa urafiki kati ya mume na mke na kwa kuzaa na kuishi kwa jamii. Wakati huo huo, ndoa zilizopangwa-ikiwa ni pamoja na zile ambazo wanandoa hawaonani hadi harusi-zilikuwa za kawaida katika karne zilizopita na bado zinafanyika hii leo katika maeneo mengi ya dunia.

Sulemani alielezea mvuto wa bwana arusi kwa mpendwa wake katika sura ya 4 na ya 7 ya Maneno ya Nyimbo. Anaelezea uzuri wake wa kimwili na tamaa yake kwa ajili yake. Anarudia katika sura ya 8, akielezea shauku yake kwa ajili yake na tamaa yake ya kumkumbatia. Wimbo wa Suleimani ni dalili nzuri ya upendo wa ndoa ambayo mvutio wa kimwili ni sehemu mojayapo.

Hii sio kusema kuwa mvutio wa kimwili ni kipengele muhimu zaidi kinachozingatiwa wakati unatafuta mume au mke. Kwa jambo moja, uzuri haupaswi kuelezwa na ulimwengu. Kile ambacho ulimwengu hupata kuwa cha kizuri sana huwa chini ya kiwango cha uzuri kilichoelezwa katika Maandiko. Urembo wa kimwili huyeyuka kwa wakati, lakini uzuri wa ndani huangaza kutoka kwa mwanamke anayempenda Mungu (Mithali 31:30). Petro anawahimiza wanawake kuendeleza uzuri wa ndani unatoka kwa " Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao" (1 Petro 3: 3-5). Uzuri wa nje hutoweka; Uzuri wa ndani ni wa milele.

Mvuto wa mwanamume lazima pia uwe kile kinachotoka ndani. Mfano dhahiri zaidi katika Maandiko ni Yesu, ambaye "Maana alikua mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani" (Isaya 53: 2). Lakini uzuri wa utukufu wake na neema, kama Mwana wa Mungu wa mwili, uliangaza ndani yake na ndani ya wote waliomwona. Kinyume kabisa ni Lucifer / Shetani ambaye anaelezewa kuwa "Wewe wakitia muhuri kipimo, umejaa hekima, na ukamilifu wa uzuri" (Ezekieli 28:12). Licha ya uzuri wake wa nje, Lucifer alikuwa mfano wa uovu na uovu.

Uzuri wa nje ni wa muda mfupi, lakini wanaume na wanawake ambao hukumu yao imeadhiriwa na dhambi huweka umuhimu usiofaa. Mtazamo wa Mungu ni tofauti. "Bwana haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali Bwana huutazama moyo" (1 Samweli 16: 7). Mume au mke anayetarajiwa lazima awe Mkristo wa kweli, aliyezaliwa mara ya pili ambaye anakua na kukua katika imani na ambaye ni mtiifu kwa Kristo. Watu wawili wenye lengo sawa katika maisha-kumtukuza Mungu katika yote wanayofanya-watapata kwamba mvuto wao wa kimwili huongezeka kila siku na huendelea kwa maisha.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni namna gani mvutio wa umbo ni muhimu wakati wa kutafuta mke?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries