settings icon
share icon
Swali

Je, Mungu alijitoa dhabihu ili atuokoe kutoka kwake kwa sababu ya kanuni aliyoitengeza yeye Mwenyewe?

Jibu


Baadhi hudai kwamba Mungu kimsingi hutuokoa kutoka kwa ghadhabu Yake kwa kujitoa Yeye mwenyewe ili kukidhi haja ya kanuni ambayo Aliiumba hapo awali. Kisha wanauliza, kwa nini uweke sheria? Kwa nini hawezi ondoa ghadhbu kando bila dhabihu? Na ni kwa jinsi gani inaleta maana kuwa Alijitoa kwa ajili yake Mwenye? Haya ni maswali mazuri, lakini yamejengwa juu ya kutokuelewa kwingi kwa kimsingi kuhusu asili ya Mungu na tabia Yake.

Kwanza, tutazingatia wazo kwamba Mungu alijitoa dhabihu yeye Mwenyewe kwa ajili yake Mwenyewe. Huku ni kutoelewa asili ya utatu wa Mungu vile Baba na Mwana wameungana. Baba alimtuma Mwana (Yohana 7:33), Mwana akatimiza mapenzi ya Baba (Yohana 17:4), na Mwana akafa kwa ajili ya wenye dhambi (Warumi 5:8). Baba hakukufa; Mwana aliyatoa maisha yake kama ridhiki kwa ajili ya dhambi (1 Yohana 4:10).

Pili, hitaji la Mungu kwamba dhabihu ni ya muhimu ili kufidia dhambi sio sheria ambayo Yeye ‘alitunga’ tu. Sheria ya Mungu si kitu ambacho Aliumba kiholela; Sheria ni upana wa asili ya utakatifu Wake. Mungu hakubuni maadili; Alijidhihirisha kwetu, na ufunuo huo wa nafsi yake ndio maadili. Mungu aliposema, “mshahara wa dhambi ni mauti” (Warumi 6:23), hakuwa anatunga sheria au kuweka adhabu mpya juu yetu; badala yake, Alikuwa anatufunulia uhalisi usiobadilika milele-ikiwa mtu ataondoka kutoka kwa Mtegemezi wa maisha, basi kimantiki unajitenga na uwezekano wa kuendelea kuwepo. Wale wanaokataa Uzima wana chaguo moja tu, nalo ni Mauti.

Kusema kwamba Mungu aliunde “kanuni” ambazo kwazo dhambi inapatanishwa ni sawa kwamba Isaac Newton aliindika sheria ya uvutano. Newton alielezea athari na asili ya mvuto, lakini sheria ya mvuto ilitangulia na kupita maelezo yake. Kwa mtindo huo huo, Biblia inaeleze asili ya dhambi na uadilifu, lakini sheria za watu wote kuhusu dhambi na uadilifu, kifo na uzima, na haki na neema vinatangulia na kupita kuandikwa kwake. Sheria za Mungu ni za milele na hutiririka kutoka kwa asili ya Mungu Mwenyewe.

Kwa kuwa Sheria ya Mungu inatoka kwa asili yake, Sheria hiyo haibadiliki. Na “linasimama imara mbinguni” (Zaburi 119:89). Mungu hawezi kuweka kando ghadhabu yake kwa dhambi kama tunavyoweza kubadilisha DNA yetu. Haki ya Mungu si mwongozo anaochagua kuufuata; haki ni sehemu ya tabia yake. Uadilifu na haki ni msingi wa utawala wake mkuu wa ulimwengu (Zaburi 97:2). Bila haki-bila ghadhabu kwa dhambi-Yeye si Mungu. Mauti hufuata dhambi si kwa sababu “Mungu amesema hivyo” ni kwa sababu dhambi ni uasi dhidi ya Uzima.

Tunapaswa pia kufafanua asili ya dhambi. Dhambi ni zaidi ya mawazo au matendo ambayo Mungu “hayapendi.” Kunacho kiwango cha kusidi ambacho dhambi hupimwa kwayo. Dhambi ni wazo au tendo lolote lisilolingana na utakatifu wa Mungu na ukamilifu kamili. Ni kile kinachopinga asili yake. Uongo ni makosa-si kwa sababu Mungu alichagua kutoupenda bali kwa sababu Mungu ni kweli, na uongo unapinga asili Yake. Mauaji ni makosa-sio kutokana na kanuni ya kiholela Mungu aliyoifnaya bali kwa sababu Mungu ni Uzima, na uuaji unapinga tabia Yake ya milele.

Kama wenye dhambi mbele za Mungu mtakatifu, tumekabiliwa na hukumu ya kweli: untengano wa milele, yaani kifo cha milele. Ikiwa Mungu angeweka kando ghadhabu yake kwa dhambi na asingetupa kile ambacho dhambi ilihitaji, angeacha kuwa mwenye haki. Lakini, kwa upendo na rehema zake kuu, Mungu alitoa njia ya kutosheleza haki na wokovu kuzidishwa: “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Katika msalaba wa Yesu, haki kamilifu na rehema kamilifu hukutana. Dhambi na udhalimu viliadhibiwa msalabani, na Mwana wa Mungu akipokea hukumu kwa ajili ya dhambi. Ni kwa sababu adhabu ya dhambi ilitoshelezwa kupitia dhabihu ya Kristo kwamba Baba anaweza zidisha rehema yake kwa wenye dhambi wasiostahili. Mungu alikuwa mwenye haki katika kuadhibu dhambi, na anaweza pia kuwahesabia haki wenye dhambi wanaompokea Kristo kwa imani (Warumi 3:26). Haki ya Mungu na huruma zake vilidhihirishwa kwa kusulubishwa kwa Kristo. Msalabani, haki ya Mungu ilitekelezwa kwa ukamilifu (juu ya Kristo), na rehema ya Mungu ilizidishwa kwa ukamilifu (kwa wote wanaoamini). Rehema kamilifu ya Mungu ilionyeshwa kupitia haki yake kamilifu.

Mungu hakujitoa dhabihu kwa ajili yake ili kutuokoa kutoka kwake kwa sababu ya kanuni aliyoitengeza yeye Mwenyewe. La, kuna uhalisi wa kiroho ambao ni hakika kama uhalisi wowote wa kimwili au sheria ya asili ambayo tunaweza kumchunguza: mojawapo ya hizo, uhalisi ni kwamba kifo kinafuata dhambi. Lakini Mungu ambaye ni upendo (1 Yohana 4:8) alimtuma Mwanawe ili atuokoe kutoka kwa dhambi zetu na uovu ambao kwa kwaida huwapata wale wanaokataa mema. “Upendo ulibanwa kwa historia yote katika sura hiyo ya upweke msalabani, ambaye alisema kwamba angeweza kuwaita malaika wakati wowote kwenye misheni ya uokoaji, lakini akachagua kutofanya hivyo-kwa sababu yetu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, Mungu alijitoa dhabihu ili atuokoe kutoka kwake kwa sababu ya kanuni aliyoitengeza yeye Mwenyewe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries