settings icon
share icon
Swali

Je, "mume wa mke mmoja" inamaanisha nini katika 1 Timotheo 3:2? Je, mume aliyetalaka anaweza kutumika kama mchungaji, mzee, au shemasi?

Jibu


Kuna angalau uwezekano wa aina tatu wa tafsiri ya maneno "mume wa mke mmoja" katika 1 Timotheo 3:2. 1) Inaweza tu kusema kwamba mwenye mke Zaidi ya mmoja hafai kuwa mzee, shemasi au mchungaji. Hii ni ndio tafsiri halisi ya maneno, lakini inaonekana kwa kiasi fulani uwezekano kwa kuzingatia kwamba mitala ni nadra kabisa katika wakati Paulo alikuwa akuandika. 2) Maneno hayo yanaweza kutafsiriwa pia "mke mmoja- mume mmoja." Hii itakuwa inaonyesha kuwa Askofu lazima awe mwaminifu kabisa kwa mwanamke ameoleka kwake. Tafsiri hii inalenga zaidi juu ya usafi wa kimaadili kuliko hali ya ndoa. 3) kifungu kinaweza pia eleweka kutangaza kwamba ili kuwa mzee / shemasi / mchungaji, mume anaweza kuwa tu ameoa mara moja, mbali na kesi cha mjane anayeoa tena.

Tafsiri ya 2) na 3) ndizo hutumika hii leo. Ufafanuzi wa 2) linaonekana kuwa la nguvu, hasa kwa sababu maandiko yanaonekana kwa ajili ya kuruhusu talaka katika mazingira ya kipekee (Mathayo 19:9; 1 Wakorintho 7:12-16). Itakuwa pia muhimu kutofautisha kati ya mtu ambaye alikuwa ametalaka na kuoa tena kabla ya kuwa Mkristo kutoka kwa mtu ambaye alitalaka na kuoa tena baada ya kuwa Mkristo. Mtu ambaye amehitimu haipaswi kutengwa na uongozi wa kanisa kwa sababu ya vitendo aliovifanya kabla ya kumjua Bwana Yesu Kristo kama Mwokozi wake. Ingawa 1 Timotheo 3:2 hasa haimtengi mtu aliyetaliki au kuoa tena kutoka kutumikia kama mzee / shemasi / mchungaji, kuna masuala mengine ya kuzingatia.

Kufuzu kwa kwanza wa mzee / shemasi / mchungaji ni kuwa "asiyelaumika" (1 Timotheo 3:2). Kama talaka / au kuoa tena kunaweza leta matokeo mabaya ya ushahidi kwa ajili ya mtu katika kanisa au jami, inaweza kuwa "asiyelaumika" ndio imemtoa nje na badala yake haihusishi hitaji la "mume wa mke mmoja ". Mzee / shemasi / mchungaji anafaa kuwa mtu ambaye Kanisa na jamii inaweza kuangalia kama mfano wa kufanana na Kristo na uongozi wa uungu. Kama talaka yake / au ikiwa hali yake ya kuoa tena inapunguza thamani ya lengo hili, labda anapaswa kutumikia katika nafasi ya mzee/ shemasi/ mchungaji. Ni muhimu kukumbuka kuwa, kwa sababu mtu hafai kuwahudumia kama mzee / shemasi / mchungaji, yeye bado ni mwanachama wa thamani katika mwili wa Kristo. Kila Mkristo ana karama ya kiroho (1 Wakorintho 12:4-7) na inaitwa kushiriki katika kiwajenga waumini wengine kwa karama hizo (1 Wakorintho 12:07). Mtu ambaye hafai nafasi ya mzee / shemasi / mchungaji bado anaweza kufundisha, kuhubiri, kutumika, omba, abudu, na kutoa mchango muhimu katika kanisa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, "mume wa mke mmoja" inamaanisha nini katika 1 Timotheo 3:2? Je, mume aliyetalaka anaweza kutumika kama mchungaji, mzee, au shemasi?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries