settings icon
share icon
Swali

Mhubiri ni nini?

Jibu


Mhubiri ni mtu ambaye hutangaza habari njema; kwa maneno mengine, mhubiri wa injili au mmishonari. Mtu mwenye zawadi ya uinjilisti ni mara nyingi mtu anaye safiri kutoka sehemu hadi nyingine ili kuhubiri Injili na kupiga toba. Waandishi wa kibinadamu wa Injili nne-Mathayo, Marko, Luka, na Yohana-wakati mwingine huitwa "Wainjilisti" kwa sababu waliandika huduma ya Yesu Kristo- "habari njema," kwa kweli.

Waefeso 4: 11-13 inasema, "Kristo mwenyewe aliwapa mitume,na wengine kuwa manabii,na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji na walimu,kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu,hata kazi ya huduma itendeke,hata mwili wa Yesu ujengwehata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa Imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu,hata kuwa mtu mkamilifu hata kufika kwenye cheo cha kimo cha ukamilifu wa Kristo . "Katika Matendo 21: 8 Filipo anaitwa minjilisti, na katika 2 Timotheo 4: 5 Paulo anahimiza Timotheo kufanya kazi ya minjilisti. Haya ndiyo matumizi matatu tu ya mhubiri wa neno katika Biblia nzima. Watu wengine wanaweza kuchukuliwa kama "wainjilisti" kwa kuwa walihubiri habari njema, ikiwa ni pamoja na Yesu Mwenyewe (Luka 20: 1) na Paulo (Warumi 1:15), lakini Filipo ndiye mtu mmoja aitwaye mhubiri katika Maandiko.

Filipo alikuwa mmoja wa madikoni saba waliochaguliwa ili mitume waweze kufanya kazi yao ya kufundisha na kusali (Matendo 6: 2-4). Kwa wazi, Filipo alikuwa amekaa Kaisaria na alikuwa ameishi huko kwa miaka 20 kabla Paulo hajafika katika Matendo 21. Filipo mwanzo kazi yake ya uhubiri ilikuwa Samaria (Matendo 8: 4-8). "Alimtangaza Masihi" kwa Wasamaria (mstari wa 5) na kufanya miujiza, ikiwa ni pamoja na kuwatoa pepo na kuponya waliopooza. Ni muhimu kuona kwamba Filipo alibatiza kwa maji kwa jina la Yesu, lakini ubatizo wa Roho Mtakatifu haukutokea mpaka mitume walifika Samaria.

Uwepo wa Petro na Yohana huko Samaria na makao ya Roho ya Wasamaria walioamini (Matendo 8:17) ilithibitisha huduma ya Philip huko. Kama mhubiri, Filipo alikuwa amehubiri injili, na, wakati Wasamaria walipoamini na kupokea Roho, walikaribishwa kanisani. Ambapo hapo awali kulikuwa na mgawanyiko na chuki kati ya Wayahudi na Wasamaria, sasa kulikuwa na uhusiano wa kiroho wa upendo (Wakolosai 3:14). Jitihada za Filipo za kupiga hatua ziliweka msingi kwa wasikilizaji wake kupokea Roho Mtakatifu kwa imani. Kazi ya awali ya mhubiri kwa wokovu ni yale waliyoitwa wainjilisti wamefanya tangu wakati huo.

Huduma ya Filipo kama mwinjilisti inaendelea katika Matendo 8 kama anaongozwa na malaika kwenda barabara ya jangwa kwenda Gaza. Kwenye barabara anakutana na mtumwa wa Ethiopia aliyekuwa afisa wa mahakama kwa malkia wa Ethiopia. Filipo anafungua kuelewa kwa Neno la Mungu kwa yule mtu, na huyo towashi anaokolewa. Filipo anambatiza mtu huyo, na Roho Mtakatifu kumnyakua Filipo mbali (Matendo 8:39). Baadaye Filipo "alionekana Azoto,alipokuwa akipita akahubiri injili katika miji yote hadi akafika Kaisaria" (aya ya 40). Kila mahali alipoenda, Filipo alishiriki injili. Hiyo ndiyo wainjilisti hufanya.

Timotheo aliambiwa kufanya mahubiri ya kabla ya wokovu ambayo ni "kazi ya minjilisti" (2 Timotheo 4: 5). Uhubiri huo huo wa habari njema ni wito wa jumla kwa wanafunzi katika Tume Kuu na sisi sote mpaka mwisho wa zama (Mathayo 28: 16-20). Katika Yuda 1: 3, watakatifu wote wanapaswa kupigana kwa bidii kwa ajili ya imani iliyotolewa kwao, na katika mstari wa 23 tunapaswa "kuwaokoa wengine kwa kuwanyakua kutoka kwa moto."

Ofisi ya muinjilisti itahitajika mpaka kanisa lifikie ukomavu wa Kristo mwenyewe (Waefeso 4:13). Habari njema inapaswa kugawanywa. Na tuna habari njema ya wote-Yesu alikufa na kufufuka tena na anaokoa wote wamwitao (Waroma 10: 9-13).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mhubiri ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries