settings icon
share icon
Swali

Mtu wa ndani ni nani?

Jibu


Paulo anatumia neon mtu wa ndani mara kadhaa katika barua zake (2 Wakorintho 4:16; Waefeso 3:16). Warumi 7: 22-23 inasema, "Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu." "Mtu wa ndani" ni njia nyingine ya kuelezea sehemu ya kiroho ya mtu. "Mtu wa nje," kwa kulinganisha, itakuwa ni sehemu inayoonekana, ya nje ya mtu.

Wanadamu waliumbwa na Mungu kwa roho, nafsi, na mwili (Mwanzo 1:27, 1 Wathesalonike 5:23). Imesemekana kwamba sisi si miili na roho; sisi ni nafsi ambazo zina miili. Mwili-"mtu wa nje" — ni nyumba yetu ya kimwili ambayo ina uzoefu na ulimwengu. Miili yetu hufanya kazi hasa kwa njia ya hisia tano na kwa kukutana na mahitaji yasiyo ya kawaida ambayo hutuongoza kula, kunywa, na kulala. Miili yetu sio maovu lakini ni zawadi kutoka kwa Mungu. Anatamani kwamba sisi tuitoe miili hiyo kama dhabihu ilyo hai kwake (Warumi 12: 1-2). Tunapokubali zawadi ya Mungu ya wokovu kupitia Kristo, miili yetu huwa hekalu ya Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 6: 19-20; 3:16).

Nafsi zetu ndio chanzo uhai wetu ambao mawazo yetu, mapenzi, na hisia hufanya kazi. Na roho zetu tunachagua kusikiliza na kutii tamaa za mwili wetu au tamaa za Roho Mtakatifu (Wagalatia 5: 16-17; Warumi 8: 9; Marko 14:38). Roho ya mtu ni chumba cha mahakama ambapo maamuzi ya uhai yanafanywa. Ni kiti cha maisha ya kibinafsi na chemchemi ambayo sifa za tabia kama ujasiri, kujihurumia, kujihoji nafsi, na kujipongeza zinatokea.

Roho yetu ina mtu wa ndani kuhusu Maandiko ambayo husema. Roho zetu ni ndio mahli Roho wa Mungu huwasiliana nasi. Yesu alisema, "Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli" (Yohana 4:24). Ni ndani ya roho zetu kwamba tumezaliwa tena (Yohana 3: 3-6). "Mtu wa ndani" ana dhamiri ambayo Roho Mtakatifu anaweza kuingia na kuhukumu dhambi (Yohana 16: 8; Matendo 24:16). Roho zetu ni sehemu zetu kama Mungu, na ujuzi wa ndani ya haki na mbaya (Warumi 2: 14-15). Waraka wa Kwanza wa Wakorintho 2:11 inasema, "Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu."

Warumi 12: 1-2 inatuhimiza sisi tusiifuatishe namna dunia hii inavyofikiria; badala yake, mtu wetu wa ndani lazima atabadilishwe na afanywe "upya katika akili zetu." Upyaji huu wa akili unakuja kama tunaruhusu Roho Mtakatifu kwa hiari kutawala ndani yetu "mtu wetu wa ndani." Anaanza kubadilisha matendo na matamanio yetu ili tufanane na Yake. Warumi 8: 13-14 inasema, "kwa maana kama tukiishi kwa kufuata mambo ya mwili, mwataka kufa; bali kama mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu."

Warumi 7 hufafanua vita vingi vya maumivu kati ya mwili na roho zetu. Roho zetu, baada ya kuzaliwa upya na nguvu za Mungu, hutamani kumtii na kufuata Yesu. Lakini mwili haufi kifo rahisi. Warumi 6 inatueleza jinsi tunavyoweza kuruhusu mtu wa ndani kuwa na ushindi juu ya mwili. Mstari wa 6 na 7 wanasema, "Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko. Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani." Mpaka tukijione wenyewe" kusulubishwa pamoja na Kristo" (Wagalatia 2:20), nafsi na mwili unapigana vita na roho kwa ajili ya udhibiti. Tunaendelea kuishi katika hali ya kushindwa mpaka tufie nafsi zetu na kuruhusu Roho kuwa na udhibiti kamili juu ya kila sehemu ya maisha yetu, mtu wa ndani na wa mtu nje.

Ni matamanio ya Mungu na mpango kwa wanadamu kwamba tuishi daima tukiongozwa na asili ya kuzaliwa tena, ambayo inaambatana na Roho wa Mungu. Lakini asili yetu ya kuanguka inataka kutawala, na hivyo vita vya kiroho vinashambuliwa. Warumi 7:24 inaleta swali ambalo kila mfuasi wa Kristo anauliza: "Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti?" Mstari wa 25 hujibu swali hili: "Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu!" Kujitoa kwa mtu wa ndani kwa udhibiti wa Roho Mtakatifu ni kiwango ambacho tunatembea katika ushindi wa kuendelea juu ya mwili wetu ulioanguka.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mtu wa ndani ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries