settings icon
share icon
Swali

Je! Ni nani mtu mwaasi sheria katika 2 Wathesalonike 2:1–12?

Jibu


Mtu wa uasi katika 2 Wathesalonike 2:1-12 ni Mpinga Kristo atakaye kuja ulimwenguni mwanzoni mwa Siku ya Bwana. Siku hii, wakati mwingine inaitwa "nyakati za mwisho," itaanza baada ya unyakuzi wa kanisa katika 1 Wathesalonike 4:13-18 (angalia 1 Wathesalonike 5:1-11). Ni vyema kukumbuka kwamba Siku ya Bwana sio ile masaa ishirini nan ne; badala yake ni muda ulio zidishwa ambao unajumuisha miaka saba ya dhiki, kuruki kwa Kristo ili aangamize waasi wote dhidi yake, miaka 1,000 ya utawala wa Kristo duniani, ushindi wa mwisho kwa Shetani, na Kiti Cheupe Kikuu cha Hukumu.

Mpinga Kristo anapewa jina "mtu mwaasi sheria" kwa sababu atampinga kila njia Mungu wa kibiblia na sheria Yake. Atakuwa mwaasi kabisa. Danieli 7 anazungumza juu ya mtu huyu kama mfalme "mwenye kuburi" ambaye "akijaribu kubadili majira na sheria" (aya ya 11 na 25). Atakuja akitoa amani ya uwongo kwa ulimwengu na kwa haiba yake ya kuvutia, ahadi nzuri, na miujiza ya kushangaza itayaunganisha mataifa yote kisiasa, kiuchumi, na kidini chini ya uongozi wake. Wakati huo huo, atafanya agano na Israeli kwa miaka mitatu na nusu (taz. Danieli 9:27). Katikati mwa miaka saba, mtu huyo mwaasi sheria atavunja agano lake na Israeli, na atasimamisha Israeli kutoa dhabihu zake (Danieli 9:27), na kuingia hekaluni kujifanya kuwa "mungu" na kudai aabudiwe (2 Wathesalonike 2: 4). Hili ndilo "chukizo linalosababisha ukiwa" ambalo Yesu alizungumzia katika Marko 13:14.

Shetani anafanya kazi kupitia Mpinga Kristo, kwa kuwa Shetani mwenyewe hana uwezo wa kubadilika. Kwa kumshika mateka na kumumliki Mpinga Kristo, Shetani anaabudiwa katika hekalu mahali ambapo Mungu wa kibiblia anaabudiwa. Ndio sababu Mpinga Kristo anaitwa mtu mwaasi sheria. Kujifanya "mungu" ndio katalio la maadili ya Mungu ya kibiblia na sheria zake.

Hatua hii ya Mpinga Kristo itasababisha machafuko katika ufalme wake wa kiulimwengu, majeshi kutoka Mashariki yataungana kupigana nay eye. Kwa sababu ya kupigana wao kwa wao majeshi ya ulimwengu yataungana kupigana na Mfalme wa wafalme na Bwana wa mabwana, ambaye anakuja kumwangusha mtu mwaasi na jeshi lake katika vita vikuu vya Armagedo (Ufunuon 16:16; 19:19). Naam, mtu mwaasi atashindwa katika vita. Yeye pamoja na manabii wake wa uwongo watatupwa katika ziwa la moto (Ufunuo 19:20). Neno la Mungu (Ufunuo 19:13), Yesu Kristo, watakuwa washindi.

Mtazamo wa haraka wa matukio ya ulimwengu wetu hii leo hufunua kwamba uasi-sheria unaongezeka. Uasi kama huo utaendelea na kuongezeka (2 Timotheo 3:13), na mtu wa uasi atakapotokea, atakaribishwa kwa mikono miwili. Wale ambao wamemkataa Mfalme wa Amani wa kweli, Yesu Kristo, wataanguka kwa ahadi tupu ya amani ya Mpinga Kristo. Vile vile ni muhimu sana kwamba kila mmoja wetu awe na hakika kwamba tumempokea Yesu Kristo kama Mwokozi wetu na tunaishi kwa ajili Yake. "Jihadharini! Kesheni! Kwa maana hamjui wakati ule" (Marko 13:33).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni nani mtu mwaasi sheria katika 2 Wathesalonike 2:1–12?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries