settings icon
share icon
Swali

Ni kwa nini Mungu aliuweka mti wa ujuzi ya mazuri na mabaya katika bustani mwa Edeni?

Jibu


Mungu aliuweka mti wa ujuzi ya mazuri na mabaya katika bustani mwa Edeni ili awape Adamu na Hawa chaguo la kumtii au kutomtii. Adamu na Hawa walikuwa huru kufanya cho chote walichotaka, ila tu kula matunda kutoka kwa mti wa ujuzi ya mazuri na mabaya. Mwanzo 2:16-17, “BWANA Mungu akamwagiza huyo mtu, akisema, Matunda ya kila mti wa bustani waweza kula, walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile kwa maana siku utakpokula matunda ya mti huo utakufa hakika.” Kama Mungu angewapa Adamu na Hawa chaguo, basi wangekuwa machine ifanyayo kazi kama mtu, kwa kufanya chenye walipangiwa kufanya. Mungu aliwaumba Adamu na Hawa wawe viumbe “huru”, wakiwa na uwezo wa kufanya maamuzi, uwezo wa kuchagua mazuri na mabaya. Ili Adamu na Hawa wawe huru, walistahili kuwa na chaguo.

Hapo mwanzo hakukuwa na kitu chochote kiovu kuhusu mti au matunda ya mti. Ni vile kuna uwezekano kuwa kukula matunda kutoka kwa mti kuliwapa Adamu na Hawa ujuzi zaidi. Lilikuwa tendo la kukaidi ambalo lilimfungua Adamu na Hawa macho kwa dhambi. Dhambi yao ya kumkaidi Mungu ilileta dhambi ulimwenguni na katika maisha yao. Kukula tunda, kama tendo la kukaidi kinyume na Mungu, ndilo liliwapa Adamu na Hawa ujuzi wa mabaya (Mwanzo 3:6-7).

Mungu hakutaka Adamu na Hawa watende dhambi. Mungu alijua mbele ya wakati matekeo ya dhambi yatakuwa. Mungu alijua Adamu na Hawa watatenda dhambi na kwa hivyo wateleta dhambi, mateso na kifo katika ulimwengu. Kwa nini, basi Mungu alimruhusu Shetani kujaribu Adamu na Hawa? Mungu alimrushu shetani kuwajaribu Adamu na Hawa ili awalazimishe kufanya uchaguzi. Adamu na Hawa walichagua penzi lao wenyewe kumkaidi Mungu na kula tunda walilokatazwa. Matokeo- uovu, dhambi, mateso, magonjwa na kifo- vimepiga ulimwengu tangu enzi hizo. Uamuzi wa Adamu na Hawa üliletea kila mtu ambaye anazaliwa kuwa na dhambi ya uzao, hali ya kutenda dhambi. Uamuzi wa Adamu na Hawa ndio hatimaye ulimwihitaji Kristo Yesu afe msalabani na kumwaga damu yake kwa ajili yetu. Kupitia kwa imani katika Kristo, tunaweza kuwa huru kutoka madhara ya dhambi, na mwishowe kutoka kwa dhambi. Ni maombi yangu kuwa tuyakumbuke maneno ya Mtume Paulo katika Warumi 7:24-25, “Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi.”

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni kwa nini Mungu aliuweka mti wa ujuzi ya mazuri na mabaya katika bustani mwa Edeni?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries