settings icon
share icon
Swali

Je! inamaanisha nini kuwa Shetani ndiye mtawala wa ufalme wa anga (Waefeso 2:2)?

Jibu


“Kwa habari zenu, mlikuwa wafu katika makosa na dhambi zenu, ambazo mlizitenda mlipofuatisha namna ya ulimwengu huu na za yule mtawala wa ufalme wa anga, yule roho atendaye kazi sasa ndani ya wale wasiotii” (Waefeso 2:1-2). Katika andiko hili mtume Paulo anaelezea Shetani kwanza kama “mtawala” aliye na nguvu, kwa sababu ana mamlaka ya kweli katika ulimwengu (1 Yohana 5:19). Nguvu hizi amepewa na Mungu (Luka 4:6). Shetani ako na uwezo juu ya magonjwa fulani (Luka 13:16; angali pia 2 Wakorintho 12:7- haijulikani kuwa “mwiba” Paulo alikua nao ilikua ugonjwa au kitu kingine). Kwa namna fulani, Shetani ako na nguvu juu ya kifo (Waebrania 2:14). Sababu ambayo Shetani anaitwa mtawala badala ya mfalme ni kwamba kuna Mfalme-Yesu Kristo (1 Timotheo 6:15).

Shetani pia ana nguvu juua ya baadhi ya watu. “wana wa kuasi” ambao wanarejelewa katika Waefeso 2:2 ni wale ambao hawajamwamini Kristo kama Bwana na Mwokozi (rejelea, Matendo 26:18; 2 Wakorintho 4:4; Ufunuo 13:12). Mapepo pia wako chini ya utawala wa Shetani (Mathayo 12:24), na mojawapo ya majina yake ya cheo ni “mtawala wa mapepo” (Mathayo 9:34). Shetani ako na ufalme (Mathayo 12:26) na kiti cha enzi (Ufunuo 2:13). Shetani anaitwa mtawala kwa sababu yeye ni mtawala na ana uwezo wa kudhihirisha uovu duniani kupitia kwa kuwashawishi watu na kuamrisha mapepo.

“Anga” katika Waefeso 2:2 inaweza kurejelea makao yasiyoonekana yaliyo juu ya dunia ambabpo Shetani na mapepo wake hutembea na kuishi. Mahali hapa, bila shaka ni mahali pa anga hewa au “anga.” katika Waefeso 6:12 Paulo anaandika, “Kwa maana kushindana kwetu si juu ya nyama na damu, bali dhidi ya falme, mamlaka, dhidi ya wakuu wa giza na majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.” Hili eneo linaitwa “anga” ovu, inaweza kuwa ni mahali halisi, lakini pia linaweza tumika sawia na neno “ulimwengu” katika Yohana 12:31. Ulimwengu wote ni milki ya Shetani (Mathayo 4:8-9).

Ingawa Shetani ana nguvu na mamlaka kwa mfumo wa dunia ya sasa ambapo yeye anaishi, nguvu zake zina kiwango, kila mara ziko chini ya uweza wa Mungu (Ayubu 1:12), na ni za muda (Warumi 16:20). Mungu hajafunua njia zote za Shetani, na ni lini utawala wake utakuwa, lakini ameifanya wazi kwamba kunayo njia moja tu ya kuepuka nguvu za mapepo ya Shetani, na hiyo njia ni kupitia kwa Mwanwe Yesu (Matendo 26:18; Wakolosai 1:13-14). Ni Yes utu ambaye alitunikwa msalabani alitangaza ushindi: “Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje” (Yohana 12:31).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! inamaanisha nini kuwa Shetani ndiye mtawala wa ufalme wa anga (Waefeso 2:2)?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries