settings icon
share icon
Swali

Kunayo kitu kama mpenzi war oho? Je! Mungu ako na mtu mmoja peke ambaye wastahili kumuoa?

Jibu


Dhana ya pamoja ya “mpenzi wa roho” ni kuwa kwa kila mtu, kuna mtu mwingine ambaye ni “mkamilifu na anamstahili” na kama utaoa yeyote mbali na huyu mpenzi wa roho, hautakuwa na furaha kamwe. Je! Hii dhana ya mpenzi wa roho ya kibibilia? La, sio. Mpenzi wa roho limetumika kama kisingizio cha talaka. Watu ambao hawana furaha katika ndoa zao, wanadai kwamba hawakuwaoa wapenzi wa roho zao na kwa hivyo lazima wawataliki na waanze kusaka mpenzi wa kweli. Hakuna kisingizio kingine ambacho si cha kibibilia kama hiki. Kama umeolewa na mtu ambaye umeoleka kwake ni mpenzi wako. Mariko 10: 7-9 yasema, “Kwa sababu huyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe,” kwa mfano wapenzi.

Ndoa uenda isiwe ya kufunganishwa na furaha vile wanaoana watakvyo penda iwe. Mume na mke huenda wasiwe na, mhemuko, na umoja wa kiroho ambao wakethamani. Na hata katika hali hii, mume na mke bado wangali wapenzi. Mwanandoa katika hali kama hiyo anastahili kutafuta kuanzisha “mpenzi wa roho” wa kweli. Kwa kutii chenye Bibilia inafundisha kuhusu ndoa (Waefeso 5:22-33), wanandoa wanaweza anzisha mapenzi, upendo na kujitolea ambao kuwa “mwili mmoja” mpenzi wa roho unahuzisha. Kama umeolewa kwa mpenzi. Haijalishi ni namna gani ndoa haina umoja, Mungu anaweza kuleta uponyaji, msamaha, urejesho, na upendo wa kweli wa ndoa na umoja.

Je! Inawezekana uoe mtu ambaye si wako? Ikiwa tutajitolea kwa Mungu na kutafuta mwongozo wake, Anaahidi kutuongoza: “Mtumaini BWANA kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe. Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako” (Methali 3:5-6). Hatari ya Methali 3:5-6 nikwamba kama haumwamini Bwana kwa moyo wako wote, na kutegemea akili zako, utaelekea mahali papaya. Naam, kuna uwezekano, wakati wa kutotii na ukosefu wa ushirika wa karibu na Mungu, kuoa mtu ambaye Mungu akukupangia uoe. Hata kama kwa hali kama hiyo, Mungu ni mwenye mamlaka na ndiye anatawala.

Hata kama ndoa haikuwa mpango wa Mungu, bado ingali katika penzi lake kuu na mpango wake. Mungu anachukia talaka (Malaki 2:16), na “kumwoa mtu asiye wako” hii kamwe haijadhihirishwa katika Bibilia kama misingi ya talaka. Kisingizio “Nilimwoa mtu ambeye sikustahili na kamwe sitakuwa na furaha ila tu nimpate mpenzi wangu wa kweli” pia sio ya kibibilia katika hali mbili. Kwanza kisingizio kwamba uamuzi wako mpaya umepita mapenzi ya Mungu na kuuharibu mpango wake. Pili, ni kisingizio kuwa Mungu hana uwezo wa kuifanya ndoa inayotaabika kuwa ya furaha, ishikanishwe na ya ufanisi. Hakuna kitu chochote tutakachokifanya ambacho kitageuza mapenzi ya Mungu. Mungu anaweza kuwachukua watu wawili, haijalishi namna hawaambatani, na kuwafinyanga kuwa watu wawili ambao ni wakamilifu kwa wao wenyewe.

Ikiwa tutautunza ushirika na Mungu, atatulinda na kutuelekeza. Ikiwa mtu anatembea na Mungu na kwa kweli kutafuta mapenzi yake, Mungu atamwongoza huyo mtu kwa mpenzi ambaye anataka. Mungu atatuongoza kwa “wapenzi” wetu ikiwa tutanyenyekea kwake na kumfuata. Ingawa kuwa mpenzo ni hali na tendo. Mume na mke ni wapenzi kwa njia kwamba “wako mwili mmoja,” kiroho, kimwili na kimhemuko wameunganishwa. Kimatendo, kuna mpangilio wakuchukuliwa ambao wanandoa ni nafsi, wapenzi na kuufanya ukweli wa kila siku kuwa wa haki. Wapenzi wa kweli umoja ni kitu cha uwezekano kwa kuweka kitika matendo kanuni na mipangalio ya bibilia kuhusu ndoa.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kunayo kitu kama mpenzi war oho? Je! Mungu ako na mtu mmoja peke ambaye wastahili kumuoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries