settings icon
share icon
Swali

Je! Nipaswa kuangalia nini katika mpenzi wa kiume wa Kikristo?

Jibu


Biblia haitaji aina ya uchumbiaji wa mahusiano tunayoona leo. Badala yake, kwa upande wa mahusiano ya kimahaba, inalenga kanuni za ndoa. Uchumbiaji leo hutumiwa kama njia ya kutathmini ikiwa mwanamume na mwanamke watakuwa waenzi wa ndoa mzuri. Kwa hivyo inafuata kwamba mpenzi wa kiume wa Kikristo lazima awe, kwanza kabisa, mwanaume unayefikiria atafanya mume mzuri Mkristo. Mwanamke Mkristo anatakiwa kutafuta mtu ambaye ni makini juu ya Mungu na dhati kuhusu uhusiano wake pamoja naye. Mtu yeyote anaweza kusema wanampenda Yesu au kwamba wao ni Wakristo. Unajuaje, unapompenda mtu, kwamba yeye ni halisi?

Biblia imejaa mistari inayoelezea ni nini Mkristo mwanaume anapaswa kuwa kama, mistari ambayo ni ya manufaa na yenye kuaminika kwa mwanamke anayetathmini mume anayeweza. Yafuatayo ni miongozo inayotokana na aya hizo. Mpenzi wa kiume wa Kikristo lazima awe

Mnyenyekevu na mwenye kufundishwa: Bibilia inatuambia kwamba mtu mwenye haki, au mtu mwenye hekima, atachukua mafundisho kwa furaha, hata wakati yanamuumiza (Zaburi 141:5; Mithali 9:9, 12:15). Mwanamume mwenye haki anaonyesha nia ya kusahihishwa na Maandiko na tabia ya kupenda na kusikiliza wale ambao wanaweza kumfundisha kutoka kwa Maandiko.

Mwaaminifu: Je! Matendo yake yanakubaliana na maneno yake? Biblia inasema kwamba mtu mwenye haki anajulikana kwa uaminifu katika shughuli zake binafsi na biashara (Waefeso 4:28). Zaidi ya hayo, wakati atakapotoa ahadi, mtu Mkristo anatimiza ahadi yake, hata ikiwa inaumiza (Zaburi 15:2-5). Kwa kifupi, tabia yake inapaswa kuwa moja ya uaminifu.

Mwenye kutojipenda: Biblia inazungumzia hasa waume wakati inawaambia wapende wake zao kama wanavyopenda miili yao wenyewe, kama vile Kristo alivyopenda kanisa na kujitolea Mwenyewe kwa ajili yake (Waefeso 5:25-28). Mpenzi wa kiume wa Kikristo anapaswa kuanza kuonyesha aina hii ya utunzaji na upendo kwa mpenzi wake wa kike kabla ya ndoa. Upendo ni rahisi katika hatua za mwanzo za kimapenzi, lakini mpenzi wa kiume wa Kikristo lazima awe aina ya mtu ambaye tabia na makusudi yake yatakuwa kupenda katika hali zote (1 Yohana 3:18).

Anaweza na tayari kukimu: Biblia inasema kwamba mtu asiyekimu familia yake ni mbaya zaidi kuliko asiyemuumini (1 Timotheo 5:8). Kukimu hakumaanishi kuleta pesa nyingi. Suala ni ikiwa anachukua jukumu la ustawi wa mkewe na watoto wake. Ni muhimu kwa wanawake kuelewa uzito wa aya hii. Mwanaume ambaye hataki kukimu ni ngumu sana kwa mwanamke kumheshimu, na kama mke anajitahidi kumheshimu mumewe, matatizo ya ndoa yataenda zaidi ya vifaa. Heshima ya mwanamke kwa mumewe na upendo wa mwanaume kwa mke wake utegemeana na kutoa maisha kwa ndoa (Waefeso 5:25-32).

Tayari kulinda kwa nguvu: Yote kimwili na kihisia, wanawake uonekana kuwa dhaifu zaidi na umia kwa urahisi zaidi kuliko wanaume. Wanahitaji kueleweka na kulindwa na kutunzwa kwa njia thabiti. Mpenzi wa kiume wa Kikristo mzuri ni mtu ambaye ataangalia na kumtunza mpenzi wake wa kike na kubeba shauku hii ya kumlinda katika ndoa (1 Petro 3:7).

Pia, hapa ni baadhi ya mambo kinyume ya kuzingatia: vitu vya kimwili (1 Yohana 2:15-16; 1 Timotheo 6:10), kudanganya (Methali 12:22, 19:22), kutoaminika kingono (Mhubiri 7:26; Mithali 7) na kutendea mabaya watu wa familia, hasa mama yake (Mithali 15:20, 19:26, 20:20; 23:22). Kawaida, utendaji wa mtu kwa mama yake ni dalili nzuri ya jinsi atakavyomtendea mke wake. Pia, tahadharini na tabia ya bila mantiki au kudhibiti au wivu, kwa kuwa haya mara nyingi husababisha vurugu (Methali 6:34; 27:4).

Hatimaye, mpenzi wa kiume wa Kikristo ni mmoja ambaye mwanamke anafanana. Kwanza, kwa maana ya kiroho — uhusiano wa wanandoa na Mungu unapaswa kuwa sababu kuu katika uhusiano wowote, na wanapaswa kufanana katika suala hilo. Waumini wanaamriwa kuoa waumini wengine (2 Wakorintho 6:14), hivyo hakuna sababu ya kuwa na uhusiano na asiyemuumini. Lakini wanandoa pia wanapaswa kuwa sawa sawa katika mambo ya vitendo zaidi, kuwa na tabia inayolingana, viwango vya bidii sawa, na malengo sawa ya maisha na maslahi. Mambo haya huongeza kwa furaha sana katika uhusiano.

Mbali na haya yote, ikiwa mtu ana hisia nzuri ya ucheshi na thabiti, silika changamfu, hii inatia moyo ajabu sana kwa mkewe. Hakuna mtu anaweza kuwa "juu" wakati wote, lakini mtu ambaye anajulikana kwa amani na furaha ya Roho ni wahi halisi. Maisha ni ngumu, na ndoa ni ngumu, pia. Kutakuwa na nyakati za huzuni, na kutakuwa na migogoro. Kwa sababu hii, mwanadoa mwenye furaha na mwenye kutia moyo ni baraka halisi (Methali 16:24, 17:22; 15:30).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Nipaswa kuangalia nini katika mpenzi wa kiume wa Kikristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries