settings icon
share icon
Swali

Mpango wa wokovu ni nini?

Jibu


Una njaa? Si njaa ya chakula, lakini je, una njaa ya kitu Fulani zaidi maishani? Je, kuna hali Fulani ya kutotosheka ndani yako? Ikiwa iko basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mkate wa kweli. Kila ajaye kwangu hatahisi njaa na aniaminiye hataona kiu” (Yohana 6:35).

Je, umechanganyikiwa? Je, huoni mbele ya maishani mwako? Je, unajihisi kama umeachwa kwenye giza na huoni pa kutokea? Ikiwa hali yako ni kama hiyo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi nuru ya ulimwengu. Anifuataye hatatembea gizani, bali atakuwa na nuru ya uzima” (Yohana 8:12).

Je, unajisikia kama umefungiwa nje ya maisha yako? Je, umejaribu njia nyingi na kutambua ya kwamba kile ulichokitarajia hakipo ndani yake? Je, unatafuta njia ya kufikia maisha makamilifu? Ikiwa haya ndiyo uyatafutayo, Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mlango wa kondoo; aingiaye kupitia mimi ataokolewa. Ataingia na kutoka na kupata malisho” (Yohana 10:9).

Je, watu wengine husababisha kushindwa kwako? Je, uhusiano wako nao umekuwa si wa kina na bila muelekeo? Je, ni kama watu wanakutumia tu kwa manufaa yao? Ikiwa ndiyo hali unayopitia Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema hutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo……. Mimi ndimi mchungaji mwema; Ninajua kondoo wangu na kondoo wangu wananijua” (Yohana 10: 11,14).

Je, unashangazwa na kinachotendeka baada ya maisha haya? Je, umechoshwa na maisha ya kupigania tu vitu vinavyooza na kushika kutu? Je, wakati mwingine maana ya maisha yako huionea shaka? Je, unataka kuishi hata baadaya kufa? Ikiwa haya ndiyo uliyonayo basi Yesu ndiye njia! Yesu alisema, “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Aniaminiye ataishi, hata ajapokufa; na aishiye na kuniamini hata kufa kamwe” (Yohana11:25-26).

Njia ni nini? Ukweli ni nini? Uzima ni nini? Yesu akajibu, “Mimi ndimi njia kweli na uzima.Hakuna afikaye kwa baba bila kupitia kwangu” (Yohana 14:6).

Njaa unayoihisi ni njaa ya kiroho, na inaweza kutoshelezwa na Yesu. Yesu ndiye pekee anaweza kuondoa giza maishani mwako. Yesu ndiye mlango wa maisha ya kutosheka. Yesu ndiye rafiki na mchungaji uliyekuwa ukitafuta. Yesu ndiye uzima wa ulimwengu wa sasa na ujao. Yesu ndiye njia ya wokovu!

Unahisi njaa, kujisikia kama uliyepotea gizani na maisha yako kukosa maana kwa kuwa umetengana na Mungu. Biblia inatuambia ya kwamba sote tumetenda dhambi na kutengana na Mungu (Mhubiri 7:20; Warumi 3:23). Kujihisi kuwa maisha yako hayana maana ni kwa kutokuwepo kwa Mungu maishani mwako. Tuliumbwa tuwe na uhusiano na Mungu. Kwa sababu ya dhambi zetu tumetengwa nje ya uhusiano huo. Vibaya zaidi ni kwamba dhambi zetu zitasababisha kutengwa sasa na hata baada ya ufufuo, milele (Warumi 6:23; Yohana 3:36).

Shida hii inawezaje kutatuliwa? Yesu ndiye njia! Yesu alichukua dhambi zetu (wakorintho wa pili 5:21). Yesu alikufa kwa ajili yetu (Warumi 5:8), akachukua adhabu iliyotupasa sisi. Siku tatu baadaye, yesu akafufuka kutoka kwa wafu kuthibitisha ushindi wake juu ya dhambi na mauti (Warumi 6:4-5). Kwa nini alifanya hivyo? Yesu alijibu swali hilo mwenyewe, “Upendo mkuu hakuna mwingine mwenye nao kama huu, kwamba atoe uhai wake kwa ajili ya rafiki” (Yohana 15:13). Yesu alikufa ili tupate kuishi. Tukiweka imani zetu ndani ya yesu tukiamini kufa kwake kuwa fidia ya dhambi zetu – dhambi zetu zote zinasamehewa na kufutwa. Atahakikisha njaa yetu imetoshelezwa. Mataa ya kimaisha yataangaza tena. Tutapata nafasi ya kufikia maisha ya utimilifu. Tutamjua rafiki yetu mwema na mchungaji pia. Tutajua ya kwamba tutaishi tena hata baada ya kufa – maisha baada ya ufufuo mbinguni milele na Yesu!

“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa mwanawe wa pekee ili kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele” (Yohana 3:16).

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mpango wa wokovu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries