settings icon
share icon
Swali

Je! utaratibu mpya wa ulimwengu ni nini?

Jibu


Utaratibu wa Dunia Mpya na nadharia ya kinjama ambayo hupendekeza kipindi kipya cha historia ambacho kitaleta mabadiliko makuu ulimwenguni kwa usawa wa falme za kidunia. Utaratibu wa Dunia Mpya inakisiwa kujumuisha kundi au makundi ya watu wasomi watakao iongoza dunia chini ya mfumo mmoja wa serikali. Ombi la Utaratibu huu Ulimwengu Mpya uko katika pendekezo lao kukwamua ulimwengu kutoka sogo la vita na mapishano ya kisiasa, na unaahidi kuangamiza umasikini, magonjwa, na njaa. Kusudi lake kukidhi mahitaji na matumaini ya watu wote ulimwenguni kupitia amani ya kiulimwengu.

Pia unaitwa "enzi mpya ya utandawazi," Utaratibu huu wa Ulimwengu mpya unadhaniwa kuondoa hitaji la kuwa na serikali tofauti za ulimwengu. Hii itakamilishwa na kuwekwa kwa mfumo mmoja wa kisiasa au mwili mmoja. Njia moja ya kufanikisha hili ni kwa kuondoa maeneo na mipaka yote inayogwanyisha mataifa ya ulimwengu. Ili kufanya mabadiliko haya yote, inaaminika kwamba Utaratibu wa Ulimwengu Mpya utasisitiza uvumilivu kwa kukuza na kukumbatia tamaduni zingine na maadili na itikadi zao. Lengo lake kuu ni kuwa na hali ya umoja na undugu na watu wote wanaozungumza lugha moja. Malengo yake mengine ni pamoja na matumizi ya sarafu moja, ulimwenguni kote, na pia umoja katika siasa, dini, na maadili. Kama matokeo, njama ya nanadharia inaamini kuwa, ulimwengu utakuwa chini ya kanuni moja, ile ya serikali moja ambayo inaahidi amani ya ulimwengu, kutokuwepo kwa vita, na kuondoa machafuko yote ya kisiasa.

Ingawa inaweza kubalika kuwa mwanadamu anahitaji tumaini ili aweze kustahimili maisha haya na kuwa na amani ya kiakili, tatizo kubwa liko katika mahali ambapo mwanadamu anaweza tafuta tumaini hilo. Maandiko yako wazi kuhusu mambo haya yote. Kama Wakristo, tumeamuriwa kutii na kuheshimu wale wako mamlakani, hii ikiwa ni pamoja na serikali yetu. Walakini tunaweza kuona kuwa kunayo madhara mabaya zaidi ya Utaratibu wa Ulimwengu Mpya, kutoka kwa mtazamo wa kiuchumi na ule wa dini (Warumi 13:1-7; Matendo 5:29).

Shida iliyoko katika kuukubali na kuudhibitisha Utaratibu wa Ulimwengu Mpya ni kwamba hamna serikali yoyote imewai toa, wala itakayo toa tumaini na amani ya kweli kwa mwanadamu. Wakati mwanadamu naigeukia serikali ili watoe amani ya ulimwengu, huwa anakata tamaa na kuwa mtumwa wa ahadi zake za uwongo. Historia imethibitisha mara kwa mara kwamba hakuna ufalme wowote wa ulimwengu uliowahi kuishi, kwa sababu tu ya kasoro zake za asili za uchoyo, ufisadi, na hamu ya nguvu.

Wale wanaotamani kukaribisha Utaratibu wa Ulimwengu Mpya, iwe ni wa kidunia au kidini, watashangazwa na mwamko mpya. Ukweli ni kwamba mafundisho ya uwongo ya dini hayawezi kuleta jamii kamili, haijalishi juhudi bunifu na maarifa ya mwanadamu. Ni mbingu pekee inayoweza kuleta amani na furaha ya kudumu. Biblia inaiweka wazi kwamba vitu vyote ambavyo vimehuzishwa na maisha haya duniani na mateso yake, ni ubatili, havitoshelezi na kifo kitaendelea kuyakabili maisha haya (2 Wakorintho 4:16; Waebrania 9:27). Vile vile ni wazi kuwa mambo haya yote hayajulikani katika mji wa mbinguni (Ufunuo 21:3-7 na Ufunuo 22). Wataondelewa. Naam kuna hitaji la tumaini. Lakini tunahitaji tumaini la mbinguni, sio tumaini la uwongo la Utaratibu wa Ulimwengu Mpya. Tumaini moja kwa waumini wote liko mbinguni pekee (Yohana 14:1-4). Haliko hapa duniani.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! utaratibu mpya wa ulimwengu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries