settings icon
share icon
Swali

Je! Moleki alikuwa nani?

Jibu


Kama ilivyo na historia nyingi za kale, asili halisi ya ibada ya Moleki haiko wazi. Neno Moleki linaaminika kutokana na mlk wa Foinike, ambayo ilirejelea aina ya dhabihu iliyofanywa kuthibitisha au kutenda ahadi. Melekh ni neno la Kiebrania kwa "mfalme." Lilikuwa la kawaida kwa Waisraeli kuunganisha jina la miungu ya kipagani na irabu katika neno la Kiebrania kwa aibu: "bosheth." Hii ndio jinsi mungu wa kike wa uzazi na vita, Astarte, akawa Ashtoreti. Mchanganyiko wa mlk, melekh, na bosheth hutababisha "Moleki," ambayo inaweza kutafsiriwa kama "mfano wa mtawala wa dhabihu la aibu." Pia limeandikwa kama Milcom, Milkim, Maliki, na Moloki. Ashtoreti alikuwa mshirika wake, na ibada ya uasherati ilizingatiwa kuwa aina muhimu ya ibada.

Wafoinike walikuwa kundi huru la watu waliokusanyika ambao waliishi Kanaani (Lebanon ya kisasa, Siria na Israeli) kati ya 1550 KK na 300 KK. Mbali na ibada za kimapenzi, ibada ya Moleki ilijumuisha dhabihu ya watoto, au "kupitisha watoto kwa njia ya moto." Inaaminika kwamba sanamu za Moleki zilikuwa sanamu za chuma pandikizi ya mtu mwenye kichwa cha fahali. Kila sanamu ilikuwa na shimo katika tumbo na labda mikono ilionyooshwa ambao ilifanya aina ya ngazi kuenda kwa shimo. Moto uliwashwa ndani au karibu na sanamu. Watoto waliwekwa katika mikono ya sanamu au shimo. Wakati wanandoa walitoa dhabihu mzaliwa wao wa kwanza, waliamini kuwa Moleki angehakikisha ustawi wa kifedha kwa familia na watoto wa baadaye.

Ibada ya Moleki haikupunguzwa kwa Kanaani. Wamonolithi katika Afrika ya Kaskazini hubeba mchongo "mlk" --mara nyingi huandikwa "mlk'mr" na "mlk'dm," ambayo inaweza kumaanisha "dhabihu ya mwanakondoo" na "dhabihu ya binadamu." Katika Kazikazini mwa Afrika, Moleki aliitwa "Kronos." Kronos alihamia Carthage huko Ugiriki, na mithiolojia yake ilikua kujumuhisha kuwa kwake Titan na baba wa Zeus. Moleki anashirikishwa na wakati mwingine analinganishwa na Ba'al, ingawa neno ba'al lililitumiwa pia kuonyesha mungu yeyote au mtawala.

Katika Mwanzo 12 Abramu alifuata wito wa Mungu wa kuhamia Kanaani. Ingawa sadaka ya binadamu haikuwa kawaida katika Ur asili ya Abramu, ilikuwa imara kabisa katika nchi yake mpya. Mungu baadaye alimuuliza Abramu kumtoa Isaka kama sadaka (Mwanzo 22:2). Lakini kisha Mungu alijitambulisha Mwenyewe kutoka kwa miungu kama Moleki. Tofauti na miungu wenyeji wa Wakanaani, Mungu wa Abramu alichukia dhabihu ya binadamu. Mungu alimwamuru Isaka kuachwa, na Yeye alitoa kondoo dume kuchukua nafasi ya Isaka (Mwanzo 22:13). Mungu alitumia tukio hili kama mfano wa jinsi angeweza baadaye kumtoa Mwanawe mwenyewe kuchukua nafasi yetu.

Zaidi ya miaka mia tano baada ya Abramu, Yoshua aliwaongoza Waisraeli kutoka jangwani kurithi Nchi ya Ahadi. Mungu alijua kwamba Waisraeli walikuwa wachanga na walivutwa kwa urahisi kutoka kumwabudu Mungu mmoja wa kweli (Kutoka 32). Kabla ya Waisraeli hata kuingia Kanaani, Mungu aliwaonya kushiriki katika ibada ya Moleki (Mambo ya Walawi 18:21) na aliwaambia mara kwa mara waharibu tamaduni hizo ziliomwabudu Moleki. Waisraeli hawakusikizai maonyo ya Mungu. Badala yake, walishirikisha ibada ya Moleki kwenye desturi zao wenyewe. Hata Sulemani, mfalme mwenye hekima zaidi, aliyumbishwa na ibada hii na akajenga mahali pa ibada kwa Moleki na miungu mingine (1 Wafalme 11:1-8). Ibada ya Moleki ilifanyika katika "mahali pa juu" (1 Wafalme 12:31) pamoja na korongo nyembamba nje ya Yerusalemu iyoitwa Bonde la Hinomu (2 Wafalme 23:10).

Licha ya jitihada za mara moja na wafalme miungu, ibada ya Moleki haikukomeshwa hadi wakati wa hutumwa wa Waisraeli katika Babeli. (Ingawa dini ya Babiloni ilikuwa ya kuabudu miungu na iliyo na sifa ya unajimu na uaguzi, haikujumuisha dhabihu ya binadamu.) Kwa namna fulani, kutawanyika kwa Waisraeli kwa ustaarabu mkubwa wa kipagani ulifanikiwa mwishowe kuwatakasa wao kwa miungu yao ya uwongo. Wakati Wayahudi waliporudi katika nchi yao, walijitolea tena kwa Mungu, na Bonde la Hinomu likageuzwa kuwa mahali pa kuchoma takataka na miili ya wahalifu waliouawa. Yesu alitumia picha ya mahali hapa-moto wa kuchoma milele, kuteketeza waathiriwa wengi wa watu--kuelezea kuzimu, ambapo wale wanaomkataa Mungu watateketea kwa milele (Mathayo 10:28).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Moleki alikuwa nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries