settings icon
share icon
Swali

Nini maana na umuhimu wa Mlo wa Mwisho?

Jibu


Mlo wa mwisho ni kile tunachoita chakula cha mwisho Yesu alikula pamoja na wanafunzi Wake kabla ya kusalitiwa na kukamatwa Kwake. Mlo wa Mwisho umeandikwa katika Injili ya Ufupisho (Mathayo 26:17-30, Marko 14:12-26; Luka 22:7-30). Ilikuwa zaidi ya chakula cha mwisho cha Yesu; Ilikuwa ni chakula cha Pasaka, pia. Moja ya wakati muhimu wa Mlo wa Mwisho ni amri ya Yesu ya kukumbuka yale aliyokuwa karibu kufanya kwa niaba ya watu wote: kumwaga damu Yake msalabani na kulipa deni la dhambi zetu (Luka 22:19).

Mbali na kutabiri mateso na kifo Chake kwa ajili ya wokovu wetu (Luka 22:15-16), Yesu pia alitumia Mlo wa Mwisho ili kutia moyoni Pasaka na maana mpya, kuanzisha Agano Jipya, kuanzisha amri kwa kanisa, na kutabiri Petro kumkataa Yeye (Luka 22:34) na usaliti wa Yuda Iskarioti (Mathayo 26:21-24).

Mlo wa mwisho ulileta kanuni ya Agano la Kale ya sikukuu ya Pasaka katika utimizaji wake. Pasaka ilikuwa tukio takatifu hasa kwa Wayahudi kwa kuwa liliwakumbusha wakati ambapo Mungu aliwaokoa kutokana na tauni ya kifo cha kimwili na kuwatoa utumwa katika Misri (Kutoka 11:1-13:16). Wakati wa Mlo wa Mwisho na mitume Wake, Yesu alichukua alama mbili zilizohusishwa na Pasaka na kuzitia moyoni na maana mpya kama namna ya kukumbuka dhabihu Yake, ambayo inatuokoa kutoka kifo cha kiroho na kutuokoa kutoka utumwa wa kiroho: "Akapokea kikombe, akashukuru, akasema, Twaeni hiki, mgawanye ninyi kwa ninyi; Maana nawaambia ya kwamba tangu sasa sinywi mazao ya mzabibu hata ufalme wa Mungu utakapokuja. Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, [Huu ndio mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]"(Luka 22:17-20) .

Maneno ya Yesu wakati wa Mlo wa Mwisho kuhusu mkate usiotiwa chachu na kikombe inarudia kile alichosema baada ya kuwalisha 5,000: "Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. . . . Mimi ndimi mkate wa uzima ulioshuka kutoka mbinguni; mtu akila mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitatoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu. . . . Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chukala cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli"(Yohana 6:35, 51, 54-55). Wokovu huja kupitia Kristo na dhabihu ya mwili Wake wa kimwili msalabani.

Pia wakati wa Mlo ya Mwisho, Yesu alifundisha kanuni za utumishi na msamaha vile aliosha miguu ya wanafunzi Wake: "Lakini kwenu ninyi sivyo; bali aliye mkubwa kwenu na awe kama aliye mdogo; na mwenye kuongoza kama yule atumikaye. Maana aliye mkubwa ni yupi? Yeye aketiye chakulani, au yule atumikaye? Siye yule aketiye chakulani? Lakini mimi kati yenu ni kama atumikaye"(Luka 22:26-27; Yohana 13:1-20).

Mlo wa mwisho leo unakumbukwa wakati wa Meza ya Bwana, au ushirika (1 Wakorintho 11:23-33). Biblia inafundisha kwamba kifo cha Yesu kilikuwa mfano katika sadaka ya Pasaka (Yohana 1:29). Yohana anasema kwamba kifo cha Yesu kinafanana na dhabihu ya Pasaka kwa kuwa mifupa yake haikuvunjika (Yohana 19:36, tazama Kutoka 12:46). Na Paulo akasema, "Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo" (1 Wakorintho 5:7). Yesu ni utimilifu wa Sheria, ikiwa ni pamoja na sikukuu za Bwana (Mathayo 5:17).

Kwa kufanana hasa, chakula cha Pasaka kilikuwa sherehe ya familia. Hata hivyo, katika Chajio cha Mwisho, mitume walikuwa pekee pamoja na Yesu (Luka 22:14), ambayo inaonyesha kuwa chakula hiki kilikuwa maana maalum kwa kanisa, ambayo mitume walikuwa msingi (Waefeso 2:20). Wakati Chakula cha Mwisho kilikuwa na maana kwa Wayahudi, ilikuwa imeundwa kwa kanisa pia. Leo hii Meza ya Bwana ni moja ya maagizo mawili yayotekelezwa na kanisa.

Mlo wa Mwisho ulijengwa katika Agano la Kale hata vile inaashiria Mpya. Yeremia 31:31 aliahidi Agano Jipya kati ya Mungu na Israeli, ambapo Mungu alisema, "Nitatia sheria yangu ndani yao, na katika mioyo yao nitaiandika. Nami niitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu "(Yeremia 31:33). Yesu alifanya rejeleo la moja kwa moja kwa Agano Jipya hili wakati wa Mlo wa mwisho: "kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu" (Luka 22:20). Mpango mpya wa Mungu ulikuwa juu ya upeo wa macho. Kwa neema ya Mungu, Agano Jipya linahusu zaidi ya Israeli; kila mtu aliye na imani katika Kristo ataokolewa (ona Waefeso 2:12-14).

Mlo wa Mwisho ulikuwa ni tukio muhimu na ulitangaza hatua ya kugeuka katika mpango wa Mungu kwa ulimwengu. Kwa kulinganisha kusulubiwa kwa Yesu kwenye sikukuu ya Pasaka, tunaweza kuona kwa urahisi asili ya ukombozi wa kifo cha Kristo. Kama ilivyoashiriwa na dhabihu ya Pasaka ya awali katika Agano la Kale, kifo cha Kristo kinalipia dhambi za watu Wake; Damu yake inatukomboa kutoka kifo na inatuokoa kutoka utumwa. Leo, Meza ya Bwana ni wakati waumini wanatafakari juu ya dhabihu kamili ya Kristo na kujua kwamba, kupitia imani yetu katika kumpokea, tutakuwa pamoja Naye milele (Luka 22:18, Ufunuo 3:20).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini maana na umuhimu wa Mlo wa Mwisho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries