settings icon
share icon
Swali

Je, ni makosa kuwa Mkristo kwa siri ili kuhifadhi maisha yako mwenyewe?

Jibu


Je, ni makosa kuishi maisha kama Wakristo wa siri kwa hofu ya kulipiza kisasi au hata kifo? Je! Wakristo wanapaswa kuwa tayari kufa kwa kukiri jina la Yesu? Je, tunapaswa kuweka imani yetu siri ili kuhifadhi maisha yetu? Hili ndilo swali ambalo ni nadharia tete tu kwa Wakristo katika sehemu nyingi za dunia, na mateso mabaya zaidi ambayo wanaweza kupokea kuwa dhihaki na / au matusi. Hata hivyo, kwa Wakristo katika sehemu fulani za dunia, swali hili ni la kweli na la utendaji-maisha yao halisi yamo hatarini. Ni jambo moja kutokuwa jasiri kama unavyopenda ili kulinda maisha yako mwenyewe na / au maisha ya familia yako. Ni jambo lingine kabisa kufanya maisha yako mwenyewe kuwa kipaumbele zaidi kuliko kuhudumia, kuheshimu, kuabudu, na kumtii Kristo. Kwa hivyo, na hiyo kusemwa, je, ni makosa kuweka imani yako ndani ya Kristo siri?

Yesu mwenyewe anatupa jibu: "Basi,kila mtu atakayenikiri mbele ya wati, nami nitamkiri mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Bali mtu yeyote atakayenikana mbele ya watu, nami nitamkana mbele za Baba yangu aliye mbinguni. Msidhani ya kuwa nimekuja kuleta Amani duniani; la! Sikuja kuleta Amani, bali upanga"(Mathayo 10: 32-34). Kristo aliweka wazi kwetu kwamba "Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi niliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia" (Yohana 15: 18-19). Kwa hivyo, wakati inaeleweka kwa mtu kuweka imani yake katika Kristo siri ili kuokoa maisha yake, kwa Mkristo, imani ya siri sio chaguo.

Katika kifungu hapo juu, neno "ulimwengu" linatoka kwa Kigiriki kosmos. Inarejelea uovu, mfumo mbaya wa ulimwengu wa kutomcha Mungu, watu wasio na maadili ambao mioyo na akili zao zinathibitiwa na Shetani (Yohana 14:30, 1 Yohana 5:19, Waefeso 2: 1-3). Shetani anamchukia Mungu. Pia huchukia wale wanaomfuata Kristo. Wakristo ni kipaumbele cha ghadhabu ya Shetani. Lengo lake ni "kuwaangamiza" (1 Petro 5: 8; Waefeso 6:11). Hatupaswi kushangaa kwamba watawala wa ulimwengu huwachukia waumini tu kwa sababu sisi "si wa ulimwengu." Sababu kwa nini Wakristo wanateswa na kuuawa kila siku kwa kukiri kwao kwa Kristo ni kwamba maisha yetu ya kiungu hutumikia kuhukumu matendo mabaya ya ulimwengu huu (Mithali 29:27). Imekuwa njia hii tangu mwanzo wa wakati na mauaji ya kwanza yaliyoandikwa wakati Kaini alimuua Abeli (Mwanzo 4: 1-8). Kwa nini Kaini alifanya hivyo? "Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya na ndugu yake yalikuwa ya haki" (1 Yohana 3:12). Vivyo hivyo, ulimwengu leo huwashabikia wale wanaofanya mabaya (Warumi 1:32) na wanawahukumu wale watakaoishi kwa haki.

Ujumbe mwingine ambao Yesu alileta ulimwenguni: "Wakati huo watawasaliti (ulimwengu) ninyi mpate dhiki, nao watawaua; nanyi mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa yote kwa ajili ya jina langu" (Mathayo 24: 9). Yesu ametuahidi hivi: nyakati za mwisho Wakristo watateswa sana na dunia hii isiyo ya Mungu. Tutatusiwa, tutatukanwa, na tutalaaniwa. Neno "watawasaliti" linatokana na neno la Kiyunani linamaanisha "kutoa," kama vile kukamatwa na polisi au jeshi (Mathayo 4:12). Wengi watauliwa. "Tutachukiwa na mataifa yote" kwa ajili ya jina lake. Katika kifungu sambamba cha Marko, Yesu anasema, "Nanyi jihadharini nafsi zenu; maana watawapeleka ninyi mabarazani; na katika masinagogi mtapigwa; nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, kuwa ushuhuda kwao"(Marko 13: 9). Tunaposhuhudia leo ulimwenguni pote, kutambuliwa kwa jina la Kristo kutatugharimu uhuru wetu, haki zetu, heshima yetu, na wakati mwingine maisha yetu.

Wakristo wana mamlaka kutoka kwa Kristo "Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu" (Mathayo 28:19). Paulo anaelezea maelekezo ya Kristo kwa swali hili: "Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, ni mizuri kama ni miguu yao wahubirio habari ya mema!"(Warumi 10: 14-15). Ili injili itangazwe, hata katika pembe za giza duniani, mtu lazima atangaze. Madhumuni yetu duniani ni kuwa mwanga wa dunia na chumvi ya dunia, kuwaambia wengine habari za kuokoa maisha za Yesu Kristo. Ndiyo, wakati mwingine tunahatarisha kuteswa kwa kufanya hivyo, na wakati mwingine tunahatarisha maisha yetu. Lakini tunajua ni mapenzi ya Mungu kwamba tushiriki ukweli Wake na wengine, na sisi pia tunajua Yeye ni mwenye nguvu ya kutukinga mpaka ujumbe wetu duniani ukamilike.

Kuishi kwa ajili ya Kristo katika ulimwengu huu inaweza kuwa ngumu, hata ukatili. Dunia hii sio nyumbani kwetu. Dunia ni uwanja wa vita. Majaribio ya maisha ni zana ambazo Mungu anatumia kwa kutujenga na kutufanya zaidi kama Yesu. Ni katika nyakati hizo za giza ambazo tunaangalia kwa Kristo na kuruhusu Nguvu Zake zifanye kazi ndani yetu. Kabla ya kupaa kwake mbinguni, Yesu alitupa amri yake ya mwisho ya kueneza injili kwa ulimwengu. Pamoja na hilo alitupa pia ahadi yake ya mwisho. "Na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:20).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni makosa kuwa Mkristo kwa siri ili kuhifadhi maisha yako mwenyewe?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries