settings icon
share icon
Swali

Je! Mkristo anapaswa kutazamaje utajiri?

Jibu


Mtazamo wa Mkristo kuhusu utajiri unapaswa kutolewa kutoka kwa Maandiko. Kuna nyakati nyingi katika Agano la Kale kwamba Mungu alitoa utajiri kwa watu Wake. Sulemani aliahidiwa utajiri na akawa tajiri zaidi ya wafalme wote wa dunia (1 Wafalme 3:11-13; 2 Mambo ya Nyakati 9:22); Daudi alisema katika 1 Mambo ya Nyakati 29:12, "Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyoyte." Ibrahimu (Mwanzo 17-20), Yakobo (Mwanzo 30-31), Yusufu (Mwanzo 41), Mfalme Yehoshafati (2 Mambo ya Nyakati 17:5), na wengine wengi walibarikiwa na Mungu na utajiri. Hata hivyo, Wayahudi walikuwa watu wateule na ahadi na tuzo za dunia. Walipewa ardhi na utajiri wote uliokuwa nayo.

Katika Agano Jipya, kuna kiwango tofauti. Kanisa halikupewa ardhi au ahadi ya utajiri. Waefeso 1:3 inatuambia, "Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa Baraka zote za rohoni, katika ulimwengu war oho, ndani yake Kristo." Kristo alizungumza katika Mathayo 13:22 kuhusu mbegu ya Neno la Mungu kuanguka miongoni mwa miiba na "udanganyifu wa mali hulisonga lile neno; likawa halizai." Hii ndiyo kumbukumbu ya kwanza ya utajiri wa kidunia katika Agano Jipya. Kwa wazi, hii si picha nzuri.

Katika Marko 10:23, "Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu!" Haikuwa haiwezekani — kwa kuwa vitu vyote vinawezekana kwa Mungu-lakini itakuwa "ngumu." Katika Luka 16:13, Yesu alisema juu ya "ukwasi" (neno la Kiaramu kwa "utajiri"): "Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali." Tena, maneno ya Yesu yanaonyesha utajiri kama ushawishi mbaya juu ya kiroho na moja ambao unaweza kutuzuia kutoka kwa Mungu.

Mungu anaongea juu ya utajiri wa kweli anayetuletea leo katika Warumi 2:4: "Au waudharau wingi wa wema wake na ustahimili wake na uvumilivu wake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvuta upate kutubu?" Huu ndio utajiri unaoleta uzima wa milele. Tena, hii inaletwa katika Warumi 9:23-24 "Tena, ili audhihirishe wingi wa utukufu wake katika vile vyombo vya rehema, alivyovitengeneza tangu zamani vipate utukufu; ndio sisi aliotuita, si watu wa Wayahudi tu, ila na watu wa mataifa pia?" Pia Waefeso 1:7 "Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake." Akizungumzia Mungu kuwapa rehema, Paulo anamsifu Mungu katika Warumi 11:33: "Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mumgu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazitafutikani!" Mkazo wa Agano Jipya ni utajiri wa Mungu ndani yetu: "Mjue tumaini la mwito"(Waefeso 1:18). Mungu kwa kweli anataka kuonyesha utajiri wake ndani yetu mbinguni: "Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu"(Waefeso 2:6-7).

Utajiri ambao Mungu anataka kwa sisi: "Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani" (Waefeso 3:16). Mstari mkubwa kwa waumini wa Agano Jipya kuhusu utajiri ni Wafilipi 4:19: "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu." Maneno haya yaliandikwa na Paulo kwa sababu Wafilipi walikuwa wametenga zawadi za dhabihu za kutunza mahitaji ya Paulo.

1 Timotheo 6:17 inatoa onyo kwa matajiri: "Walio matajiri wa ulimwengu wa sasa uwaagize wasijivune, wala wasiutumainie utajiri usio yakini, bali wamtumaini Mungu atupaye vitu vyote kwa wingi ili tuvitumie kwa furaha." Yakobo 5:1-3 inatupa onyo lingine juu ya utajiri uliopatikana vibaya: "Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia. Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo. Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiweka akiba katika siku za mwisho." Wakati wa mwisho utajiri huo unatajwa katika Biblia ni katika Ufunuo 18:17, akizungumzia uharibifu mkubwa wa Babeli:" Katika saa moja utajiri mwingi namna hii umekuwa ukiwa!"

Kwa muhtasari, Israeli ilipewa ahadi na tuzo za duniani kama watu wateule wa Mungu duniani. Mungu alitoa mifano mingi na aina na ukweli kupitia kwao. Watu wengi wanatamani kuchukua baraka zao, lakini sio laana zao. Hata hivyo, katika maendeleo ya ufunuo, Mungu amefunua kwa njia ya Yesu Kristo huduma bora zaidi: "Lakini sasa amepata huduma iliyo bora Zaidi, kwa kadiri alivyo mjumbe wa agano lililo bora, lililoamriwa juu ya ahadi zilizo bora" (Waebrania 8:6).

Mungu hahukumu mtu yeyote kwa kuwa na utajiri. Utajiri huja kwa watu kutoka vyanzo vingi, lakini anatoa onyo kali kwa wale wanaoutafuta zaidi kuliko wanavyomtafuta Mungu na kuutumamini zaidi kuliko Mungu. Tamaa yake kubwa sana ni kwa sisi kuweka mioyo yetu juu ya mambo ya mbinguni na si juu ya mambo ya duniani. Hii inaweza kuonekana kuwa ya juu sana na isiyoweza kupatikana, lakini Paulo aliandika, "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" (Wafilipi 4:13). Siri ni kumjua Kristo kama Mwokozi na kuruhusu Roho Mtakatifu kufuata mawazo na mioyo yetu kwa Yake (Warumi 12:1-2).

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mkristo anapaswa kutazamaje utajiri?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries