settings icon
share icon
Swali

Mkristo anapaswa kuwa na mtizamo gani kwa uraibu?

Jibu


Neno uraibu lina maana mbili za msingi. Ya kwanza ni "hali ya kutegemea kimwili au kisaikolojia tabia inayoletwa na mihadarati." Wale ambao wamevumiwa au "wamepewa divai nyingi" (Tito 1: 7; 2: 3), "walevi" (1 Timotheo 3: 3) au "wanywaji" (1 Timotheo 3: 8) hawatakiwi kufundisha au kushikilia nafasi ya mamlaka katika kanisa. Ni dhahiri kuwa uongozi wa kanisa unahitaji kuwa wa busara na kujidhibiti ili, kwa mfano wao, waweze kufundisha wengine kuwa sawia, kwa maana tunajua kwamba "walevi. . . hawatairithi Ufalme wa Mungu" (1 Wakorintho 6:10). Waumini hawapaswi kutegemea pombe, na hii pia itatumika kwa uraibu wa mihadarati, yaani madawa ya kulevya, ponografia, kamari, ulafi, tumbaku, nk.

Ufafanuzi wa pili wa kulevya ni "hali ya kuwa na mshiko au kushiriki katika kitu cha kawaida au kwa kulazimisha." Hii inasungumzia hali yoyote isiyo ya kawaida (kwa Mkristo, angalau) uvumilivu na kitu chochote isipokuwa Mungu: michezo, kazi, ununuzi na / au kupata "wengine," hata familia au watoto. Tunapaswa "mpende Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote" (Kumbukumbu la Torati 6: 5). Hii ni kulingana na Yesu ambayo ni amri ya kwanza na kubwa (Mathayo 22: 37-38). Basi tunaweza kumaliza kwa kusema, kwamba uraibu kwa kitu chochote kile isipokuwa Mungu Mwenyewe ni kibaya. Mungu anafaa kuwa kutafutwa katika tabia zetu. Kujihusisha na chochote kile hutuweka mbali na Yeye na haimpendezi. Yeye peke yake anastahili umakini wetu wote, upendo, na huduma yetu kamili. Kutoa vitu hivi kwa kitu chochote au mtu mwingine ni ibada ya sanamu.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mkristo anapaswa kuwa na mtizamo gani kwa uraibu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries