settings icon
share icon
Swali

Inawezekana kuwa Mkristo shoga?

Jibu


"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti, wala wevi, wala watamanio, wala walevi, wala watukanaji, wala wanyang'anyi"(1 Wakorintho 6: 9-10). Kuna mwelekeo wa kutangaza ushoga kama dhambi mbaya Zaidi kati ya dhambi zote. Ingawa haiwezi kukanwa, kuongea Kibiblia, ushoga ni uovu na usio wa kawaida (Warumi 1: 26-27), kwa maana hakuna mahali Biblia inaelezea ushoga kama dhambi isiyosamehewa. Wala Biblia haifundishi kwamba ushoga ni dhambi ambayo kamwe Wakristo hawawezi kupambana nayo.

Labda hiyo ni maneno kuu katika swali la kama inawezekana kuwa Mkristo shoga: "kupambana dhidi." Inawezekana Mkristo kupambana na majaribu ya ushoga. Mashoga wengi ambao wanakuwa Wakristo wanaendelea kukabiliana na hisia na tamaa za ushoga. Baadhi ya wanaume na wanawake ambao wanavutiwa na watu wa jinsi tafauti wamepata "spaki" ya maslahi ya ushoga wakati fulani katika maisha yao. Iwapo tamaa na majaribu haya yapo au hayapo hayatambui kama mtu ni Mkristo. Biblia iko wazi kuwa hakuna Mkristo hana dhambi (1 Yohana 1: 8,10). Wakati dhambi / majaribu maalum hutofautiana kutoka kwa Mkristo mmoja hadi mwingine, Wakristo wote wanakabiliana na dhambi, na Wakristo wote wakati mwingine hushindwa katika makabiliano hayo (1 Wakorintho 10:13).

Kile kinachofautisha maisha ya Mkristo kutoka maisha ya asiye Kikristo ni mapambano dhidi ya dhambi. Maisha ya mkristo ni safari ya kuendelea ya kushinda "matendo ya mwili" (Wagalatia 5: 19-21) na kuruhusu Roho wa Mungu kuzalisha "matunda ya Roho" (Wagalatia 5: 22-23). Ndiyo, Wakristo hufanya dhambi, wakati mwingine kwa kutisha. Kwa kusikitisha, wakati mwingine Wakristo hawatofautishwi na wasio Wakristo. Hata hivyo, Mkristo wa kweli atatubu kila wakati, hatimaye atarudi kwa Mungu, na daima ataanza mapambano dhidi ya dhambi. Lakini Biblia haitoi msaada kwa wazo kwamba mtu ambaye anarudiarudia na kwa kutotubu anashiriki katika dhambi kwa kweli anaweza kuwa Mkristo. Angalia 1 Wakorintho 6:11, "Na baadhi yenu mlikuwa watu wa namna hii; lakini mlioshwa, lakini mlitakaswa, lakini mlihesabiwa haki katika jina la Bwana Yesu Kristo, na katika Roho wa Mungu wetu."

Wakorintho wa Kwanza 6: 9-10 huorodhesha dhambi ambazo, ikiwa kujiingiza kwa kuendelea, tambua mtu kama asiyekombolewa-sio Mkristo. Mara nyingi, ushoga huchaguliwa kutoka kwenye orodha hii. Ikiwa mtu anakabiliana na majaribu ya ushoga, mtu huyo anadhaniwa kuwa hajaokoka. Ikiwa mtu kwa kweli anajihusisha na vitendo vya ushoga, mtu huyo ni dhahiri kuwa hajaokoka. Hata hivyo, mawazo sawa hayafanyiki, angalau si kwa mkazo sawa, kuhusu dhambi nyingine katika orodha: uzinzi (ngono kabla ya ndoa), ibada ya sanamu, uzinzi, wizi, wivu, ulevi, unyanyasaji, na udanganyifu. Haifuati utaratibu, kwa mfano, kutangaza wale walio na hatia ya ngono kabla ya ndoa kama "Wakristo wasiotii," huku wakitangaza kwa hakika mashoga sio Wakristo.

Inawezekana kuwa Mkristo shoga? Ikiwa maneno "Mkristo shoga" inamaanisha mtu anayekabiliana dhidi ya tamaa na majaribu ya ushoga — ndiyo, "Mkristo shoga" inawezekana. Hata hivyo, maelezo "Mkristo shoga" sio sahihi kwa mtu kama huyo, kwa kuwa yeye hatamani kuwa shoga, na anajitahidi dhidi ya majaribu. Mtu kama huyo si "Mkristo shoga," bali ni Mkristo anayejitahidi, kama vile kuna Wakristo wanaojitahidi na uzinzi, uongo, na kuiba. Ikiwa maneno "Mkristo shoga" yanamaanisha mtu ambaye anashiriki, anarudiarudia na hatubu maisha ya ushoga- hapana, haiwezekani kwa mtu huyo kuwa Mkristo wa kweli.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Inawezekana kuwa Mkristo shoga?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries