settings icon
share icon
Swali

Mimi ni Mkristo ambaye amezoea kuvuta sigara. Ninawezaje kuacha?

Jibu


Wakristo wengi ambao wamekuwa wanavutaji sigara wakumbwa kwa miaka mingi wanaweza kuhisi kwa urahisi taabu ya mtu yeyote anayejaribu kuacha kuvuta sigara na anaweza kuelewa kikamilifu mapambano wanaokabiliana nayo wale wanaotamani kuacha. Kuacha si rahisi kwa hakika, lakini inaweza kufanyika. Wavutaji wengi wa furushi mbili kwa siku sasa wako huru na uvutaji na wanaweza kuthibitisha ukweli kwamba inaweza kufanywa wakati tunageuza suala hili kwa Mungu na kutegemea nguvu na uwezo Wake.

Kuna sababu nyingi za kuacha tabia ya kuvuta sigara ni wazo nzuri kwa kila mtu, lakini hasa kwa Wakristo. Ikiwa Mkristo hana uhakika ni kwa nini aache kuvuta sigara na kutokuwa na hakika ikiwa au sio kufanya dhambi, makala yetu yenye mada "Je! Ni mtazamo gani wa Mkristo kuhusu kuvuta sigara? Je! Kuvuta sigara ni dhambi?" Itakuwa mahali pazuri kuanzia. Sababu zilizotajwa katika makala zinapaswa kutoa msukumo mkubwa kwa mvutaji sigara ambaye bado hana uhakika ikiwa ataacha au kutoacha. Wale ambao wameamua kuacha kuvuta sigara wanapaswa kuelewa kwamba, kuzungumza kwa huruma, kuacha kuvuta sigara ni moja ya mambo magumu zaidi kufanya. Utafiti umeonyesha kwamba nikotini ya kuzoesha sana, hata ya kuzoesha zaidi kuliko heroini, wengine wanasema.

Lakini asili ya kuzoesha mahitaji ya nikotini haipaswi kutuvunja moyo. Paulo anatuambia, "Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu" (Wafilipi 4:13). Ingawa ni ngumu, na uondoaji kamili unaweza kuchukua muda kabla ya mtu kuwa na haja tena ya sigara, kama Wakristo tunapaswa kumtazama Mungu ambaye msaada wetu hutoka. Tuweke mioyo yetu juu ya mambo ya juu na kuomba Bwana atatupa nguvu za kupata ushindi katika jaribio hili. Watu wengine humwaacha Bwana nje katika jaribio lao la kushinda tabia mbaya, na hilo ni kosa kubwa. Maombi husaidia katika aina hizi za hali, na tunaalikwa kuchukua matatizo yetu moja kwa moja kwenye kiti cha enzi cha Mungu na kwa Yeye anaweza kuyatatua (Waebrania 4:16).

Kutegemea nguvu za Roho Mtakatifu haimaanishi kwamba vifaa vya afya vya kusimamisha uvutaji sigara haviwezi kutumika pia. Wengi wamepata usaidizi mkubwa kwa njia ya plasta, fizi, tembe, nk. Baada ya maombi na kushauriana na daktari, ikiwa Mungu anakupa amani kuhusu kutumia msaada wa dawa za kusimamiza uvutaji sigara, hakuna sababu ya kibiblia kwa nini huwezi.

Mungu ametangaza kwamba neema yake ni ya kutosha (2 Wakorintho 12:9). Ambapo sisi ni dhaifu, Yeye ni mwenye nguvu. Tamaa yetu kwa sigara itapunguzwa vile tutakavyokua na kupata nguvu katika Bwana. Uwezo wa Mungu utafanya kazi ndani yetu ili kupunguza shinikizo la kuvuta sigara, yote kwa utukufu Wake. Mungu atatupa nguvu ya kuweka Kristo kwanza na sisi wenyewe mwisho. Katika hili tutapata kwamba kile tunachoacha kitakuwa zaidi ya fidia kwa kile tunachopata.

Kuzamizwa katika Neno la Mungu ni muhimu kwa Mkristo ambaye anatamani kuacha kuvuta sigara. Hapa ni baadhi ya mistari ya kukariri na kutafakari, mistari ambayo imesaidia wengine kupata ushindi juu ya kuzoea kuvuta sigara:

Yohana 8:32, "Tena mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru."

Yohana 8:36, "Basi Mwana akiwaweka huru, mtakuwa huru kweli kweli."

1 Wakorintho 6:19-20, "Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe; maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu."

Waebrania 12:1-2, "Basi na sisi pia, kwa kuwa tunazungukwa na wingu kubwa la mashahidi namna hii, na tuweke kando kila mzigo mzito, na dhambi ile ituzingayo kwa upesi; na tupige mbio kwa saburi katika yale mashondano yaliyowekwa mbele yetu, tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza Imani yetu."

Warumi 13:14, "Basi mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake."

1 Wakorintho 9:27, "Bali nautesa mwili wangu na kuutumikisha; isiwe, nikiisha kuwahubiri wengine, mwenyewe niwe mtu wa kukataliwa."

Mathayo 19:26, "Kwa wanadamu jambo hilo haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana."

Yohana 15: 5, "Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yeke, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi humwezi kufanya neno lo lote."

Waefeso 4:22, "Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya."

Wafilipi 4:13, "Niyaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu."

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mimi ni Mkristo ambaye amezoea kuvuta sigara. Ninawezaje kuacha?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries