settings icon
share icon
Swali

Je! Mimi ni wa Kanisa la Siku za Mwisho, kwa nini napaswa kuzingatia kuwa Mkristo?

Jibu


Mtu yeyote kutoka dini yoyote-au hakuna dini kabisa-ambaye anauliza, "Kwa nini napaswa kuzingatia kuwa Mkristo?" inapaswa kuzingatia madai ya Ukristo.Kwa mfuasi wa kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho anauliza swali hili, tofauti kati ya mafundisho ya Ukristo wa Kibiblia na falsafa ya Watakatifu wa Siku za Mwisho inapaswa kuwa sehemu ya msingi wa kuulizia. Ikiwa Biblia ni Neno la Mungu (Joseph Smith na Brigham Young wote wawili waliamini hili), basi imani za msingi za Mormonism na Watakatifu wa Siku za Mwisho (ikiwa imani hizo ni za kuaminika) lazima ziwe thabiti na kile Biblia inafundisha.Hata hivyo, kuna kutofautiana, na tutaangalia maeneo manne ya tofauti kati ya Mormonism na Biblia.

1) Mfuasi wa kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho ambaye anazingatia kuwa Mkristo anapaswa kuelewa kwamba Mormonism inafundisha kutegemea juu ya vyanzo vya ziada vya kibiblia. Biblia inafundisha kwamba ni ya kutosha kwa mafundisho katika maisha ya Kikristo (2 Timotheo 3:16) na kwamba Mungu alilaani bayana mtu yeyote aliyedai mamlaka ya kuongezea kile ambacho Mungu alikuwa amefunua katika Biblia. Kwa maneno mengine, Mungu alitamka ufunuo Wake ulioandikwa kuwa kamili (Ufunuo 22: 18-19). Kwa hivyo, hakuna sababu ya Mungu kuandika zaidi. Mungu ambaye anaandika Kitabu Chake, anasema ni kamili, na kisha baadaye anagundua kwamba alisahau jambo fulani ikiwa hakuwa na mpango kwa siku zijazo au hakujua vya kutosha kuandika kila kitu mara ya kwanza. Mungu kama huyo si Mungu wa Biblia. Bado, Mormonism inafundisha kwamba Biblia ni moja tu ya vyanzo vinne vya mamlaka, vingine vitatu ni Kitabu cha Mormon, Mafundisho na Maagano, na Lulu la Bei kubwa. Havi vitatu vinatoka kwa mtu mmoja ambaye alivitangaza kuwa vimeongozwa na Mungu licha ya kuwa kinyume na Biblia, maandiko ya kwanza na ya kweli tu yaliyoongozwa na Mungu. Kuongezea nyongeza za maandishi kwenye Maandiko na kuiita kuwa imeongozwa ni kupingana na Mungu.

2) Mfuasi wa kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho ambaye anazingatia kuwa Mkristo anapaswa kuelewa kwamba Mormonism inaendeleza mungu mdogo. Mormonism inafundisha kwamba Mungu hakuwa daima Mwenye Ukuu juu ya ulimwengu (Mafundisho ya Watakatifu wa siku za mwisho, uk. 321) lakini alipata hali hiyo kupitia maisha ya haki (Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, uk. 345). Lakini ni nani anayefafanua haki? Kiwango hiki kinaweza kuja kutoka tu kwa Mungu Mwenyewe. Kwa hivyo, mafundisho ya kuwa Mungu akawa Mungu kwa kufikia viwango vilivyowekwa tayari kutoka kwa Mungu ni kinyume. Zaidi ya hayo, mungu ambaye sio wa milele na si wa uwepo wake peke yake sio Mungu wa Biblia. Bibilia inafundisha kwamba Mungu ni wa uwepo wake Mwenyewe na wa milele (Kumbukumbu la Torati 33:27, Zaburi 90: 2, 1 Timotheo 1:17) na Yeye haumbwi lakini Muumbaji Mwenyewe (Mwanzo 1, Zaburi 24: 1, Isaya 37:16; Wakolosai 1: 17-18).

3) Mfuasi wa Kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho ambaye anazingatia kuwa Mkristo anapaswa kuelewa kwamba Mormonism inafundisha mtazamo wa shinikizo za ubinadamu ambao unatofautiana kabisa na mafundisho ya kibiblia. Mormonism inafundisha kwamba mwanadamu yeyote anaweza pia kuwa mungu (Mafundisho ya Nabii Joseph Smith, uk. 345-354; Mafundisho na Maagano 132: 20). Hata hivyo Biblia inafundisha mara kwa mara kwamba sisi sote kiasili ni wenye dhambi (Yeremia 17: 9; Warumi 3: 10-23; 8: 7) na kwamba Mungu peke yake ni Mungu (1 Samweli 2: 2; Isaya 44: 6, 8; 46: 9). Isaya 43:10 imeandika maneno ya Mungu mwenyewe: "Kabla yangu hakuumbwa Mungu aweye yote, wala baada yangu mimi hatakuwapo mwingine." Jinsi Mormonism inaweza dai kuwa watu watakuwa miungu katika uso wa ushahidi wa ajabu wa maandiko kama hayo ni ushuhuda wa kina cha tamaa ya mtu ya kunyang'anya nafasi ya Mungu, tamaa iliyozaliwa ndani ya moyo wa Shetani (Isaya 14:14) na kupitishwa na yeye kwa Adamu na Hawa katika Bustani (Mwanzo 3: 5). Tamaa ya kuutwaa kiti cha enzi cha Mungu-au kugawana-huainisha wote ambao ni wa baba yao shetani, ikiwa ni pamoja na Mpinga Kristo, ambaye atafanya tamaa sawa katika nyakati za mwisho (2 Wathesalonike 2: 3-4). Katika historia, dini nyingi za uongo zimekuwa na tamaa ile ile ya kuwa Mungu. Lakini Mungu anasema hakuna Mungu ila Yeye, na tusithubutu kuenda kinyume Naye.

4) Mfuasi wa Kanisa la Watakatifu wa Siku za Mwisho ambaye anazingatia kuwa Mkristo anapaswa kuelewa kwamba Mormonism inafundisha kwamba tunaweza kupata wokovu wetu, kinyume na Maandiko (Makala ya Imani, p.92; 2 Nifai 25:23). Ingawa hakika tutaishi tofauti kwa sababu ya imani yetu, sio kazi zetu ambazo zinatuokoa, lakini neema tu ya Mungu kwa njia ya imani anatupa kama zawadi ya bure (Waefeso 2: 4-10). Hii ni kwa sababu Mungu anakubali tu haki yake kamilifu. Kristo alikufa msalabani ili kubadilisha ukamilifu wake kwa ajili ya dhambi zetu (2 Wakorintho 5:21). Tunaweza tu kufanywa takatifu machoni pa Mungu kupitia imani katika Kristo (1 Wakorintho 1: 2).

Hatimaye, imani katika Kristo wa uongo inaongoza kwenye wokovu wa uwongo. Wokovu wowote ambao "hupatikana" ni wokovu wa uwongo (Warumi 3: 20-28). Hatuwezi kustahiki wokovu kwa sifa zetu wenyewe. Ikiwa hatuwezi kuamini Neno la Mungu, basi hatuna msingi wa kuamini kabia. Ikiwa tunaweza kuamini Neno la Mungu, basi tunapaswa kutambua kwamba Neno Lake ni thabiti na la kuaminika. Ikiwa Mungu hakuweza kuhifadhi neno lake bila usahihi, basi hakuwa Mungu. Tofauti kati ya Mormonism na Ukristo ni kwamba Ukristo hutangaza Mungu ambaye ni milele na wa uwepo wake mwenyewe, ambaye aliweka kiwango kamili na takatifu ambacho hatuwezi kuishi nacho, na ni nani basi, kwa upendo wake mkubwa, alilipa bei ya dhambi zetu kwa kumtuma Mwanawe afe msalabani kwa ajili yetu.

Ikiwa uko tayari kuweka imani yako katika dhabihu ya kutosha ya Yesu Kristo, unaweza kuzungumza maneno yafuatayo kwa Mungu: "Mungu Baba, najua kwamba mimi ni mwenye dhambi na ninastahili ghadhabu yako. Ninatambua na kuamini kwamba Yesu ndiye Mwokozi pekee. Ninaweka imani yangu kwa Yesu pekee ili aniokoe mimi. Mungu Baba, tafadhali nisamehe, nisafishe, na ubadilishe. Asante kwa neema yako ya ajabu na huruma! "

Je, umefanya uamuzi kwa Kristo kwa kile ulicho soma hapa? kama ndiyo, tafadhali bonyeza kwa “Nime mkubali Kristo hivi leo” hapo chini.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mimi ni wa Kanisa la Siku za Mwisho, kwa nini napaswa kuzingatia kuwa Mkristo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries