settings icon
share icon
Swali

Je! Harakati ya ustawi wa Israeli/ Mkristo mwanachama wa harakati ya ustawi wa Israeli ni nini?

Jibu


Harakati ya ustawi wa Israeli, tu ni harakati ya kisiasa katika mwanzo wake, leo imekuwa zaidi ya itikadi kuliko kitu kingine chochote. Harakati ya ustawi wa Israeli ni harakati ya kimataifa kwa kurudi kwa Wayahudi kwa Uyahudi, nchi ya Israeli, wakati wa kutumia haki ya kuhifadhi mamlaka ya serikali juu ya nchi ya Israeli, ambayo iliahidiwa kwao katika Maandiko ya Kiebrania. Mizizi kwa harakati ya ustawi wa Israeli iko kati ya Mwanzo sura ya 12 na 15, ambayo Mungu anafanya agano na Ibrahimu akimwahidi kwamba wazao wake watapata urithi wa ardhi kati ya Misri na Mto wa Euphrates.

Kutokana na ukweli kwamba Harakati ya ustawi wa Israeli ilianza kama harakati ya kisiasa, kulikuwepo miongoni mwa Wayahudi wa kidunia na Wayahudi wasiokuwa wa kidini mstari wa mawazo kwamba usuli wa kidini ya Wayahudi haikuwa na uhusiano na Harakati ya ustawi wa Israeli. Inasemekana kwamba harakati ya ustawi wa Israeli ilikuwa badala yake ni jibu la watu wa Kiyahudi kwa mateso ya duniani kote wakati wa Vita vya Dunia vya I na II. Hakuna taifa litawaingiza ndani, kwa hivyo walilazimika kuunda taifa lao wenyewe, ardhi ya ukoo wao kuwa mahali pa kufaa zaidi.

Bila kujali, harakati ya Wayahudi, iliyoanza mwishoni mwa miaka ya 1890, ilitimizwa mnamo mwaka wa 1948 wakati Israeli ilitambuliwa rasmi kama nchi na kupewa uhuru kama taifa ndani ya Palestina na Umoja wa Mataifa. Hii ni wakati, kiufundi, harakati ya kisiasa ya Wayahudi ilimalizika na itikadi ya Harakati ya Ustawi wa Israeli ikaanza, na kama vile, imekuwa mada ya kujadiliwa sana. Wengine wangeweza kusema kuwa Harakati ya ustawi wa Israeli imekuwa motisha kwa ubaguzi wa rangi, au jibu dhidi ya anti-semitism. Wengine wanaamini kwamba Harakati ya ustawi wa Israeli kama ilivyopo sasa ni tu uzalendo wa Kiyahudi.

Kuhusishwa na Harakati ya ustawi wa Israeli ya Wayahudi ni Mkristo mwanachama wa Harakati ya ustawi wa Israeli. Mkristo mwanachama wa Harakati ya ustawi wa Israeli ni msaada wa Mataifa tu wa Harakati ya ustawi wa Israeli ya Wayahudi kulingana na ahadi za Israeli zinazopatikana katika Biblia, vifungu kama vile Yeremia 32 na Ezekieli 34. Wayahudi Wakristo kimsingi ni kiinjili na utoa msaada kwa njia yoyote iwezekanavyo kwa nchi ya Kiyahudi ya Israeli. Kurudi kwa Wayahudi kwa Nchi ya Ahadi ni utimilifu wa unabii na unaonekana, hususan kwa wa mgawanyo, kama ishara kwamba dunia imeingia wakati wa mwisho.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Harakati ya ustawi wa Israeli/ Mkristo mwanachama wa harakati ya ustawi wa Israeli ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries