settings icon
share icon
Swali

Je Mkristo anayerudi rudi nyuma bado ameokolewa?

Jibu


Hili ni swali ambalo limejadiliwa bila mwisho zaidi ya miaka. Neno "aliyerudi nyuma" au "anayerudi nyuma" halionekani katika Agano Jipya na linatumika katika Agano la Kale hasa Israeli. Wayahudi, ingawa walikuwa watu wa Mungu waliochaguliwa, daima walimkataa na kupinga neno lake (Yeremia 8: 9). Ndiyo sababu walilazimika kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi mara kwa mara ili kurejesha uhusiano wao na Mungu waliyemkosea. Mkristo, hata hivyo, amejipatia mwenyewe dhabihu kamilifu, la mara moja na mwisho la Kristo na haitaji tena dhabihu zaidi kwa dhambi zake. Mungu mwenyewe amepata wokovu wetu kwa ajili yetu (2 Wakorintho 5:21), na kwa sababu tumeokolewa na Yeye, Mkristo wa kweli hawezi kuanguka ili asirudi.

Wakristo hufanya dhambi (1 Yohana 1: 8), lakini maisha ya mkristo haipaswi kuwa na sifa ya maisha ya dhambi. Waumini ni uumbaji mpya (2 Wakorintho 5:17). Tuna Roho Mtakatifu ndani yetu ambaye hutoa matunda mema (Wagalatia 5: 22-23). Maisha ya mkristo yanapaswa kuwa maisha yaliyobadilika. Wakristo wanasamehewa bila kujali mara ngapi wanafanya dhambi, lakini wakati huo huo Wakristo wanapaswa kuishi maisha ya utakatifu zaidi wakati wao wanapokua karibu na Mungu na zaidi kama Kristo. Tunapaswa kuwa na wasiwasi mkubwa juu ya mtu anayesema ni mwamini bado anaishi maisha ambayo inasema vinginevyo. Ndiyo, Mkristo wa kweli ambaye huanguka tena katika dhambi kwa muda mfupi bado ameokolewa, lakini wakati huo huo mtu anayeishi maisha yanayodhibitiwa na dhambi sio Mkristo wa kweli.

Je, kuhusu mtu anayemkana Kristo? Biblia inatuambia kwamba kama mtu anamkana Kristo, kwa kweli hakuwa amemjua Kristo kwa kuanzia. "Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu "(1 Yohana 2:19). Mtu ambaye anamkataa Kristo na kurudi nyuma kwa imani ni kuonyesha kwamba yeye kamwe hakuwa wa Kristo. Wale ambao ni wa Kristo hubaki na Kristo. Wale ambao wanarejelea imani yao kamwe hawakuwa nayo kwa kuanza. "Ni neno la kuaminiwa. Kwa maana, kama tukifa pamoja naye, tutaishi pamoja naye pia; Kama tukistahimili, tutamiliki pamoja naye; Kama tukimkana yeye, yeye naye atatukana sisi; Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe "(2 Timotheo 2: 11-13).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je Mkristo anayerudi rudi nyuma bado ameokolewa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries