settings icon
share icon
Swali

Muumini anafaa kuwania cheo cha kisiasa?

Jibu


Muumini kujihusisha ama kutojihusisha katika siasa ni dhana ambayo imeibua hisia mingi na kali.Bibilia haijatoa mwelekeo kamili kuhusu kuwania kisiasa.Ila sharia za waumini hutoa maamuzi kuhusu kuwania siasa katika nchi.Anayehisi kuwania siasa anafaa kuhusisha Mungu kimaombi ili aweze kukubarika kitabia vilevile.

Mataifa ambayo watawala wanapendekezwa na kuchaguliwa na wenye nchi ni zile zinazozingatia kuthibiti vita vya kisiasa na uhuru. Waumini hudhulumiwa na kudharauliwa,kunyanyaswa mbele ya uongozi usiopenda kuabudu kwao na hivyo kuwanyamazisha wakakosa kujitetea. Hao wakristo wanatangaza neno kwa kuhofia uhai wao.Sehemu zingine,waumini wana uhuru kuongea na kupendekeza wakuu wao pasipo kuhofia uhai wao wala jamii zenyewe.

Wakuu tunaowapendelea na kuwachagua wanaweza kudhuru mazingira na uhuru wetu. Wana uwezo wa kuathiri ama kuhifadhi uhuru wetu na haki ya kuabudu na kuhubiri neno. Wana uwezo kupotoza maadili ya nchi ama kuongoza kwa manufaa ya watu.Vile waumini wanajikakamua kuwa katika uongozi,kwa nafasi za kutajika ama duni,wana haki ya kutangaza injili unaongezeka na kuthaminiwa. Waumini katika uongozi wana nafasi ya kubadilisha mambo mengi kwa wema. William Wilberforce, mkuu wa kisheria wa Kiingereza wa karne ya 19 aliteseka ilimradi kuthibiti biashara ya watu iliyonoga enzi hizo.Mishowe alifaulu na hadi sasa anathaminiwa kwa jihada zake na kujikaza katika sheria za waumini.

Vilevile tuna msemo wa zamani: "Siasa ni shughuli haramu." Viongozi pamoja waliobora,wanaweza kupotozwa kwa sababu ya uongozi muovu ulio uongozini. Wanaokalia uongozi,kama Nyanja za kutambulika,wamo hatarini kwa kuhujumiwa na wale ambao wana nia ya kutaka mahitaji yao kupewa kipaumbele.Pale mapeni yapatikana kwa wingi n ahata utawala,hupotovu wa maadili umekitiri. Waumini wanaojihusiza na uongozi wa ulimwengu,wanapaswa kuwa macho wakiwa dunia hiyo,ila wasikuwe wa dunia. Hakuna katika ulimwengu uhai ni bora mno kama "mazungumzo mabaya huharibu tabia njema" (1 Wakorintho 15:33) zaidi ya ukuu wa uongozi.

Kristo akanena utawala wake si wa dunia hii (Yohana 18:36). Utawala wa Yesu haujihusishi na ile ya ulimwengu ama wakuu wa dunia. Waumini wanafaa kujuhusisha na utawala wa milele,wala si wa wakati kidogo.Waumini hawana vikwazo kujiingiza katika utawala,ilimradi wasisahau kuwa wao ni kioo cha Yesu ulimwenguni. Haya ndiyo maelekezo ya tunayotakiwa kufanya,na jukumu litufaalo kwa watu duniani ni,kuwaleta kwa Mugu kwa njia ya Kristo.(2 Wakorintho 5:20).

Ikiwa hivo Muumini anafaa kuwania utawala wa dunia?Wachache wa Waumin ni naam,na wengine ni makosa.Hapa ni uchaguzi wa moyoni unaofaa kuhusisha Mungu anayepeana kwa wamuhitajio kwa Imani. (Yakobo 1: 5).Waumini walio watawala wanafaa kufahamu kwamba matakwa ya Mungu yanafaa kutekelezwa Zaidi kuliko yale yanayohusika na utawala wa dunia. Paulo ananena kuwa shughuli zote tutendazo,zinafaa kuwa na sifa kwa Mungu si wanadamu, (1 Wakorintho 10:31; Wakolosai 3:17).Kama Muumini atawania ofisi,inafaa kama atatenda ipasavyo kwa madhumuni ya Mungu pasipo kutenga sharia za Waumini.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Muumini anafaa kuwania cheo cha kisiasa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries