settings icon
share icon
Swali

Mke wa kaini alikuwa nani?

Jibu


Biblia haielezi kwa kina juu ya mke wa kaini kama alikuwa nani. Jibu linalotarajiwa ni kwamba mke wa kaini alikuwa dadake. Biblia haielezi umri wa Kaini wakati alipomuua ndugu yake Habili (Mwanzo 4:8). Kwa kuwa wote walikuwa wakulima, lazima wawe walikuwa watu wazima, hata pengine na jamii zao. Adam na Hawa walikuwa wamepata watoto wengine mbali na Kaini na Habili wakati Habili alipouawa. Walipata wengi wengine baadaye (mwanzo 5:4). Ile hali ya Kaini kuhofu sana juu ya usalama wake baada ya kumuua Habili (mwanzo 4:14) inathibitisha kulikuwako na watoto wengi wengine pia na wajukuu na hata vilembwe wa Adamu na Hawa.

Kwa kuwa Adamu na Hawa walikuwa wanadamu wa kwanza duniani, watoto wao hawakuwa na lengine ila kuoana. Mungu hakukataza kuoana kwa jinsi hii mapema mpaka dunia ilipokuwa na watu wakutisha ndipo akakataza aina hii ya kuoana (mambo ya walawi 18:6-18). Sababu ya madhara ya ndoa za kaka na dada ni kwamba kama kila mmoja wao alikuwa na hali Fulani ya kilema ndani yaoya kurithi basi atakayezaliwa atakuwa mwenye kurithi kutoka kwa wote wazazi wawili, hivyo basi kuwa hali mbaya zaidi kuliko waliomzaa. Kadri dunia inavyoendelea, vilema hivi vinaendelea kuzidi. Lakini Adamu na Hawa hawakuwa na kilema chochote ndani yao na ika sababisha jamii zao kuwa na afya njema sana kuliko yetu hivi sasa. Haifurahishi kuona ya kwamba mke wa Kaini alikuwa dadake. Kwa kuwa Mungu alianza na mke mmoja na mme mmoja, waliofuata hawakuwa na lengine ila kuoa dada zao.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mke wa kaini alikuwa nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries