settings icon
share icon
Swali

Nini maana ya mkate usiotiwa chachu?

Jibu


Biblia inatuambia kwamba Waisraeli wangekula mikate isiyotiwa chachu kila mwaka wakati wa Pasaka kama ukumbusho wa Kutoka utumwani Misri. Kwa kuwa wana wa Israeli waliondoka Misri kwa haraka, hawakuwa na wakati wa mkate wa kukanda, hivyo ulifanyika Pasaka hiyo ya kwanza bila ya chachu, pia inajulikana kama chachu. Katika kuelezea mkate huu na kwa ni nini ulilawa, Biblia inatujulisha yafuatayo: "Usimle pamoja na mikate iliyotiwa chachu; siku saba utakula naye mikate isiyotiwa chachu, nayo ni mikate ya mateso; kwa maana ulitoka nchi ya Misri kwa haraka; ili upate kukumbuka siku uliyotoka nchi ya Misri, siku zote za maisha yako" (Kumbukumbu la Torati 16: 3). Amri zaidi juu ya kula mkate usiotiwa chachu hupatikana katika Kutoka 12: 8; 29: 2; na Hesabu 9:11. Hadi hii leo, katika nyumba za Wayahudi, sherehe ya Pasaka inajumuisha mikate isiyotiwa chachu.

Kulingana na kamusi (lexicon) ya Kiebrania, neno "mikate isiyotiwa chachu" linatokana na neno matzoh, ambalo linamaanisha "mkate au keki bila chachu." Lexicon pia inasema kuwa matzoh kwa upande wake hutoka kwa neno linamaanishalo "kuchuchura au kuvyonza." Kwa kutaja neno hili la pili la Kiebrania, lexicon inasema, "Kwa maana ya ulaji kwa ukarimu kwa uzuri." Kwa hiyo inawezekana kwamba mkate usiotiwa chachu, ingawa inaweza kuwa mzito na laini, unaweza pia kuwa ladha tamu sana.

Katika Biblia, chachu karibu kila wakati hutumika kama mfano wa dhambi. Kama chachu ambayo inaenea katika mchuzi wote wa unga, dhambi itaenea kwa mtu, kanisa au taifa, hatimaye kuharibu na kuwaleta washiriki wake katika utumwa wake na hatimaye kufa (Wagalatia 5: 9). Warumi 6:23 inatuambia kwamba "mshahara wa dhambi ni mauti," ambayo ni hukumu ya Mungu kwa ajili ya dhambi, na hii ndiyo sababu Kristo alikufa — kutoa njia ya kuondokana na hukumu hii kwa ajili ya dhambi ikiwa mtu atatubu dhambi zake, kumkubali Kristo kama dhabihu yake ya Pasaka, na moyo wake ugeuke ili apate kuimarisha maisha yake kwa kile ambacho Mungu anaamuru.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Nini maana ya mkate usiotiwa chachu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries