settings icon
share icon
Swali

Je! Mizungu ni nini?

Jibu


Kamusi inafafanua mizungu kama "liofichwa, siri na fumbo, hasa kufungamana na hali kupita akili." Mifano ya mazoea ya mizungu ni unajimu, uchawi (Wicca), ulozi, kupiga ramli, maajabu (yote uchawi na uganga), mbao za Ouija, Kadi za Tarot, uroho, parapsychology, na ushetani. Wanadamu daima wamevutiwa na mizungu, tangu nyakati za kale hata leo. Mazoea ya mizungu na matukio ya akili yamewavutia mamilioni ya watu ulimwenguni kote, na hii haijapunguzwa kwa wasiojua au wasio na elimu. Kuna sababu kadhaa ambazo zinafanya mizungu kuvutia sana kila mtu, hata katika umri wetu wa maendeleo ya kiteknolojia na kisayansi.

Kwa jambo moja, mazoea ya mizungu inavutia udadisi wetu wa asili. Watu wengi ambao wanajihusisha na mizunu huanza na vitendo "visio dhuru" kama vile kucheza na mbao za Ouija nje ya udadisi. Wengi ambao wameanza njia hii wamejikuta wakienda kina na kina ndani ya mizungu. Kwa bahati mbaya, aina hii ya ushiriki inafanana na mchanga didimizi-rahisi kuingia na ngumu kutoka. Mvuto mwingine wa mizungu ni kwamba inaonekana kutoa majibu ya haraka na rahisi kwa maswali ya maisha. Mnajimu kwa furaha anachora ramani ya baadaye yako, mbao ya Ouija na kadi za Tarot zinakupa mwelekeo, na akili inapata kuwasiliana na shangazi yako Esta ambaye anakuambia yote ni sawa baada ya maisha. Mazoea ya mizungu hudhibitiwa na pepo, ambayo hutoa habari ya kutosha tu ili kuwavutia waathiriwa wao, huku wakiweka zaidi na Zaidi uthibiti juu ya mioyo na akili ya kudanganywa.

Hatari ya vitendo vya mizungu haviwezi kutiwa chumvi. Biblia inatuambia kwamba Mungu huchukia mizungu na aliwaonya Waisraeli dhidi ya kuhusika nao. Mataifa ya kipagani yaliyozunguka Israeli yalikuwa na mwinuko mkali wa mizungu-uaguzi, ulozi, uchawi, uzimu-na hii ndiyo sababu moja Mungu aliwapa watu wake mamlaka ya kuwafukuza kutoka nchi (Kumbukumbu la Torati 18: 9-14). Agano Jipya inatuambia kwamba kuongezeka kwa maslahi katika mizungu ni ishara ya mwisho wa umri: "Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na Imani, wakisikiliza roho zindanganyazo, na mafundisho ya mashetani" (1 Timotheo 4:1).

Je! Tunawezaje kutambua mizungu na wale ambao wanaiendeleza? Tukio la Paulo na Barnaba katika siku za kanisa ya mwanzo ni mahali pazuri kuanza. "Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote mpaka Pafo, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa uongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu; mtu huyu alikuwa pamoja na liwali Sergio Paulo, mtu mwenye akili. Yeye liwali akawaita Barnaba na Sauli waje kwake, akataka kulisikia neno na Mungu. Lakini Elima, yule mchawi (maana ndiyo tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kutumia yule liwali moyo wa kuiacha ile Imani. Lakini Sauli, ambaye ndiye Paulo, akijaa Roho Mtakatifu, akamkazia macho, akasema, Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa Ibilisi, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?"(Matendo 13: 6-10).

Kutoka kwa akaunti hii, tunaona sifa kadhaa za wale wanaoshiriki katika uchawi. Wao ni manabii wa uongo (mstari wa 6) ambao wanakataa mafundisho ya msingi ya Ukristo: uungu wa Kristo, kuanguka kwa mwanadamu katika dhambi, mbinguni, kuzimu, wokovu na kazi ya kulipa ya Kristo msalabani. Pili, wanatafuta kuwashawishi watu, hasa wale walio katika nafasi za mamlaka na kuwageuza kutoka kwa imani (mistari 6-7). Tatu, wanafanya kila kitu katika uwezo wao ili kuzuia injili ya kweli ya Kristo kuenea, kupingana na watumishi Wake kila upande (mstari wa 8). Wakati ukweli wa injili ya wokovu kwa njia ya imani ndani ya Kristo inakatizwa, kufanywa hafifu, au kukataliwa kabisa, Shetani na mapepo wake hufurahi.

Hakuna kosa la ukweli kwamba uchawi katika fomu zake zote lazima uepukwe. Tunapaswa "Tuwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze"(1 Petro 5: 8). Sehemu ya kujidhibiti na kuwa macho ni ya hekima kwa mipango ya Shetani, lakini si kuchunguza maelezo ya kila mazoea ya uchawi na jambo. Badala yake, tunapaswa kuelewa lengo kuu la shetani-uharibifu wa roho zetu-na kuchukua chukizo kwa kuvaa "silaha kamili za Mungu" (Waefeso 6: 10-18). Basi tu tunaweza kusimama imara na kuzima "mishale ya moto" ya mwovu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Mizungu ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries