settings icon
share icon
Swali

Miujiza ya Yesu ilikuwa gani? Ni miujiza gani Yesu alifanya?

Jibu


Muujiza wa Mungu ni tukio lisilo la kawaida au asili ambalo linaonyesha au kudhibitisha uumbe maalumu kupitia kazi ya uungu. Miujiza yote aliyoifanya ilikuwa ya kumtukuza Mungu, kusaidia wengine, kudhibitisha kuwa hakika alikuwa kile alichosema yuko-Mwana wa Mungu. Kwa mfano wakati alituliza mawimbi katika Mathayo 8, wanafunzi walishangaa na wakuuliza, "Ni mtu wa namna gani huyu? Hata pepo na bahari vinamtii!" (aya ya 27).

Injili imenakili wingi wa miujiza ambayo Yesu alitenda. Ijapokuwa wingi wa mambo ambayo Yesu alifanya hayangeandikwa kwa muda mfupi kama huo. Yohana anakubali kwa wazi, "Yesu alifanya mbele ya wanafunzi wake ishara nyingine nyingi ambazo hazikuandikwa katika kitabu hiki…Kuna mambo mengine mengi aliyofanya Yesu, ambayo kama yangeandikwa yote, moja baada ya lingine, nadhani hata ulimwengu wenyewe usingetosha kuviweka vitabu ambavyo vingeandikwa" (Yohana 20:30 na 21:25).

Injili tofauti mara nyingi zimenakili miujiza ile ile, na kila moja yao inatoa maelezo zaidi tofauti. Wakati mwingine, ni vigumu kujua ikiwa muujiza fulani uliorekodiwa katika injili kama ni muujiza mmoja ulioandikwa kutoka mitizamo tofauti au ama miujiza mbili zimerekodiwa. Hakuna mwandishi wa injili anashughulika na kufuata utaratibu na wakati mwingine hawatupi maelezo yote ambayo tunaweza taka kujua.

Miujiza Yesu alifanya na imeorodheshwa hapa chini imewekwa katika makundi tofauti hii ni pamoja na kumbukumbu bila kujaribu kuamua ni miujiza gani iliyonakiliwa zaidi ya mara moja na ni gani inaweza kuwa tofauti na zingine katika Injili:

Miujiza ya uponyaji

• Kutakazwa kwa mtu wa ukoma: Mathayo 8:1–4; Marko 1:41–45; Luka 5:12–14; 17:11–19

• Vipofu wapokea uponyaji: Mathayo 9:27–31; Marko 8:22–26; 10:46–52 Luka 18:35–43; Yohana 9:1–38

• Watu waliponywa kutoka mbali: Mathayo 8:5–13; Luka 7:2–10; Yohana 4:46–54

• Mama mkwe wake Petro aliponywa: Marko 1:29–31

• Mtu aliyepooza aponywa: Mathayo 9:1–8; Marko 2:1–12; Luka 5:17–26

• Watu walioguza pindo ya nguo ya Yesu waliponywa: Mathayo 9:20–23; 14:35–36; Marko 5:25–34; 6:53–56; Luka 8:43–48

• Uponya mbali mbail siku ya Sabto: Marko 3:1–6; Luka 6:6–10; 13:10–17; 14:1–6; Yohana 5:1–18

• Mtu kiziwi na kigugumizi aliponywa: Marko 7:31–37

• Sikio liliokatwa lilirejeshwa: Luka 22:47–53

• Mapepo yaliondolewa (na magonjwa ya kimwili yaliyotokana na mapepo yaliponywa): Mathayo 9:32–33; 17:14–18; Marko 9:14–29; Luka 9:37–42

• Mapepo yalikemewa (na hakuna magonjwa ya kimwili yametajwa): Mathayo 8:28–34; 15:21–28; Marko 1:23–27; 5:1–20; 7:24–30; Luka 4:31–37; 8:26–39

• Umati uliponywa: Mathayo 9:35; 15:29–31; Marko 1:32–34; 3:9–12; Luka 6:17–19

• Wafu walifufuliwa: Mathayo 9:18–26; Marko 5:21–43; 8:40–56; Yohana 11:1–45

Miujiza ingine

• Umati ulilishwa (chakula kilizidishwa): Mathayo 14:13–21; 15:32–39; Marko 6:33–44; 8:1–10; Luka 9:12–17; Yohana 6:1–14

• Kutembea juu ya maji: Mathayo 14:22–33 (Petro pia); Marko 6:45–52; Yohana 6:15–21

• Kutuliza bahari: Mathayo 8:22–25; Marko 4:35–41; Luka 8:22–25

• Kujaza neti na samaki: Luka 5:1–11; Yohana 21:1–14

• Petro kufua samaki iliyekuwa na shekeli mudomoni (kwa ushuru wa hekalu): Mathayo 17:24–27

• Kugeuza maji kuwa divai: Yohana 2:1–11

• Aliulaani mti na ukanyauka: Mathayo 21:18–22; Marko 11:12–25

Kutokana na orodha yah apo juu, tunaona kuwa wingi wa miujiza zilizoandikwa katika Injili ilikuwa miujiza ya uponyaji. Huku wale waliopokea uponyaji waliponywa kutokana na maradhi yao ya kimwili, kusudi la miujiza iliyotajwa, sio ya kuondoa uchungu wa mwili. Miujiza ya uponyaji kila mara hulenga kwenye kweli kuu, ambayo ni kuwa, Yesu ni Mwana wa Mungu aliye na mamlaka. Wakati anakemea mapepo, mamlaka yake juu yao yamesisitizwa. Wakati anaponya siku ya Sabao, mamlaka yake kama Bwana wa Sabato yametiliwa mkazo. Vile vile wingi wa miujiza husisistiza mamlaka ya Yesu juu ya ulimwengu.

Hakuna njia nyingine bora ya kuchunguza miujiza ya Yesu mbali na kusoma Injili na kutengeza orodha ya kila muujiza na maelezo yaliyotolewa. (Kwa mfano, katika Yohana 2 tunasoma kuwa Yesu alibadilisha maji na kuwa divai. Muujiza huo uliondolea mbali aibu ya mwandalizi wa sherehe na ulifurahisha mamake ambaye alimsihi kuhusika, lakini matokeo ya kimsingi yameandikiwa aya ya 11: "Yesu alifanya ishara hii ya kwanza huko Kana, Galilaya, akaonesha utukufu wake; nao wanafunzi wake wakamwamini.") Wakati mwingine kusudi la miujiza limetolewa moja kwa moja, na wakati mwingine imeandikwa kwa ajili ya wale walioiona. Yesu hakutenda miujiza kwa sababu ya kujionyesha. Kila muujiza ulilenga ukweli mkuu. Hasa Yohana anasisitiza swala hili kwa kurejelea miujiza ya Yesu kama "ishara."

Kulishwa kwa watu 5,000 ni mfano tu. Yohana 6 inaanza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanamfuata Yesu kwa sababu waliona ishara. Mtu anaweza dhani hili ni jambo nzuri. Yesu anaenda mbele na kuulisha umati zaidi ya watu 5,000 wanaume, na wamama pamoja na watoto, kwa kutumia mikate tano na samaki mbili. Alafu usiku akatoweka.

Asubuhi iliyofuatia, watu walienda wakimtafuta. Ingawa Yesu hakufurahishwa na akakabili nia yao ya kumtafuta: "Yesu akawajibu, "Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba" (Yohana 6:26). Kuna kinaya hapa. Walikuwa wanamtafuta Yesu kwa sababu walipata chakula cha bure kama matokeo ya muujiza. Hamna shaka hapa, wilidhani kuwa huu ulikuwa mpango mzuri sana. Ikiwa Yesu angeendelea kuwalisha, yote ingekuwa sawa. Hata hivyo, Yesu anasema kwamba hakuiona ishara vizuri. Waliona muujiza, na bado hawangeona zaidi ya mikate na samaki. "Ishara" ambayo Yesu aliifanya inaashiria kitu kikuu. Ingawa umati uliona na ukashiriki miujiza, ulikosa maana ya ishara na hilo ndilo lilikuwa lengo la Yesu, Mkate wa Uzima. Katika huduma ya Yesu yote, watu wengi walishuhudia miujiza kama njia ya kukimu mahitaji yao badala ya kuelekezwa kwa maana kuu.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Miujiza ya Yesu ilikuwa gani? Ni miujiza gani Yesu alifanya?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries