settings icon
share icon
Swali

Je! Ni misingi gani ya Kibiblia kwa talaka?

Jibu


Wakati wa kujadili kile ambacho Biblia inasema kuhusu talaka, ni muhimu kukumbuka maneno ya Malaki 2:16, "Ninachukia talaka, asema Bwana Mungu." Misingi yeyote ambayo Biblia inaweza kutoa kwa ajili ya talaka, hiyo haimaanishi Mungu anatamani talaka kutokea katika matukio hayo. Badala ya kuuliza "ni ______ misingi kwa talaka," mara nyingi swali linapaswa kuwa "ni _______ misingi kwa msamaha, kurejesha, na / au kushauri?"

Biblia inatoa misingi miwili ya wazi kwa talaka: (1) uasherati (Mathayo 5:32; 19: 9) na (2) kuachwa na asiyeamini (1 Wakorintho 7:15). Hata katika matukio haya mawili, ingawa, talaka haihitajiki au hata kutiwa moyo. Mengi ambayo yanaweza kusemwa ni kwamba uasherati na kuachwa ni misingi (posho) kwa talaka. Kukiri, msamaha, upatanisho, na kurejesha daima ni hatua za kwanza. Talaka inapaswa kuonekana tu kama kimbilio la mwisho.

Je! Kuna misingi yoyote ya talaka zaidi ya kile Biblia inasema waziwazi? Labda, lakini hatuwezi dhania juu ya Neno la Mungu. Ni hatari sana kwenda zaidi ya kile Biblia inasema (1 Wakorintho 4: 6). Misingi zaidi ya mara kwa mara ya talaka ambayo watu huulizia kuhusu ni unyanyasaji wa mwanandoa (kihisia au kimwili), unyanyasaji wa watoto (kihisia, kimwili, au kingono), kuzoea picha za ngono, matumizi ya dawa za kulevya / pombe, uhalifu / kifungo jela, na matumizi mabaya ya fedha (kama vile kwa njia ya kuzoea kamari). Hakuna hata mojawapo ya haya yanaweza kudaiwa kuwa misingi ya waziwazi ya kibiblia ya talaka.

Hiyo haimaanishi, ingawa, kwamba hakuna hata mmoja yao ni misingi ya talaka ambazo Mungu atakubali. Kwa mfano, hatuwezi kufikiri kwamba itakuwa ni hamu ya Mungu kwa mke kubaki na mume ambaye humdhulumu kimwili na/au watoto wao. Katika hali hiyo, mke anapaswa kujitenga haswa mwenyewe na watoto kutoka kwa mume mnyanyasaji. Hata hivyo, hata katika hali kama hiyo, muda wa kujitenga na lengo la toba na kurejesha lazima iwe bora, sio muhimu kuanza utendaji wa talaka mara moja. Tafadhali elewa, kwa kusema kuwa hayo juu sio misingi ya kibiblia ya talaka, hatusemi haswa kwamba mume/mke ambaye mwanandoa wake anahusika katika shughuli hizo anapaswa kubaki katika hali hiyo. Ikiwa kuna hatari yoyote kwa mwenyewe au watoto, kujitenga ni hatua nzuri na sahihi.

Njia nyingine ya kuangalia suala hili ni kutofautisha kati ya misingi ya kibiblia ya talaka na misingi ya kibiblia ya talaka na kuolewa tena. Wengine hutafsiri misingi mbili ya kibiblia ya talaka zilizotajwa hapo juu kama misingi pekee ya kuolewa tena baada ya talaka, lakini inaruhusu talaka bila kuoa tena katika mifano mingine. Ingawa hii ni tafsiri inayokubalika, inaonekana kuja karibu sana na kudhani juu ya Neno la Mungu.

Kwa muhtasari, ni misingi gani ya kibiblia ya talaka? Jibu ni uasherati na kuachwa. Je, kuna misingi ya ziada ya talaka zaidi ya hizi mbili? Inawezekana. Je! Talaka inapaswa kuchukuliwa kiurahasi au kuajiriwa kama msaada wa kwanza? Hakika hapana. Mungu anaweza kubadilisha na kurekebisha mtu yeyote. Mungu anaweza kuponya na kuifanya upya ndoa yeyote. Talaka inapaswa kutokea tu katika matukio ya dhambi ya mara kwa mara na isiyo na toba.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni misingi gani ya Kibiblia kwa talaka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries