settings icon
share icon
Swali

Mtu anawezaje kukabiliana na migogoro katika ndoa?

Jibu


Kwa sababu ya hali ya kuanguka ya mwanadamu, migogoro ya ndoa ni hali ya maisha, hata kwa waumini katika Kristo. Mawasiliano ya upendo hayaji kwa kawaida au kwa urahisi kwa mtu yeyote. Kwa wasioamini, suluhisho kwa migogoro ni ngumu kwa sababu bila ya Kristo wanadamu hawana uwezo wa upendo usio na ubinafsi (Waefeso 4: 22-32). Wakristo, hata hivyo, wana Biblia kwa maagizo katika mahusiano. Kutumia kanuni za kibiblia za mahusiano itatuwezesha kutatua migogoro ya ndoa kwa ufanisi zaidi.

Kanuni ya kwanza na muhimu sana katika kutatua migogoro katika mahusiano, hasa katika ndoa, ni kupendana kama vile Kristo alitupenda (Yohana 13:34) na akajitoa mwenyewe kwa ajili yetu. Waefeso 5: 21¬-6: 4 inaelezea mahusiano ndani ya familia: tunapaswa kuwajisilisha sisi kwa sisi na kwa upendo na kuweka mahitaji ya wengine mbele ya yetu wenyewe. Hii ni kweli hasa katika ndoa ambapo mume anapaswa kumpenda mke wake kama Kristo alivyolipenda kanisa na kumtunza yeye kama anavyojali mwili wake mwenyewe. Kwa upande mwingine, mke anapaswa kujiwasilisha kwa mumewe na kumheshimu (Waefeso 5: 22-33).

Hii itaonekana kuwa ni maelekezo rahisi sana isipokuwa hali ya kawaida ya binadamu huwa wanarudia hali baada ya kitendo katika mahusiano, badala ya kuwa dhahatari kabla ya tendo. Wanawake huwa tayari sana kujiwasilisha kwa waume wanaowapenda kama Kristo alivyolipenda kanisa, na waume wako tayari zaidi kuwapenda wake ambao wanawaheshimu na kunajiwasilisha. Hupo kuna shida. Kila mmoja anasubiri mwingine kufanya kitendo cha kwanza. Lakini amri za Mungu kwa waume na wake sio za masharti. Uwasilishaji hautegemei upendo, na upendo hautegemei heshima. Kuchukua hatua ya kwanza kwa utiifu, bila kujali vitendo vya mwingine, huelekeza katika kulemaza mgogoro na kuanzisha mfumo mpya wa tabia.

hilo likiwa katika akili, wakati mgogoro unajibuka katika ndoa hatua ya kwanza ni kujiioji (2 Wakorintho 13: 5). Baada ya kuletea haja zetu kwa Bwana na kuwa waaminifu kwetu wenyewe kwa kushindwa kwetu wenyewe au tamaa za ubinafsi, basi tunaweza kuwafikia wengine na wasiwasi zetu. Zaidi ya hayo, Mungu aliwaumba waumini ili kukidhi mahitaji ya wengine kwa amani (Wakolosai 3:15). Sisi sote tunahitaji neema kwa makosa yetu wenyewe na tunapaswa kuwa na neema kwa wengine tunapowasilisha mahitaji yetu na haja zetu (Wakolosai 4: 6).

Kuzungumza ukweli katika upendo ni muhimu kwa kusikilizwa kwa sababu wakati tunapowasiliana na wengine thamani yao machoni petu wataweza kukubali kweli ngumu (Waefeso 4:15). Watu wanaojihisi kushambuliwa na kuhukumiwa watakuwa wagumu na kwa wakati huo, mawasiliano yatavunjika. Kinyume chake, watu wanaojisihisi kuwa tunawajali na tunawatakia mambo mema watatuamini kuwasiliana nao kwa upendo na ustawi wao. Hivyo kwa kuwasiliana ukweli katika upendo ni muhimu kabisa kwa kutatua migogoro. Hili ni kweli hasa katika ndoa, ambapo kuwa karibu na mpenzi ambaye ametukwaza mara nyingi hudhihirisha mbaya zaidi yaliyo ndani yetu. Hisia za kusikitisha zinazalisha maneno yenye ukali ambayo, kwa upande wake, hutoa hisia zaidi za kuumiza. Kujifunza nidhamu ya kufikiri kwa makini na kuomba kabla ya kuzungumza inaweza kukanya migogoro hii ya inayojirudia rudia. Kuwasiliana kwa kiungu kunaweza kuweka kwa maneno rahisi kuwa, kumbuka kuwatendea wengine kwa njia tunayotaka watutendee (Luka 6:31). Mungu alisema kuwa heri ni waleta amani, na hilo ndilo lengo la Wakristo (Mathayo 5: 9).

Kuna sehemu mingi ya mahusiano, migogoro, na mawasiliano, na Biblia imejaa busara kwa kuishi maisha ya kiungu. Hapa ni amri maalum ya maandiko ya jinsi tunapaswa kutendeana:

Ili kutatua mgogoro wa ndoa, ni lazima:
Kuwa na amani na mtu mwingine — Marko 9:50
Pendaneni — Yohana 13:34; Warumi 12:10; 1 Petro 4: 8; 1 Yohana 3:11, 23; 4: 7, 11, 12
Iinuana — Warumi 14:19; Waefeso 4:12; 1 Wathesalonike 5:11
Kuwa na akili sawa kwa kila mmoja — Warumi 12:16
Tanguliza mwenzio Warumi 12:10
Salimianeni — Warumi 16:16
Ona wengine kuwa bora zaidi kukuliko wewe — Wafilipi 2: 3
Hudumiana nyinyi kwa nyinyi — Wagalatia 5:13
Pokeana ninyi kwa ninyi — Warumi 15: 7
Jitoleeni ninyi kwa ninyi — Warumi 12:10
Furahini au ombolezeni pamoja — Warumi 12:15
Imizaneni ninyi kwa ninyi — Warumi 15:14; Wakolosai 3:16
Tunzaneni ninyi kwa ninyi — 1 Wakorintho 12:25
Onyesheana huruma nyinyi kwa nyinyi — Warumi 15: 1-5; Waefeso 4: 2; Wakolosai 3:13
Kuwa wema na kusameheana nyinyi kwa nyinyi — Waefeso 4:32; Wakolosai 3:13
Nyenyekeana nyinyi kwa nyinyi — Warumi 12:10; Waefeso 5:21; 1 Petro 5: 5
Farijiana — 1 Wathesalonike 4:18
Himizana nyinyi kwa nyinyi — 1 Wathesalonike 5:11; Waebrania 3:13
Kuwa na huruma nyinyi kwa nyinyi — 1 Petro 3: 8
Ombeaneni nyinyi kwa nyinyi — Yakobo 5:16
Kiri makosa yenu nyinyi kwa nyinyi — Yakobo 5:16
Karibeshi nyinyi kwa nyinyi — Warumi 14: 1; 15: 7

Ili kutatua mgogoro wa ndoa, hatupaswi:
Kuwa na kiburi kwa mwingine — 1 Wakorintho 4: 6
Kuhukumiana — Warumi 12:16
Kudanganyana nyinyi kwa nyinyi — Wakolosai 3: 9
Kuwa sehemu pamoja na 1 Timotheo 5:21
Tusichokozana na kuhusudiana — Wagalatia 5:26
Tusiwakiane tamaa sisi kwa sisi- Warumi 1:27
Tusichukiane sisi kwa sisi — Tito 3: 3
Tusipelekane mahakamani — 1 Wakorintho 6: 1-7
Tusitumiane vibaya — Wagalatia 5:15

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mtu anawezaje kukabiliana na migogoro katika ndoa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries