settings icon
share icon
Swali

Mfano ni nini?

Jibu


Mfano ni, kwa kweli, kitu "kilichosemwa mkabala" na kitu lingine. Mifano ya Yesu ilikuwa simulizi ambazo "zilisemwa" na ukweli ili kuonyesha ukweli huo. Mifano yake ilikuwa misaada ya kufundisha na inaweza kuzingatiwa kama milinganisho iliyopanuliwa au milinganisho iliyovuviwa Maelezo ya kawaida ya fumbo ni kwamba ni simulizi ya kidunia iliyo na maana ya kimbingu.

Kwa muda katika huduma yake, Yesu alitegemea mifano sana. Aliwaambia wengi kwa mifano; kwa kweli, kulingana na Marko 4:34, "Hakusema nao neno lolote pasipo mfano." Kuna mifano 35 ya Yesu iliyorekodiwa katika Injili.

Kamwe haikuwa hivyo kila wakati. Mwanzoni mwa huduma yake, Yesu hakuwa ametumia mifano. Kwa ghafla, Akaanza kusimulia mifano peke yake, kwa kuwashangaza wanafunzi wake, ambao walimwuliza, "Kwa nini unasema na watu kwa mifano?" (Mathayo 13:10).

Yesu alielezea kwamba kutumia kwake mifano kulikuwa na madhumuni aina mbili: kufunua ukweli kwa wale ambao walitaka kuujua na kuficha ukweli kutoka kwa wale ambao hawakujali. Katika sura iliyotangulia ya (Mathayo 12), Mafarisayo walikuwa wamemkataa Masihi wao hadharani na walimkufuru Roho Mtakatifu (Mathayo 12: 22-32). Walitimiza unabii wa Isaya wa watu wenye mioyo migumu, vipofu kiroho (Isaya 6: 9-10). Jibu la Yesu lilikuwa kuanza kufundisha kwa mifano. Wale ambao, kama Mafarisayo, walikuwa na dhana mbaya dhidi ya mafundisho ya Bwana wangeipuuza mifano kama upuuzi usio na maana. Walakini, wale ambao walitafuta kweli kabisa wangeielewa.

Yesu alihakikisha kuwa wanafunzi wake wanaelewa maana ya mifano: "Hakusema nao neno lolote pasipo mfano. Lakini alipokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu" (Marko 4:34).

Kutafsiri fumbo kunaweza kuwa na changamoto kwa mwanafunzi wa Biblia. Wakati mwingine, tafsiri ni rahisi kwa sababu Bwana mwenyewe alitoa tafsiri hiyo — Mfano wa Mpanzi na Mfano wa Ngano na magugu yote imefafanuliwa katika Mathayo 13. Hapa kuna kanuni ambazo zinazosaidia katika kutafsiri mifano mingine:

1) Tambua wigo wa ukweli wa kiroho unaowasilishwa. Wakati mwingine, mfano hutanguliwa na maneno ya utangulizi ambayo hutoa muktadha. Kwa mfano, mara nyingi Yesu alitangulia mfano kwa maneno "hivi ndivyo ufalme wa mbinguni ulivyo." Pia, kabla ya Mfano wa Mfarisayo na Mtoza Ushuru, tunasoma haya: "Yesu akatoa mfano huu kwa wale waliojiamini kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine" (Luka 18: 9). Utangulizi huu unafafanua mada inayoolezwa (uadilifu nafsia na kiburi cha kiroho).

2) Tofautisha kati ya hoja kuu ya hadithi na kile kilichopo ambacho kinasaidia kuelezea hadithi. Kwa maneno mengine, sio kila elezo la ndani la mfano lina maana ya kiroho. Baadhi ya maelezo yapo tu ili kusaidia hadithi kuonekana kweli zaidi. Kwa mfano, katika tafsiri ya Yesu mwenyewe ya Mfano wa Mpanzi, hasemi chochote juu ya ukweli kwamba kuna aina nne (na ni nne tu) za mchanga. Maelezo hayo hayakuwa na maana kwa uhakika wa houja ya jumla ambayo Yesu alikuwa anasungumzia.

3) Linganisha Maandiko kwa Maandiko. Kanuni hii ya kimsingi ya ufafanuzi wa maandiko (hamaniutiki) sio ya muhimu sana wakati wa kuidadisi mifano. Mifano ya Yesu kamwe haitahitilafiana na Neno lingine la Mungu, ambalo alikuja kuelezea (Yohana 12:49). Mifano imekusudiwa kuonyesha mafundisho, na mafundisho ambayo Yesu alielezea yanapatikana wazi yakifundishwa mahali pengine katika Biblia.

Kunayo mifano mingine katika Biblia mbali na ile inayopatikana katika Injili. Kitabu cha Mithali kimejaa vielelezo — pindi Sulemani alipotumia linganisho kufundisha ukweli, haswa kwa mithali ambaanifu, matokeo yalikuwa mfano rahisi. Kwa mfano, Mithali 20: 2 inasema, "Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene." Kunguruma kwa simba "husema mkabala" na hasira ya mfalme kwa kusudi la kulinganisha. Hicho ndicho kiini cha lugha ya kifumbo.

Baada ya kuwaambia baadhi ya mifano Yake, Yesu alisema, "Mwenye masikio ya kusikia, na asikie" (Marko 4: 9, 23). Huu ulikuwa wito wa kuusikiliza mifano, na sio tu kama vile mtu atasikiliza simulizi ya kawaida lakini kama yule anayetafuta ukweli wa Mungu. Mungu atujalie masikio sisi wote ya "kusikia" kwa kweli.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mfano ni nini?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries