settings icon
share icon
Swali

Je! Ni kwa nini kuna tafauti kubwa sana juu ya meza ya Bwana?

Jibu


Chakula takatifu au Meza ya Bwana (pia inajulikana katika makanisa mengine kama meza ya Bwana au Ekaristi) ni chanzo cha kutokubaliana sana ndani ya kanisa kwa ujumla. Kilichokubaliwa kinapatikana wazi katika Maandiko: sherehe hii ilianzishwa na Yesu wakati wa chakula cha jioni cha mwisho na wanafunzi Wake. Wakati huo, aliwapa mkate na "kikombe." Akawaambia kwamba vitu hivi ni mwili na damu yake (Mathayo 26: 26-28; Marko 14: 22-24). Pia aliwaamuru kurudia sherehe hiyo kwa kumkumbuka (Luka 22:19).

Utata kuhusu meza ya Bwana hutokana na maswali mengi kama vile: Je! Yesu alikuwa anazungumzia mwili wake na damu yake kiriwaya kwa uhalisi, au Je! maneno yake kiajabu ilikuwa mchanganyiko wa riwaya na lugha halisi? Je! kanisa linapaswa kuadhimisha meza ya Bwana mara ngapi? Je! pasaka inapaswa kuwa namna ya kupokea neema au ukumbusho tu? Je! Ni kitu gani kilikuwa ndani ya kikombe-divai iliyotiwa chachwa au mzabibu usio na chachu?

Kwa sababu Yesu hakutoa maagizo mahususi, ya hatua kwa hatua kuhusu ibada hiyo, kwa kawaida, kuna mabishano kuhusu jinsi na vipi na lini, na nini hasa mkate na divai vinawakilisha. Kuna mabishano ikiwa kweli au la kiuhalisi vitu hivi vinawakilisha damu na mwili wa Kristo (mafundisho ya Katoliki kuwa mkate na divai hubadilika na kuwa mwili halisi wa Kristo), ikiwa zina Roho Wake (mafundisho ya Luther kuwa dam una mwili wa Yesu Kristo upo Pamoja na divai na mkate), au ikiwa divai na mkate ni ishara tu za mwili Wake na damu. Kunayo maoni tofauti juu ya liturujia (kawaida ya ibada na sala ya dini) ambayo inapaswa kuzungumziwa na ikiwa kukiri kunapaswa kuwa sehemu ya ibada. Madhehebu yanatofautiana juu ya ukawaida wa ushirika, jinsi inapaswa kufanywa, na nanani.

Kunayo matukio manne ya meza ya Bwana akiwa na wanfunzi wake: matatu katika Injili na moja katika 1 Wakorintho 11:24-25). Tunapoyaangalia matukio kwa upamoja, tunajua yafuatayo:

1. Wakati wa chakula cha Pasaka, Yesu aliubariki, akaumega, na kuwapa wanafunzi wake mkate, akisema, "Huu ndio mwili wangu, uliotolewa kwa ajili yenu. Fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. "

2. Pia alipitisha kikombe akiwambia wagawane wao kwa wao: "Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu. Fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu" aliwaagiza wao wote kukinywa.

3. Ilikuwa ni wakati huu wa chakula kwamba Yesu alisema kuwa mmoja wa wanafunzi wake atamsaliti.

4. Yesu anasema hatakunywa tena tunda la mzabibu hadi Atakapokunywa upya na wafuasi wake katika ufalme wa Baba.

Alipoanzisha Meza ya Bwana, Yesu alikuwa akilenga uhusiano wa kiroho kati Yake na wanafunzi Wake. Hakutoa maelezo ya jinsi au lini au wapi au nani apewe viashiria hivyo, na kwa hivyo, makanisa anuwai yana uhuru wa kuamua habari hizo wenyewe. Kwa mfano, ikiwa kama kanisa linaadhimiza meza ya Bwana moja kwa juma au mara moja kwa mwezi sio muhimu sana.

Walakini, tafuati nyingine juu ya meza ya Bwana ni muhimu kitheolojia. Kwa mfano, ikiwa kula Meza ya Bwana ni lazima ili kupokea neema, basi neema sio bure kweli na lazima ipatikane kwa matendo tunayofanya, ambayo ni kinyume na Tito 3: 5. Na, ikiwa mkate ni mwili wa Kristo, basi Bwana anatolewa dhabihu tena na tena, ambayo ni kinyume na Warumi 6: 9-10. Maswala haya ni muhimu ya kutosha kugawanya kanisa kwa miaka na kweli suala likawa jambo la mabishano wakati wa Mageuzi ya Kiprotestanti.

Kuelewa kwamba tunaokolewa kwa neema, kupitia imani, mbali na matendo (Waefeso 2: 8-9) na tukizingatia maneno ya Yesu kuhusu viashiria vya meza ya Bwana kuwa ya mfano, tunazingatia uzuri wa agano jipya (Mathayo 26:28)) lililoidhinishwa na damu ya Yesu mwenyewe. Tunakumbuka dhabihu yake kwa ajili yetu mara nyingi tunapokula Meza ya Bwana (Luka 22:19). Na tunatarajia kushiriki tena kikombe pamoja na Kristo katika ufalme wa Mungu (Mathayo 26:29; Marko 14:25; Luka 22:18).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Ni kwa nini kuna tafauti kubwa sana juu ya meza ya Bwana?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries