settings icon
share icon
Swali

Ni mara ngapi meza / mwili wa Bwana unapaswa kuzingatiwa?

Jibu


Hakuna mahali popote Bibilia hutueleza ni mara ngapi tunapaswa kuchukua ushirika. 1 Wakorintho 11: 23-26 inaandika maagizo yafuatayo ya ushirika: "Kwa maana mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo." Kifungu hiki kinatoa maelekezo yote tunayohitaji ili kufanya ibada ya ushirika na kuelewa umuhimu wa kile tunachofanya.

Mkate ambso Yesu aliumega unawakilisha mwili Wake uliovunjika msalabani kwa ajili yetu. Kikombe kinawakilisha damu aliyomwagika kwa niaba yetu, kuziba agano kati yake na sisi. Kila wakati tunapozingatia amri ya ushirika, hatukumbuki tu yale aliyetufanyia, lakini tuna "onyesha" pia kwa wote wanaoangalia na wote wanaoshiriki. Ushirika ni picha nzuri ya kile kilichotokea msalabani, chenye inamaanisha, na jinsi inavyo badilisha maisha yetu kama waumini.

Inaonekana kwamba, kwa kuwa tunachukua Meza ya Bwana kukumbuka kifo cha Kristo, tunapaswa kukichukua kila mara na inavyostahili. Makanisa mengine yana huduma ya kila mwezi ya meza ya Bwana; wengine hufanya baada ya miezi; wengine kila wiki. Tangu Biblia haitupi maelekezo maalum kuhusu ni mara ngapi, kuna usawa fulani katika kanisa mara ngapi inapaswa kuzingatia meza ya Bwana. Inapaswa kuwa kila mara kuzingatia Kristo, bila kuwa ya mara nyingi haitakuwa ya kawaida. Kwa hali yoyote, haijalishi ni mara ngapi inaadimishwa, bali ni tabia ya moyo wa wale wanaoshiriki. Tunapaswa kula na heshima, upendo, na hisia kamili ya shukrani kwa Bwana Yesu, ambaye alikuwa tayari kufa msalabani kuzibeba dhambi zetu mwenyewe.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni mara ngapi meza / mwili wa Bwana unapaswa kuzingatiwa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries