settings icon
share icon
Swali

Kanisa linaweza aje endelea/kuishi wakati mchungaji ameondoka?

Jibu


Bila shaka kumpoteza mchungaji inaeza kuwa wakati mgumu na mwenye msukosuko kwa kanisa, haswa ikiwa mchungaji ameondoka kwa mazingira magumu. Ikiwa mchungaji anastaafu baada ya huduma refu na ya uaminifu, ama kuhamia maeneo mengine ili kujibu wito wa Mungu itakua ni huzuni ulio na furaha. Umati wake unaeza mpea kwaheri kwa kumpea zawadi na kumshangilia, kumshukuru kwa sifa za kipekee na makumbusho na kushangilia pamoja na yeye anapohamia maisha na shirika ingine. Yeye na familia yake wataendelea kua kwa nyoyo za wafuasi wake wa kitambo na kushikiliwa kwa maombi.

Vipi kuhusu wakati mchungaji anaondoka kwa sababu ya mazingira ambayo si bora,kama vile yeye kuwa na maadili potovu, kutoridhika na utendaji wake (iwe halisi ama isiyotambulika) ama mgawanyiko wa kanisa? Je, wale wanaobaki huwa wanarekebisha aje chochote kile ambacho kimeharibiwa, na kushikilia kanisa pamoja na kuendelea mbele kwa hatma ya baadaye?

Kitu cha kwanza cha muhimu kabisa katika kujibu maswali haya inaanza na kuelewa haswa kanisa linamilikiwa na nani. Kanisa halimilikiwi na mchungaji ama uongozi ama ata umati. Kanisa ni la Kristo , ambaye ni kichwa cha kanisa lake. Neno kanisa lina maana ya 'umoja wa walio na wito.' Hawa walio na wito huwa wanakusanyika kumwabudu mkuu wao. Wamejitolea kufuata mienendo yake kwa lolote wanalo fanya, kumheshimu na kupeana picha nzuri yake kwa ulimwengu unaotazama. Kanisa ni mwili wa Kristo na alikufa kwa ajili ya mwili wake, na mwili wake unaishi kwa ajili yake. Hadi pale tu uongozi utajitolea kwa mpango huu wa kibiblia na umati kushikilia ukweli huu, hakuna mchungaji atakaye fanikiwa. Kwa hivyo hatua ya kwanza katika kushinda hasara ya kumpoteza mchungaji ni viongozi kuja pamoja na kuelewa kanisa. Kuongezea lazima viongozi hawa wakue na umoja kujitolea na kuelewa kanisa, ikiwemo kanisa ya mtaa nay a kimataifa. Migawanyiko mingi kanisani hutokea kwa sababu ya tofauti ya imani na kujitolea kwa viongozi, na kwa hakika wachungaji wengi huondoka kwa sababu hii. Kwa hivyo kabla ya kuanza kutafuta mchungaji mwingine , uongozi wa kanisa uanafaa kukubaliana kuhusu mwongozo wa kanisa.

Pili, uongozi unafaa kuelewa na ujitolee katika ukuu wa Mungu kwa kila kitu, lakini haswa wakati mchungaji anaondoka. Hakuna chochote kilitokea ambacho ni mshangao kwa Mungu; aidha yeye ndo alisababisha mchungaji kuondoka ama akakubali ili aweze kutimiza malengo yake ya kimungu. Kwa njia yoyote , ametuhakikishia kwamba kila kitu hufanyika kwa umoja milele kwa wale ambao wanampenda na wameitwa kwa malengo yake ( Warumi 8:28), na kanisa linaweza kujitia moyo katika hekima kwamba wanaongozwa na Mungu mkuu ambayo amejihusisha na kila jambo katika maisha yao na ushirika wa kanisa, vile vile kwa mchungaji pia. Kuamini udhabiti mkuu wa Mungu kwa kanisa lake linaeza fanya watu kuongea kitu moja na Paulo, "Lakini Mungu ashukuriwe, ambaye hutuongoza katika ushindi tukiwa ndani ya Krist. Naye hututumia sisi kueneza maarifa ya kumjua yeye kila mahali kama harufu nzuri" (2 Wakorintho 2:14).

Tatu, kuondoka kwa mchungaji ni fursa nzuri ya kutathmini upya/ ama kufafanua upya utume na kazi ya kanisa. Kuna mamlaka za kawaida kutoka kwa maandiko- kufunza na kuhubiri neno, kuabudu, kumtukuza Mungu, na kutimiza tume ili kueneza injili, lakini ni kwa njia gani haswa hizi vitu zimepewa kipau mbele kanisani, na ni aina gani ya mchungaji anahitajika ili kufanikisha malengo ya kanisa? Ikiwa kanisa linasisitiza kuwafikia wamishonari, kwa mfano, mchungaji mwenye maono kama hayo anafaa kutafutwa. Ikiwa kanisa linahisi kuwa limepewa wito wa kuwahudumia watoto, maskini, wazee, ama kwa wahamiaji wa mtaa, kidini mchungaji huyo anafaa awe na moyo kwa huduma hizo. Migawanyiko ya kanisa imetokea ambapo mchungaji na uongozi wanakua na maoni tofauti kuhusu wito nah ii inaeza epukika kwa kuwa na maono mazuri kuhusu jukumu la kanisa katika jamii na ulimwengu kwa jumla.

Mwisho, kabla ya jaribio lolote la kumbadilisha mchungaji, uongozi unafaa kuchambua kwa nni aliondoka. Ikiwa shida ambazo zilisababisha yeye kuondoka kabla ya wakati kutimia zipo bado, kuepuka marudio machungu itakua ngumu. Kwa mfano, ikiwa kuna shida ya dhambi miongoni mwa umati na haikushughulikiwa vilivyo, inafaa kushughulikiwa kabla ya kuita mchungaji mwingine kwa kanisa. Mtume Paulo alikabiliana na makundi ya watu walio watenda dhambi kupita kiasi na wenye shingo ngumu katika kanisa la Korintho , ambayo ilikua inagawanyika na kupatwa na migogoro kila wakati. Walikua na ubinafsi, hawana utaratibu, na wa kidunia. Dhambi ilichafua meza ya Bwana. Walipigana wenyewe kwa wenyewe, kushtakiana wenyewe kwa wenyewe na kufanya usherati kiholela miongoni mwao, na walikua na furaha. Kualika mchungaji katika kanisa ambalo washiriki wako na tabia kama hizi na hajui ni mbaya sana na itapelekea mchungaji huyo kuondoka kwa mazingira ya huzuni. Ni jukumu la uongozi wa kanisa kuzingtia kanuni za Mathayo 18, haswa kabla ya mchungaji mwingine kukuja ama badae bora yake anajua hali ilivyo.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kanisa linaweza aje endelea/kuishi wakati mchungaji ameondoka?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries