settings icon
share icon
Swali

Ina maana gani kuvaa mavazi ya heshima?

Jibu


Katika kuelezea hali ya mavazi inayofaa kwa wanawake katika kanisa, mtume Paulo anawahimiza kuvaa "kwa heshima" na "Kujistiri inavyostahili" kisha anaendelea kupambanua mavazi yasiyo ya heshima na matendo mema ambayo yanafaa kwa wale wanaodai kuwa waabudu wa kweli wa Mungu (1 Timotheo 2: 9-10). Heshima katika jinsi tunavyovaa sio tu katika kanisa; ni kuwa kiwango cha Wakristo wote wakati wote. Ili kuelewa maana ya kuvaa mavazi ya heshima ni muhimu kuchunguza mitazamo na malengo ya moyo. Wale ambao nyoyo zao hutegemea Mungu watajitahidi kuvaa mavazi ya heshima, kwa ustadi, na kwa usahihi. Wale ambao nyoyo zao hutegemea wao wenyewe huvaa kwa namna inayolenga kujishughulisha wenyewe bila kujali mathara kwa wao wenyewe au wengine.

Mwanamke mwenye kumcha Mungu anajitahidi kufanya kila kitu kwa mtazamo wa kimungu. Anajua kwamba Mungu anataka watu wake wajishughulishe kw a utukufu wake na hali ya kiroho ya ndugu na dada zao katika Kristo. Ikiwa mwanamke anayesema kuwa Mkristo bado anavaa kwa njia ambayo itaelekeza macho kwa mwili wake, yeye ni shahidi maskini wa Yule ambaye alinunua nafsi yake kwa kuf a msalabani. Yeye husahau kuwa mwili wake umekombolewa na Kristo na sasa ni hekalu la Roho Mtakatifu (1 Wakorintho 6: 19-20). Anaambia ulimwengu kwamba anaona thamani yake kama ni ya kimwili na kwamba mvuto wake kwa wengine hutegemea ni kiasi gani cha mwili wake anaowafunulia. Zaidi ya hayo, kwa kuvaa kwa njia isiyo ya heshima, akionyesha mwili wake kwa wanaume ili kusababishs tamaa, huwafanya ndugu zake katika Kristo kutenda dhambi, kitu kilichohukumiwa na Mungu (Mathayo 5: 27-29). Mithali 7:10 inataja mwanamke "amevaa kama kahaba na kwa nia ya hila." Hapa tunaona maelezo ya mtu ambaye hali yake ya moyo inaonyeshwa kwa njia yake ya kuvaa.

Andiko linasema kuwa mwanamke anapaswa kuvaa mavazi ya heshima, lakini nini hasa maana yake katika jamii ya kisasa? Je! Mwanamke anapaswa kujifunika kutoka kichwa hadi chini a miguu? Kuna dini duniani ambazo hudai hili kwa wanawake. Lakini je, hii ndiyo maana ya Kibiblia kumaanisha heshima? Tena, tunapaswa kurudi kwenye suala la mtazamo wa moyo. Ikiwa moyo wa mwanamke umegemea kuelekea utakatifu, yeye atavalia nguo ambazo sio za kuchochea au kujionyesha kwa umma, nguo ambazo hazionyeshi kinyume na ushahidi wake binafsi kama mtoto wa Mungu. Hata wakati kila mtu yeyote anavaa mavazi yasio na heshima, anakataa majaribu ya kwenda pamoja na umati. Anajua aina hizi za nguo zimeundwa kutekeleza kipaumbele kwa mwili wake na kusababisha watu kuwa na tamaa, lakini yeye ni mwenye ana hekima ya kutosha kujua kwamba aina hiyo ya tahadhari tu inapunguza gharama yake.

Anachukia wazo la kuwasababisha wanaume kutenda dhambi kwa sababu ya mavazi yak, kwa sababu anataka kumpenda na kumheshimu Mungu na anataka wengine wafanye hivyo. Heshima katika mavazi huonyesha unyenyekevu na utakatifu wa moyo, mitazamo ambayo inapaswa kuwa kielelezo cha wanawake wote wanaoishi kufurahia na kumheshimu Mungu.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ina maana gani kuvaa mavazi ya heshima?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries