settings icon
share icon
Swali

Ni mambo gani muhimu ya kuelewa kuhusu maumbile/asili ya Mungu?

Jibu


Sehemu ya muhimu ya asili ya Mungu ni utakatifu wake. Takatifu inamaanisha "kutengwa kando" na hakika Mungu anajitenga toka kwa viumbe vyake kwa misingi ya asili na sifa zake. Ufunuo 15:4 yasema, "Wewe peke yako ni Mtakatifu." Ufunuo 4:8 inaelezea viumbe wanne walio hai ambao wanamwimbia Mungu usiku na mchana, "Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, Bwana, Mungu Mwenye Nguvu, aliyekuwako na anayekuja." Ni utakatifu wa Mungu ambao unamfanya awe "moto unaochoma" ambao utahukumu dhambi zote (Waebrania 12:29). Tamatizo nzuri zana zinazosifu utukufu wa Mungu zinapatikana katika Biblia yote, ikiwa ni pamoja na Zaburi 99:9; Zaburi 33:21; Zaburi 77:13; Zaburi 89:18; Zaburi 105:3; na zinginezo.

Ni muhimu pia kuelewa kwamba Mungu ni roho wa milele (Yohana 4:24). Ni Mungu mmoja (Kumbukumbu 6:4) ambaye amekuwemo kama nafsi tatu tofauti: Baba, Mwana, na Rohom Mtakatifu. Yeye hana mwili halisi (ingawa Mwana aliutwaa mwili). Kanuni ni potovu ikiwa inakana Utatu, inamtizama Mungu kuwa Baba kama vile mwanadamu, au kukana ubinadamu na uungu wa Kristo (ona 2 Yohana 1:7)

Mungu pia katika asili yake ni mwenye enzi. Yeye haukumiwe na yeyote na ako na mamlaka yote juu ulimwengu wote na kila kitu kilichomo. Uwezo wake unadhihirisha katika njia nyingi, ikiwa ni pamoja na uenye enzi wake. Njia zake zote si haki (Zaburi 145:17), hata kama ikiwa mwanadamu ataamini njia nzake kuwa "haki" au la hiyo haijalishi. Bwana Mungu hazuiliwi na wakati au nafasi. Yeye ako na mpango, amekuwa nao tangu kale iliyopita, na mapenzi yake yatatimia (Danieli 4:37; Zaburi 115:3).

Sehemu ingine muhimu ya asili ya Mungu ni kutobadilika kwake. Yeye habadiliki, Yeye ni yule yule "jana leo na milele" (Waebrania 13:8). Anaielezea wazi katika Malaki 3:6, "Mimi ni Mwenyezi-Mungu, mimi sibadiliki." Kwa sababu ya asili yake isiyobadilika badilika, tunaweza kutegemea baraka zake: "Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu" (Yakobo 1:17).

Uenye enzi wa Menyezi hunena na kuume wake kutenda kile apendacho, na uenye enzi wake hunena na uwezo wake kufanya hivyo. Pai yeye anajua kila kitu, toka mwanzo hadi mwisho, kila kitu tunachowaza, fanya na kusema. Yeye ako na ufahamu wa kila mmoja ambaye amewai ishi au atakayeishi, anawajua kwa karibu sana katika kila njia. Inatia moyo kusikia meneno ya Mungu katika Yeremia 1:5, "Kabla hujachukuliwa mimba, mimi nilikujua, kabla hujazaliwa, mimi nilikuweka wakfu."

Tusipuuze ghadhabu ya Mungu, ambayo hububuchika toka kwa utakatifu wake. Yeye ana hasira takatifu dhidi ya dhambi (Zaburi 7:11), na kwa sababu ya hukumu ya Mungu ijayo, mwanadamu anahitaji ujumbe wa neema na wokovu wa Injili. Pia ni asili ya Mungu kupenda (1 Yohana 4:16), na katika upendo wake kwa ulimwengu, alimtuma Mwanawe wa pekee, Yesu Kristo kutukomboa (Yohana 3:16). Hakuna kitu kingine mbali dhabihu kamilifu itafanya hivyo.

Upendo ni zaidi ya sifa ya Mungu; hakika yeye ni kiini cha upendo. Hii imetajwa vyema katika 1 Yohana 4:8, "Mtu asiye na upendo hamjui Mungu, maana Mungu ni upendo." Upendo wa Mungu ni wa milele. Kwa sababu habadiliki, upendo wake haubadiliki. Upendo wake ni kamilifu na takatifu.

"Maana ninajua hakika kwamba hakuna kitu kiwezacho kututenganisha na upendo wake: Wala kifo, wala uhai; wala malaika au nguvu nyingine za mbinguni; wala yanayotokea sasa, wala yatakayotokea baadaye; wala mamlaka; wala ulimwengu wa juu, wala wa chini kabisa. Hakuna kiumbe chochote kiatakachoweza kututenga na upendo wa Mungu katika Kristo Yesu Bwana wetu."

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni mambo gani muhimu ya kuelewa kuhusu maumbile/asili ya Mungu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries