settings icon
share icon
Swali

Ikiwa Yesu alilipa bei ya dhambi zetu, kwa nini bado tunakabiliwa na matokeo ya dhambi zetu?

Jibu


Maandiko yanasema, "Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu" (Warumi 6:23). Kristo alilipa adhabu ya dhambi zetu. Sisi wote tunastahili mauti, ambayo ndiyo adhabu ya mwisho kwa dhambi. Kila mtu atalipia dhambi yake isipokuwa akuje kwa Kristo, ambaye amelipa bei ya dhambi yetu kwa damu yake. Adamu na Hawa walipata matokeo ya dhambi yao kwa kufukuzwa kutoka Bustani. Badala ya "matokeo," tunapaswa kuifikiria kama "nidhamu." Mwandishi wa Waebrania anasema hivi juu ya nidhamu na kusudi lake: "Na umesahau kabisa maneno ya kuwatia moyo ambayo Mungu aliwaambia, watoto wake? Alisema, 'mtoto wangu, usipuuzie wakati Bwana anakuadhibu, wala usivunjike moyo akikosoa. Kwa maana Bwana anawaadhibu wale anaowapenda, na anawaadhibu wale anaokubali kama watoto wake.

"Tena mmeyasahau yale maonyo, yasemayo nanyi kama kusema na wana, mwanangu, usiyadharau marudia ya Bwana, wala usizimie moyo ukikemewa naye; maana yeye ambaye Bwana ampenda, humrudi, naye humpiga kila mwana amkubaliye. Ni kwa ajili ya kurudiwa mwastahimili; Mungu awatendea kama wana; maana ni mwana yupi asiyerudiwa na babaye? Basi kama mkiwa hamna kurudiwa, ambako ni fungu la wote, ndipo mmekuwa wana wa haramu ninyi, wala si wana wa halali. Na pamoja na hayo tulikuwa na baba zetu wa mwili walioturudi, nasi tukawastahi; basi si afadhali sana kujitia chini ya Baba war oho zetu na kuishi? Maana ni hakika, hao kwa siku chache waliturudi kama walivyoona vema wenyewe; bali yeye kwa faida yetu, ili tuushiriki utakatifu wake. Kila adhabu wakati wake haionekani kuwa kitu cha furaha, bali cha huzuni; lakini baadaye huwaletea wao waliozoezwa nayo matunda ya haki yenye amani" (Waebrania 12: 5-11).

Mungu anaonyesha upendo wake kwa kutukosoa na/au kutumia nidhamu kutuleta mahali ambapo anataka tuwe. Baba mwema hufanya nini wakati anapomwona mtoto wake akipotea njia sahihi? Anamrudisha kwa njia ya nidhamu. Adhabu inaweza kuja kwa aina nyingi, kulingana na uzito wa kosa. Ikiwa mtoto hajawahi kuadhibiwa au kamwe kuteseka na matokeo ya hatua yake mbaya, hawezi kujifunza nini kilicho sahihi.

Kwa hivyo, kutokana na upendo Mungu anawaadhibu wale walio wake. Ikiwa haujawahi kuteseka na matokeo ya dhambi yako, utajuaje unapofanya lililo sahihi au lisilo sahihi? Mtunga-zaburi anasema, "Je! Wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, hawakumwita Mungu" (Zaburi 53: 4). Angalia pia Zaburi 10:11, "Asema moyoni mwake, Mungu amesahau, Aficha uso wake, haoni kamwe." Ikiwa Mungu hakuleta matokeo, hatuwezi kujifunza kutokana na makosa yetu na kubadili njia zetu. Mungu huwaadhibu pekee wale ambao ni wake, na hufanya hivyo kwa sababu ya upendo kwetu, sio kutudhuru au kutuvunja chini.Ni njia ya Mungu ya kusema, "Mtoto wangu, unaenda njia mbaya, na ni wakati wa kugeuka na kufanya yaliyo sawa." Ikiwa hatutakosolewa tunapofanya makosa, basi tutaendelea kufanya makosa.

Mungu amelipa adhabu kwa ajili ya dhambi zetu ili hatupaswi kuteseka kifo cha pili, ambayo ni Jahannamu (Ufunuo 20:14). Kwa sababu ya upendo wake kwetu, Yeye hutuadhibu na hutuleta katika uhusiano na Yeye ambayo anataka. Kwa hivyo wakati ujao unapohisi kuwa unasumbuliwa na matokeo ya dhambi yako, kumbuka ni Mungu anayekuadhibu kutokana na upendo.

Hatimaye, vitendo vya kutotii sheria za Mungu mara nyingi husababisha madhara ya muda ambayo hayahusiani na nidhamu ya Mungu. Kwa mfano, muuaji ambaye anakuja kwa Kristo na kutubu dhambi zake zote atapokea msamaha wa Mungu kwa maana ya milele, naye atakuwa na ushirika kamili na Mungu wa milele mbinguni. Hata hivyo, jamii ambayo anaishi bado itahitaji kwamba kulipa bei ya uhalifu wake kwa maana ya muda. Anaweza kutumia maisha yake yote gerezani au hata kuuliwa kwa ajili ya uhalifu wake. Lakini hata katika hali hizi, anaweza kutumika sana kwa Mungu wakati akingojea ukombozi wake wa mwisho na furaha ya milele.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ikiwa Yesu alilipa bei ya dhambi zetu, kwa nini bado tunakabiliwa na matokeo ya dhambi zetu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries