settings icon
share icon
Swali

Matezo ni nini? Tutawezaje kujua kuwa matezo yatadumu miaka saba?

Jibu


Matezo ni kipindi cha miaka saba kijao cha wakati ambao Mungu atamaliza kuwaadhibu Waisraeli na kumalizia hukumu yake kwa ulimwengu usioamini. Kanisa likiundwa na wote ambao wamemwani Yesu Kristo kama mwokozi wa maisha yao na kuokolewa kutoka ile hukumu ya dhambi, hawatakuwa hapo wakati wa matezo. Kinasa litaondolewa katika ulimwengu katika tukio liitwalo unyakuzi (1 Wathesalonike 4:13-18; 1 Wakorintho 15:51-53). Kanisa limeokolewa kutoka kwa ghadhabu ijayo ( 1 Wathesalonike 5:9). Katika Bibilia yote, matezo yameelezwa kwa majina mengine kama siku ya bwana (Isaya 2:12; 13:6-9; Yoeli 1:15; 2:1-31; 3:14; 1 Wathesalonike 5:2); nyakati ngumu au matezo (Kumbukumbu La Torati 4:30; Sefania 1:1); matezo makuu, ambayo yamaanisha kuwa magumu kwa kipindi kingine nusu cha hiyo miaka saba (Mathayo 24:21); muda au siku ya matezo (Danieli 12:1; Sefania 1:15), siku ya metezo ya Yakobo (Yeremia 30:7).

Eleo lingine la Danieli 9:24-27 ni la maana ili tuelewe lengo na wakati wa matezo. Ukurasa huu unazungumzia juu ya majuma 70 ambayo yametangazwa kunyume na “watu wako.” Watu wa Danieli ni Wayahudi, taifa la Isreli, na Danieli 9:24 yazungumzia kipindi cha muda ambao Mungu amepeana “kumaliza uazi wote, kuweka kikomo dhambi, kutoa utakazo wa uovu wote, kuleta utakatifu wa milele, kutia muhuri maono na unabii na kutia mafuta yeye aliye matakatifu wa watakatifu.” Bwana Mungu asema, “sabini na saba” itatimiza mambo haya yote. Miaka sabini mara saba au miaka 490. (metezo mengine yaleekeza majuma 70 ya miaka.) Haya yamethibitishwa kwa sehemu ingine ya Danieli. Katika aya ya 25 na 26, Danieli anaambiwa kuwa Masia atapunguza baada ya “saba saba na sitini na mbili saba” (69 kwa jumla), kwa kwanzia na agizo la kujenga Yerusalemu. Kwa njia nyingine mwaka wa 69 katika miaka 483 baada ya agizo la kuijenge tena Yerusalemu hadi wakati Yesu alisulubiwa. Wasomi wengine wa kikristo, mbali na mitazamo ya juu ya nyakati za mwisho (matukio yajayo), wako na elewo la hapo juu la miaka 70 ya Danieli.

Miaka 483 ikishapita tangu agizo kutolewa kuijenga Yerusalemu na kutoweka kwa Masia, hili linaacha miaka saba kutimizwa kulinga na Danieli 9:24: “Muda wa majuma sabini umeamriwa juu ya watu wako, na juu ya mji wako mtakatifu, ili kukomesha makosa, na kuishiliza dhambi, na kufanya upatanisho kwa ajili ya uovu, na kuleta haki ya milele, na kutia muhuri maono na unabii na kumtia mafuta yeye aliye mtakatifu.” Huu wakati wa mwisho wa miaka sabini unajulikana kama wakati wa matezo-ni wakati ambao Mungu alimaliza kuhukumu Israeli kwa dhambi zao.

Danieli 9:27 linatupa mwangaza kidogo wa miaka saba ya matezo: “Naye atafanya agano thabiti na watu wengi kwa muda wa juma moja; na kwa nusu ya juma hiyo ataikomesha sadaka na dhabihu; na mahali pake litasimama chukizo la uharibifu; na hivyo, hata ukomo, na ghadhabu iliyokusudiwa imemwagwa juu yake Mwenye kuharibu.” Mtu ambaye aya hii inazungumzia ni mtu ambaye Yesu anamwita “chukizo la uharibifu.” (Mathayo 24:15) na anaitwa “mnyama” katika Ufunuo Wa Yohana 13. Danieli 9:27 yasema kwamba mnyama atafanya agano kwa miaka saba, lakini katikati mwa majuma haya (miaka 3½ kuwa matezo), atavunja agano, na kukomesha thabihu zote. Ufunuo Wa Yohana 13 yafafanua kuwa mnyama huyu ataweka sanamu yake katika hekalu na kutaka watu wamsujudu. Ufunuo Wa Yohana 13:5 yasema kwamba haya yatendaelea kwa kipindi cha miezi 42, ambayo ni 3½ . jinsi Danieli 9:27, inasema kuwa haya yatatokea katikati mwa majuma, na Ufunuo Wa Yohana 13:5 yasema kuwa mnyama atafanya hivyo kwa kipindi cha miezi 42, ni rahisi kuona kuwa muda wote ni miezi 84 au miaka saba. Pia Danieli 7:25 mahali ambapo “wakati, na nyakati mbili, na nusu wakati” (wakat= mwaka 1, nyakati mbili= miaka 2, nusu wakati= ½ ; jumla ya 3½ ) pia yaasiria “matezo makuu,” mwisho wa kipindi cha miaka saba ya matezo wakati mnyama atakuwa mamlakani.

Kwa maelezo zaidi kuhusu matezo, angalia Ufunuo Wa Yohana 11:2-3, ambayo yazungumzia siku 1260 na miezi 42, na Danieli 12:11-12, ambayo yazungumzia siku 1290 na siku 1335. Hizi siku zinaashiria muda wa katikati wa matezo. Siku zaidi katika Danieli 12 zaweza jumulisha wakati na mwisho wa hukumu ya mataifa (Mathayo 25:31-46) na wakati wa miaka elfu moja ya ufalme wa Kristo utakapo wekwa msingi (Ufunuo Wa Yohana 20:4-6).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Matezo ni nini? Tutawezaje kujua kuwa matezo yatadumu miaka saba?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries