settings icon
share icon
Swali

Kwa nini Mungu anaruhusu matendo mazuri kufanyikia watu waovu?

Jibu


Swali hili linafanana na kinyume chake: "Kwa nini Mungu anaruhusu matendo mabaya yafanyikie watu wema?" Maswali yote mawili yanarejelea kile kinachoonekana kuwa udhalimu wenye shida tunayoshuhudia kila siku. Zaburi ya 73 ni jibu letu kwa maswali sawa ambayo pia yalimuuma mtunga-zaburi. Alijikuta katika dhiki ya kutisha na kwa uchungu wa roho anaandika, "Lakini mimi, miguu yangu ilikuwa karibu kuteleza; Nilikuwa nimekwisha kupoteza mwelekeo wangu. Kwa maana niliwachukia wenye kiburi wakati niliona mafanikio ya waovu "(Zaburi 73: 2-3).

Mwandishi wa zaburi hii ni mtu kwa jina Asafu, kiongozi wa mojapo za kwaya ya hekalu.Kwa kawaida, hakuwa mtu mwenye mali, badala yake alikuwa mtu aliyepeana maisha yake kumtumkia Mungu(angalia 1wakolosai25). Lakini, kama sisi, alikuwa amepitia mashida Fulani na kujiuliza udhalimu wake. Aliwaangalia watu waovu waliomzunguka wakiishi kwa amri zao wenyewe,wakifurahia mali yao na burudani za kila aina za dunia na wakikusanya utajiri.Analalamika,"Hawana mashida;miili zao ni zenye afya na nguvu.Wako huru kutoka mizigo ya kawaida na mwanadamu;hawakumbani na magonjwa ya wanadamu"(zaburu73:4-5).

Asaph alikuwa akiwaangalia watu hawa ambao hawakuwa na matatizo. Wanaweza kulipa bili zao. Walikuwa na mengi ya kula na anasa nyingi. Lakini Asafu masikini alikuwa ameshughulika na kuongoza kwaya na kujaribu kuishi maisha ya kimungu. Na kufanya mambo mabaya zaidi, uchaguzi wake kumtumikia Mungu haukuonekana kumsaidia. Alianza kuwachukia watu hawa na hata kumuuliza Mungu kwa nini angeweza kuruhusu kitu hicho kutokea.

Ni mara ngapi tunajipata tunafanana na Asafu? Tunatoa maisha yetu kwa kumtumikia Mungu. Kisha tunashuhudia watu waovu, wasiomcha Mungu wanaotuzunguka hupata mali mpya, nyumba za kifahari, kukuzwa, na mavazi mazuri, wakati tunaangaika kifedha. Jibu liko katika Zaburi yote. Asafu aliwachukia watu hawa waovu mpaka akagundua jambo moja muhimu sana. Alipoingia patakatifu pa Mungu, alielewa kikamilifu hatima yao ya mwisho: "Wakati nilijaribu kuelewa haya yote, ilikuwa ngumu kwangu mpaka nikaingia patakatifu pa Mungu; basi nilielewa hatima yao ya mwisho. Hakika wewe huwaweka juu ya ardhi inayoteleza; unawaweka chini kuwaangamiza. Jinsi gani wanaangamizwa kwa ghafla, wameangamizwa kabisa na hofu! Kama ndoto wakati mtu anaamka, basi wakati unapoinuka, Ee Bwana, utawadharau kwa mawazo" (Zaburi 73: 16-20). Wale ambao wana utajiri wa muda duniani ni kweli ni ombaomba wa kiroho kwa sababu hawana utajiri wa kweli-uzima wa milele.

Kuna mara nyingi ambapo hatuelewi kinachotokea kwetu, wala hatuelewi jinsi huduma inavyofanya kazi. Wakati Asafu aliingia patakatifu pa Mungu, alianza kuona kwamba hakuna haja ya kuwa na wivu juu ya mafanikio ya waovu kwa sababu mafanikio yao ni udanganyifu. Alianza kuelewa kwamba mdanganyifu wa kale, Shetani, alikuwa ametumia uongo kumvuruga kutoka kwa ukweli wa Mungu. Baada ya kuingia patakatifu, Asafu aligundua kwamba mafanikio ni utimilifu wa kidunia, kama ndoto nzuri ambayo inatupendeza kwa muda mfupi tu, lakini, tunapoamka, tunagundua kuwa haikuwa halisi. Asafu anajikemea mwenyewe kwa upumbavu wake mwenyewe. Anakubali kuwa "mpumbavu na mjinga" kuwachukia waovu au kuwa na wivu wa kuangamia (Zaburi 73:22). Mawazo yake kisha yakarudi kwa furaha yake mwenyewe kwa Mungu wakati aligundua furaha zaidi, utimilifu, na mafanikio ya kweli ya kiroho aliyo nayo katika Muumba.

Tunaweza kosa kuwa na kila kitu tunachotaka hapa duniani, lakini siku moja tutafanikiwa kwa kila kitu milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu. Wakati wowote tunapojaribiwa kujaribu njia nyingine, tunapaswa kumbuka kwamba iyo njia nyingine mwisho wake ni mauti (Mathayo 7:13). Lakini njia nyembamba mbele yetu kupitia Yesu ndiyo njia pekee inayoongoza kwenye uzima wa milele. Hiyo inapaswa kuwa furaha yetu na faraja yetu. "Ni nani ninaye mbinguni isipokuwa wewe? Na ulimwengu haitamani kitu ingine isipokuwa wewe. ... Wale walio mbali na wewe wataangamia; unawaangamiza wote wasioaminifu kwako. Lakini kwangu, ni vizuri kuwa karibu na Mungu. Nimemfanya Bwana Mwenye Enzi Kuu kimbilio langu. . . "(Zaburi 73:25, 27-28)

Hatuhitaji kujishughulisha wenyewe wakati matendo mazuri yanaonekana kufanyikia watu waovu. Tunahitaji tu kuweka lengo letu kwa Muumba wetu na kuingia katika kuwepo Kwake kila siku kupitia njia ya Neno Lake takatifu. Huko tutapata ukweli, kuridhika, utajiri wa kiroho, na furaha ya milele.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Kwa nini Mungu anaruhusu matendo mazuri kufanyikia watu waovu?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries