settings icon
share icon
Swali

Ninaweza kufanya nini wakati mimi ni chini ya mashambulizi ya kiroho?

Jibu


Kitu cha kwanza cha kufanya wakati tunaamini kuwa tunaweza kuwa chini ya mashambulizi ya kiroho ni kuamua, kadiri tunavyoweza, kama tunachokiona ni mashambulizi ya kiroho kutoka kwa nguvu za pepo au tu matokeo ya kuishi katika ulimwengu ulio na dhambi . Watu wengine hulaumu kila dhambi, migogoro yote, na kila tatizo juu ya mapepo wanaoamini wanahitaji kukemewa nje. Mtume Paulo anawaagiza Wakristo kupigana vita dhidi dhambi iliyo ndani yao wenyewe (Warumi 6) na kupigana vita dhidi ya mwovu (Waefeso 6: 10-18). Lakini ikiwa sisi tunashambuliwa kiroho kutoka kwa nguvu za pepo au tu kupambana na uovu ndani yetu wenyewe na yale yaliyomo duniani, mpango wa vita ni sawa.

Mambo muhimu katika mpango wa vita yanapatikana katika Waefeso 6: 10-18. Paulo anaanza kwa kusema kwamba lazima tuwe hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu Zake, si kwa nguvu zetu wenyewe, ambazo sio sawa na za shetani na majeshi yake. Paulo basi anatuhimiza kuvaa silaha zote za Mungu, ndiyo njia pekee ya kusimama dhidi ya mashambulizi ya kiroho. Kwa nguvu zetu wenyewe, hatuwezi kushinda "majeshi ya kiroho ya uovu katika hali za mbinguni" (mstari wa 12). Ni "silaha kamili za Mungu" ambazo zitatuwezesha kuhimili mashambulizi ya kiroho. Tunaweza tu kuwa hodari katika nguvu za Bwana; ni silaha za Mungu zinazotulinda, na vita yetu ni dhidi ya nguvu za kiroho za uovu duniani.

Waefeso 6: 13-18 inatueleza silaha za kiroho ambazo Mungu anatupa, na habari njema ni kwamba mambo haya yanapatikana kwa urahisi kwa wote wanao wa Kristo. Tunapaswa kusimama imara na

Hali tumejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani, na kufungiwa miguu utayari tupatao kwa Injili ya amani; zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu; wa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote.'' (Waefeso 6:18). Je! Vipande hivi vya silaha za kiroho vinawakilisha nini katika vita vya kiroho? Tunapaswa kusema kweli dhidi ya uongo wa Shetani. Tunapaswa kupumzika katika ukweli kwamba tunasemwa kuwa wenye haki kwa sababu ya sadaka ya Kristo kwa ajili yetu. Tunapaswa kutangaza injili bila kujali upinzani gani tunaopokea. Hatupaswi kutingizika katika imani yetu, haijalishi jinsi tunavyoshambuliwa. Ulinzi wetu wa mwisho ni uhakika tunao wa wokovu wetu, uhakikisho kwamba hakuna nguvu ya kiroho inaweza kuchukua. Silaha yetu ni Neno la Mungu, si maoni yetu na hisia zetu. Hatimaye, tunapaswa kufuata mfano wa Yesu kwa kutambua kwamba baadhi ya ushindi wa kiroho huwezekana tu kwa njia ya sala.

Yesu ndiye mfano wetu mkuu wakati wa kuljiinda kutoka mashambulizi ya kiroho. Angalia jinsi Yesu alivyo yazuia mashambulizi ya moja kwa moja kutoka kwa Shetani wakati alijaribiwa naye jangwani (Mathayo 4: 1-11). Kila jaribio lilijibiwa kwa njia ile ile-na maneno "Imeandikwa" na nukuu kutoka kwa Maandiko. Yesu alijua Neno la Mungu aliye hai ni silaha yenye nguvu zaidi dhidi ya majaribu ya shetani. Ikiwa Yesu mwenyewe alitumia Neno kupinga shetani, je! Tunatamani kutumia chochote kinginecho?

Mfano bora wa jinsi ya kutoshiriki katika mapambano ya kiroho ni wana saba wa Skewa, kuhani mkuu wa Kiyahudi, ambaye alizunguka kufukuza pepo wabaya kwa kutaja jina la Bwana Yesu juu ya wale waliopagawa na pepo wahafu. Siku moja yule pepo mchafu akawajibu, akawaambia, Yesu namjua na Paulo namfahamu, lakini ninyi ni nani?" Na yule mtu aliyepagawa na pepo mchafu akawarukia wawili, akawaweza, akawashinda, hata wakatoka mbio katika nyumba ile hali wa uchi na kujeruhiwa."(Matendo 19: 15-16). Wana saba wa Skewa walikuwa wakitumia jina la Yesu, lakini kwa sababu hawakuwa na uhusiano na Yesu, maneno yao hayakuwa na nguvu yoyote au mamlaka. Hawakutegemea Yesu kama Bwana na Mwokozi wao, na hawakuwa wakitumia neno la Mungu katika vita vyao vya kiroho. Matokeo yake nikuwa, walipata kichapo cha aibu. Hebu tupate kujifunza kutoka kwa mfano wao mbaya na kufanya vita vya kiroho kama vile Biblia inavyoeleza.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ninaweza kufanya nini wakati mimi ni chini ya mashambulizi ya kiroho?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries