settings icon
share icon
Swali

Ni wakati gani wa shida ya Yakobo?

Jibu


Maneno "wakati wa shida ya Yakobo" ni nukuu kutoka Yeremia 30: 7 ambayo inasema, "Kweli, siku hiyo ni kubwa, hakuna nyingine kama hiyo; ni siku ya huzuni kwa watu wa Yakobo; hata hivyo, wataokolewa humo".

Katika mistari iliyopita ya Yeremia 30, tunaona kwamba Bwana anasema na Yeremia nabii kuhusu Yuda na Israeli (30: 3-4). Katika mstari wa 3, Bwana anaahidi kwamba siku moja baadaye, atawaletea Yuda na Israeli tena kwenye nchi aliyowaahidi baba zao. Mstari wa 5 unaelezea wakati wa hofu kubwa na kutetemeka. Mstari wa 6 unaelezea wakati huu kwa njia ambayo picha wanadamu wanapitia maumivu ya kujifungua, tena kuonyesha muda wa uchungu. Lakini kuna tumaini kwa Yuda na Israeli, ingawa huu unaitwa "wakati wa dhiki ya Yakobo" Bwana ameahidi kuwa ataokoa Yakobo (akizungumzia Yuda na Israeli) kutoka wakati huu wa shida kubwa (mstari wa 7) .

Katika Yeremia 30: 10-11 Bwana asema hivi, "Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Usiogope ee Yakobo mtumishi wangu, wala usifadhaike, ee Israeli; maan nitakuokoa huko mbali uliko, na wazawa wako kutoka uhamishoni. Utarudi na kuishi kwa amani, wala hakuna mtu atakayekuogopesha. Maana mimi niko pamoja nawe, kukuokoa. Mimi mweneyzi-Mungu nimesema. Nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambayo nilikutawanya kati yao; lakini wewe sitakuongamiza kabisa. Nitakuadhibu kadiri unavyostahili wala sitakuacha uende bila kukuandibu. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema."

Pia, Bwana anasema atawaangamiza mataifa ambao walishikilia Yuda na Israeli katika uhamisho, na hawezi kuruhusu Yakobo kuangamizwa kabisa. Hata hivyo, ni lazima ieleweke kwamba Bwana anaelezea huu kama wakati wa nidhamu kwa watu Wake. Anasema juu ya Yakobo, " Nitayaangamiza kabisa mataifa yote ambayo nilikutawanya kati yao; lakini wewe sitakuongamiza kabisa. Nitakuadhibu kadiri unavyostahili wala sitakuacha uende bila kukuandibu."

Yeremia 30: 7 inasema, "Kweli siku hiyo ni kubwa, hakuna nyingine kama hiyo." Wakati wa pekee ambao unafanana na maelezo haya ni kipindi cha dhiki. Wakati huu haufananiki na historia.

Yesu alielezea dhiki kwa kutumia picha sawa na Yeremia. Katika Mathayo 24: 6-8, alisema kuwa kuonekana kwa Wakristo wa uongo, vita na uvumi wa vita, njaa, na tetemeko la ardhi ni "mwanzo wa maumivu ya uzao."

Paulo, pia, alielezea dhiki hii kuwa kama maumivu ya uzazi. Wathesalonike wa kwanza 5: 3 inasema, "Watu watakapokuwa wanasema: "Kila kitu ni shwari na salama", ndipo uharibifu utakapowaangukia ghafla! Mambo hayo yatatukia ghafla kama uchungu wa uzazi unavyomjia mama anayejifungua, wala watu hawataweza kuepukana nayo." Tukio hili linafuatia Ukombozi na kunyakuliwa kwa Kanisa, katika 4: 13-18. Katika 5: 9, Paulo anathibitisha ukosefu wa Kanisa kutoka wakati huu kwa kusema, "Maana Mungu hakututeua ili tuangamizwe na ghadabu yake, bali tuupate wokovu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo." Ghadhabu inayozungumziwa hapa ni hukumu ya Mungu juu ya ulimwengu usioamini na nidhamu Yake kwa Israeli wakati wa dhiki.

Uu "uchungu wa uzazi" umeelezwa kwa undani katika Ufunuo 6-12 Sehemu ya kusudi la Dhiki ni kurejesha Israeli kwa Bwana.

Kwa wale ambao wamempokea Kristo kama Mwokozi kutoka kwa dhambi, wakati wa shida ya Yakobo ni kitu ambacho tunapaswa kumsifu Bwana, kwa maana inaonyesha kwamba Mungu anaweka ahadi zake. Alituahidi uzima wa milele kwa njia ya Kristo Bwana wetu, na ameahidi nchi, uzao, na baraka kwa Ibrahimu na uzao wake wa kimwili. Hata hivyo, kabla ya kutimiza ahadi hizo, atakuwa na upendo lakini wa kuadhibu taifa la Israeli ili waweze kurejea kwake.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Ni wakati gani wa shida ya Yakobo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries