settings icon
share icon
Swali

'Maranatha' ina maana gani?

Jibu


Maranatha ni neno la Kiaramu ambalo linamaanisha "Bwana anakuja" au "Ee Bwana njoo." Kanisa la kwanza lilikumbwa na mateso mengi, na maisha hayakuwa rahisi kwa Mkristo chini ya utawala wa Kirumi. Warumi walihitaji kila mtu kukili kwamba Kaisari alikuwa mungu. Wakristo wa kwanza walijua kwamba kuna Mungu mmoja tu na Bwana mmoja-ambaye ni Yesu Kristo-na kwa dhamiri njema hawakuweza kumwita Kaisari "Bwana," kwa hiyo Warumi waliwaona kama waasi, waliwatesa, na kuwaua.

kwa kuishi chini ya hali ngumu kama hiyo, maadili ya waumini yalijengeka kwa matumaini ya ujio wa Kristo. Na hapo "Maranatha!" ikawa salamu ya kawaida ya waumini waliodhulumiwa, ikibadilisha ile salamu ya Kiyahudi shalomu ("amani"). Wafuasi wa Yesu walijua kuwa hakutakuwa na amani kwa sababu Yesu alikuwa amekwisha waambia hivyo (Mathayo 10:34, Luka 12:51). Lakini pia walijua kuwa Bwana angerudi kuanzisha ufalme Wake, na kutokana na ukweli huo walipata faraja kubwa. Kila mara wajikumbusha na kukumbusha kwamba Bwana anakuja (Luka 21:28, Ufunuo 22:12). Yesu alifundisha mifano mingi juu ya mada hii ya kukesha na kusubiri na kuwa tayari kwa kurudi kwake (Mathayo 25: 1-13; Luka 12: 35-40).

Leo hii, waumini katika Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo wanaishi maisha yao kwa nuru ya ufahamu kwamba Anaweza rudi wakati wowote. Tunapaswa kuwa tayari wakati parapanda italia. Kila siku tunapaswa kumtarajia ujio Wake, na kila siku tunapaswa kutazamia ujio Wake. Maranatha hutukumbusha kulenga macho yetu kwa mambo ya milele ya Roho Mtakatifu. Kudumu kwa vitu vya kimwili ni kudumu mara kwa mara katika akili hati hati. Tukiangalia chini, twaona ardhi; tukiangalia kando, twaona vitu vya dunia. Lakini tukitazama juu, twaona tumaini la ujio wa karibuni wa Bwana wetu Yesu Kristo. Kwa wale ambao wamekufa moyo hii leo, Maranatha! Kwa wale ambao wana wanahofu hii leo, Maranatha! Kwa wale wote ambao wamejawa na wasiwasi juu ya matatizo yanayowakabili, Maranatha! Bwana wetu anakuja!

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

'Maranatha' ina maana gani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries