settings icon
share icon
Swali

Je! Tunawezaje kutofautisha maradhi ya akili na kupagagwa na pepo?

Jibu


Jibu fupi kwa swali hili ni kwamba biblia haizungumzii tofauti kati ya kupagagwa na pepo na maradhi ya akili. Kwa sababu Mungu alichagua kutowandaa Wakristo kwa kazi hii, pengine tunapaswa kudhani hili sio jambo ambalo tumelitiwa kufanya. Hata hivyo kuna mambo mawili tunayoyajua kwa uhakika kutoka kwa Maandiko.

Kwanza, tunajua kutoka katika Biblia kwamba mapepo wanaweza na huwapagaga watu ambao sio wa Kristo, na Maandiko yanatoa baadhi ya mifano ya watu waliopagagwa na mapepo. Kutokana na maelezo haya, tunaweza kupata baadhi ya dalili za ushawishi wa pepo na vile vile kupata ufahamu kuhusu jinsi pepo anavyomshika mtu. Katika baadhi ya vifungu hivi, kupagagagwa na mapepo husababisha magonjwa ya kimwili (kutoweza kuongea, dalili ya kifafa, upofu, nakadhalika. (Mathayo 9:32-33, Marko 9:17-18); katika hali nyingine pepo humfanya mtu kutenda maovu (Yudasi ndiye mfano mkuu); katika Matendo 16:16-18, inaonekana roho alimpa kijakazi uwezo fulani wa kujua mambo zaidi ya ujuzi wake mwenyewe (roho ya uaguzi); kwa habari ya pepo kwa Mgerasi aliyekuwa amepagagwa na wingi wa mapepo, alikuwa na nguvu zisizo za kibinadamu, akajikata, akizunguka huku na huku akiwa uchi, akakaa kati ya mawe ya kaburi (Marko 5::1-17). Mfalme Sauli baada ya kuasi dhidi ya BWANA, alisumbuliwa na roho mchavu (1 Samueli 16:14-15; 18:10-11; 19:9-10) na matokeo ya dhahiri ya tabia ya kuhusunika na ongezeko la nia ya kutaka kumuua Daudi (mfalme aliyefuata wa Israeli na aliyetiwa wakfu na Mungu).

Pili, tunapaswa kutiwa moyo pakubwa kwa kujua kwamba haiwezekani kwa Mkristo kupagagwa na pepo. Muumini amejazwa na Roho Mtakatifu wa Mungu ambaye huja na kukaa ndani ya mioyo yetu wakati tunayatoa maisha yetu kwa Kristo (2 Wakorintho 1:22). Ufafanuzi wa kupagagwa na pepo kama “ovu” lamaanisha “najisi” katika Kiyunani (Marko 5:2), kwa hiyo humfanya Roho Mtakatifu asiweze kushiriki na kudumu ndani ya kiumbe kama huyo. Kwa wale ambao hawana Roho Mtakatifu, hata hivyo, hakuna kiasi cha “kusafisha maisha yao” kitakachozuia pepo kuwatawala au kuwashawishi. Mfano wa Yesu katika Mathayo 12:43 unaweka hili wazi:

“Pepo mchafu amtokapo mtu, hutangatanga katika sehemu zisizo na maji akitafuta mahali pa kupumzika, lakini hapati. Ndipo husema, ‘Nitarudi kwenye nyumba yangu nilikotoka.’ Naye arudipo huikuta ile nyumba ikiwa tupu, imefagiliwa na kupangwa vizuri. Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza.” Hapa Yesu anafundisha kwamba hatuna uwezo wa kuifagia na “kuipanga” mioyo yetu wenyewe kwa sababu mioyo yetu “ni mdanganyifu kuliko vitu vyote, ni mwovu kupita kiasi” (Yeremia 17:9). Ni Mungu pekee anaweza kutuokoa na kutuumbia moyo mpya (Ezekieli 36:26) na kutufanya viumbe vipya katika Kristo (2 Wakorintho 5:17).

Hata hivyo, huku Wakristo wakiwa hawawezi pagagwa na pepo, hii haipaswi kukanganywa ili kumaanisha kuwa ni kushawishika na pepo. Mtume Petro ni kielelezo cha muumini ambaye alishawishika na shetani (Mathayo 16:23). Hili laweza kutokea hasa tunapokuwa hatujakomaa katika imani na hatujashiriki vya kutosha katika nidhamu za kiroho za kujifunza Maandiko na maombi kila mara.

Mwisho, neno kwa mwenye busara: baadhi ya watu husitawisha mvuto usiofaa wa shughuli za uchawi na mapepo. Huu ni ushauri potovu. Ikiwa tutamtafuta Mungu pamoja na maisha yetu na tujivike silaha zake na kutegemea nguvu zake (sio nguvu zetu) (Weafeso 6:10-18), hatuna lolote la kuogopa kutoka kwa shetani, kwa kuwa Mungu anatawala vyote. Tunapokuwa ndani ya Kristo, na Yeye ndani yetu, hatuna cha kuogopa kutoka kwa yule mwovu kwa sababu “yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu” (1 Yohana 4:4).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Tunawezaje kutofautisha maradhi ya akili na kupagagwa na pepo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries