settings icon
share icon
Swali

Je, ni ufunguo gani katika ufanisi wa sala?

Jibu


Kila mtu anataka maombi yao kuwa "yenye ufanisi" sana, ili tukizingatia "matokeo" ya sala zetu, tunapoteza kuona nafasi ya ajabu tuliyo nayo katika sala. Kwamba watu kama sisi wanaweza kuzungumza na Muumba wa Ulimwengu kwa yenyewe ni jambo la kushangaza. Jambo la kushangaza zaidi ni ukweli kwamba Yeye husikia na hutenda kwa niaba yetu! Jambo la kwanza tunalohitaji kuelewa juu ya maombi yenye ufanisi ni kwamba Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo alipatwa kuteseka na kufa msalabani na hata kutuwezesha sisi kuingia katika kiti cha neema kuabudu na kuomba (Waebrania 10: 19-25).

Ingawa Biblia inatoa mwongozo mkubwa juu ya jinsi tunaweza kuimarisha mawasiliano yetu na Muumba, sala ya ufanisi ni zaidi ya mtu aneyefanya maombi kuliko ilivyo kwa "jinsi tunapaswa kuomba." Kwa kweli, Maandiko yanasema, "Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii" (Yakobo 5:16), na kwamba "Macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake hukielekea kilio chao" (1 Petro 3: 12; Zaburi 34:15), na tena, "sala ya waadilifu inampendeza" (Mithali 15: 8). Maombi yalimwokoa Danieli mwenye haki kutoka kwenye shimo la simba (Danieli 6:11), na jangwani, watu waliochaguliwa na Mungu walifaidika na uhusiano wa Musa na Mungu (Kutoka 16-17). Sala ya Hana aliyekuwa tasa na mwenye unyenyekevu ilisababisha kuja kwa nabii Samweli (1 Samweli 1:20), na sala za mtume Paulo hata zilifanya dunia kutetemeka (Matendo 16: 25-26). Kwa wazi, maombi ya upendo ya watoto wa Mungu wenye haki yanaweza kufanikisha mengi (Hesabu 11: 2).

Tunahitaji kuhakikisha kwamba maombi yetu yanaambatana na mapenzi ya Mungu. "Na huu ndio ujasiri tulio nao kwake, ya kuwa, tukiomba kitu sawasawa na mapenzi yake, atusikia. Na kama tukijua kwamba atusikia, tuombacho chote, twajua kwamba tunazo zile haja tulizomwomba" (1 Yohana 5: 14-15). Kuomba kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu ni muhimu kuomba kulingana na vile atakavyohitaji, na tunaweza kuona mapenzi ya Mungu yaliyofunuliwa katika Maandiko. Na kama hatujui jinsi ya kuomba, Paulo anatukumbusha kuwa kama watoto wa Mungu tunaweza kutegemea Roho Mtakatifu kutuombea, kama "Roho anaombea watakatifu kulingana na mapenzi ya Mungu" (Warumi 8:27). Na kwa kuwa Roho wa Mungu anajua mawazo ya Mungu, sala ya Roho daima inazingatia mapenzi ya Baba.

Zaidi ya hayo, sala ni kitu ambacho waumini wanapaswa kufanya "daima" (1 Wathesalonike 5:17). Katika Luka 18: 1, kwa mfano, tunaambiwa kuomba kwa uvumilivu "bila kuchoka" Pia, tunapowasilisha maombi yetu kwa Mungu, tunapaswa kuomba kwa imani (Yakobo 1: 5; Marko 11: 22- 24), pamoja na shukrani (Wafilipi 4: 6), na roho wa msamaha kwa wengine (Marko 11:25), kwa jina la Kristo (Yohana 14: 13-14), na kama ilivyoelezwa hapo juu, na moyo unaofaa na Mungu (Yakobo 5:16). Ni nguvu ya imani yetu, sio urefu wa sala zetu ambazo hupendeza Yeye ambaye tunaomba kwake, kwa hiyo hatuhitaji kumvutia Mungu kwa uelevu wetu au akili. Baada ya yote, Mungu anajua mahitaji yetu hata kabla ya kuuliza (Mathayo 6: 8).

Pia, tunapaswa kuhakikisha kuwa hatuna dhambi ambayo haijakiriwa mioyoni mwetu tunapoomba, kwa kuwa hii inaweza kuwa kizuizi kwa sala ya ufanisi. " lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia" (Isaya 59: 2; Zaburi 66:18). Kwa bahati nzuri, "Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote" (1 Yohana 1: 9).

Kikwazo kingine cha mawasiliano bora na Mungu ni kuomba kwa tamaa za ubinafsi na nia mbaya. "Hata mwaomba, wala hampati kwa sababu mwaomba vibaya, ili mvitumie kwa tamaa zenu" (Yakobo 4: 3). Kupinga wito wa Mungu au kupuuza ushauri Wake (Methali 1: 24-28), kuabudu sanamu (Yeremia 11: 11-14), au kuziba masikio kwa kilio cha maskini (Methali 21:13) huwa vikwazo vya ziada kwa maisha ya maombi ya ufanisi.

Sala thabiti ni njia ya kuimarisha uhusiano wetu na Baba yetu wa mbinguni. Tunapojifunza na kutii Neno Lake na kutafuta kumpendeza, Mungu yule ambaye alisimamisha jua juu ya sala ya Yoshua (Yoshua 10: 12-13) anatualika kuja kwa ujasiri mbele ya kiti cha neema na kuomba kwa ujasiri kwamba Atazidisha huruma na neema yake kutusaidia wakati wetu wa mahitaji (Waebrania 4:16).

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, ni ufunguo gani katika ufanisi wa sala?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries