Swali
Ninawezaje kumtambua mwalimu wa uongo/ nabii wa uongo?
Jibu
Yesu alituonya kuwa “Wakristo wa uongo na manabii wa uongo” watakuja na kujaribu kuwadanganya hata wateule (Mathayo 24:23-27; angalia pia 2 Petero 3:3 na Yuda 17-18). Njia nzuri ya kujilinda na uongo na walimu wa uongo ni kuijua kweli. Ili ugundue pingamizi lichunguze pingamizi lenyewe. Muumuni yeyote ambaye, “analisoma Neno la ukweli” (2 Timotheo 2:15) na anafanyia uchunguzi Bibilia kwa makini anaweza kuitambua kanuni ya uongo. Kwa mfano, muumuni ambaye amesoma kazi ya Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu katika Mathayo 3:16-17 papo hapo atashuku kanuni ambayo yakana utatu wa Mungu. Kwa hivyo, hatua ya kwanza ni kuisoma Bibilia na kuhukumu mafunzo yote kwa chenye maandiko yanasema.
Yesu alisema “kwa matunda yake mti hutambulikana” (Mathayo 12:33). Wakati unayatafuta “matunda” hapa kuna majaribio matatu hasa wastahili kuyatumia kutambua uangalifu wa mafunzo yake:
1) Huyu mwalimu anasema nini kuhusu Yesu? Katika Mathayo 16:15-16 Yesu anauliza, “Akawambia, Nyinyi mwaninena mini kuwa ni nani? Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Katika 2 Yohana 9, tunasoma, “Kila apitaye cheo, wala asidumu katika mafundisho ya Kristo, yeye hana Mungu. Yeye adumuye katika mafundisno haya, huyo ana Baba na Mwana pia.” Kwa njia nyingine, Yesu Kristo ako hali moja na Mungu, yeyote ambaye anapuuza kifo cha Yesu kuwa kama dhabihu, na kukataa ubinadamu wa Yesu. Yohana wa kwanza 22: 22 yasema, “Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia.”
2) Je! Huyu mwalimu anaihubiri injili? Injili imefafanuliwa kuwa habari njema kuhusu kifo cha Yesu, kuzikwa kwa Yesu, na kufufuka kwa Yesu, kulingana na maandiko (1 Wakorintho 15:1-4). Jinsi yo yote ile yatakayo kuwa mazuri, kauli “Mungu anakupenda,” “Mungu anatutaka tuwalishe wenye njaa,” na “Mungu anataka uwe tajiri” sio ujumbe kamili wa injili. Vile Paulo anatuonya katika Wagalatia 1:7 “Wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na kutaka kuigeuza injili ya Kristo.” Hakuna mtu yeyote, hata mhubiri mkuu, ako na uhuru wa kuigeuza injili ambayo Mungu alitupa. “Kama tulivyotangulia kusema, na sasa, nasema tena, mtu awaye yote akiwahubiri ninyi injili yo yote isipokuwa hiyo mliyoipokea, na alaaniwe” (Wagalatia 1:9).
3) Je! Huyo mwalimu anamiliki tabia ambazo zamtukuza Mungu? Kusungumzia walimu wa uongo, Yuda 11 yasema, “Ole wao! Kwa sababu walikwenda katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wemeangamia katika maasi ya Kora.” Kwa njia nyingine, mwalimu wa uongo anaweza kujulikana kwa kiburi chake (Kaini aliukataa mpango wa Mungu), tamaa (Balaamu anatabiri kwa ujira), na maasi (Kora anajinua zaidi ya Musa). Yesu alisema tuwe macho na watu kama hao na kwamba tutawajua kwa matunda yao (Mathayo 7:15-20).
Kwa uchunguzi zaidi, visome hivyo vitabu vya Bibilia hasa vyenye tumeviandika ili ukabiliane na mafunzo ya uongo katika kanisa: Wagalatia, 2 Petero, 1 Yohana, 2 Yohana, na Yuda. Kila mara ni vigumu kumtambua mwalimu wa uongo/ nabii wa uongo. Shetani anajigeuza kama malaika wa mwanga (2 Wakorintho 11:15). Ni kwa kujizoesha na ukweli kamili tutaweza kuwatambua wapingamizi.
English
Ninawezaje kumtambua mwalimu wa uongo/ nabii wa uongo?