settings icon
share icon
Swali

Je! Biblia inasema nini kuhusu kiasi cha mamlaka Wakristo wako nayo?

Jibu


Nguvu inaweza kufafanuliwa kam uwezo wa kufanya kitu kulingana na vitu kama nguvu, ustadi, rasilimali, au mamlaka uliyopewa. Biblia inasema, mamlaka ya Mkristo hutoka kwa Mungu kupitia Roho Mtakatifu.

Mungu ndiye chanzo cha mwisho cha mamlaka. Mamlaka yote hutoka Kwake na yote yako chini yake. "Ee Bwana, ukuu ni wako, na uweza, na utukufu, na kushinda, na enzi; maana vitu vyote vilivyo mbinguni na duniani ni vyako; ufalme ni wako, Ee Bwana, nawe umetukuzwa, u mkuu juu ya vitu vyote. Utajiri na heshima hutoka kwako wewe, nawe watawala juu ya vyote; na mkononi mwako mna uweza na nguvu; tena mkononi mwako mna kuwatukuza na kuwawezesha wote" (1Mambo ya Nyakati 29:11-12).

Vifungu vingi vya Agano la Kale vinazungumza juu ya Mungu kuwapa wanyonge nguvu zake: "Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo" (Isaya 40:29). Zaburi 68:35 inasema kuwa Mungu huwapa nguvu watu wake: "Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu." Mara kwa mara tunasoma kuwa nguvu za Mungu zilipewa wafalme (1Saueli 2:10) na manabii: "Bali mimi, hakika nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana; nimejaa hukumu na uwezo; nimhubiri Yakobo kosa lake, na Israeli dhambi yake" (Mika 3:8).

Mungu katika nguvu yake isiyo na mwisho aliyoimimina kwa maisha ya watu Wake inaonekana katika matumizi mengi katika Maandiko. Biblia inasema Injili yenyewe ni nguvu ya Mungu kwa wokovu: "Kwa maana siionei haya Injili; kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia" (Warumi 1:16; pia 1 Wakorintho 1:18).

Nguvy ya Mkristo-uwezo wake wa kufanya kitu chochote cha thamani- hupokewa kutoka kwa Roho Mtakatifu. Wakati Yesu alipaa angani, aliwaambia wanafunzi wake kungoja nguvu waliyohitaji: "Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi" (Matendo 1:8). Bila Roho Mtakatifu, wanafunzi wangekuwa wanazungusha magurudumu yao, haijalishi walikuwa na talanta kiasi gani, nguvu au motisha waliyokuwa nayo katika kuhiburi injili.

Nguvu ya Mkrisoto kutoka kwa Mungu huimarisha mtu wa ndani: "awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani" (Waefeso 3:16). Msife moyo kwa sababu, hata "Kwa hiyo hatulegei; bali ijapokuwa utu wetu wa nje unachakaa, lakini utu wetu wa ndani unafanywa upya siku kwa siku" (2Wakorintho 4:16).

Nguvu ya Mkristo kutoka kwa Mungu humweshesha kuwa mhudumu wa injili: "Injili hiyo ambayo nalifanywa mhudumu wake, kwa kadiri ya kipawa cha neema ya Mungu niliyopewa kwa kadiri ya utendaji wa uweza wake" (Waefeso 3:7).

Nguvu ya Mkristo sio yake mwenyewe. Baada ya Mungu kumtumia Petro kumponya kiwete mwombaji, mtume huyo aliwaeleza walimtizama kwa mshangao kuwa mtu huyu ambaye ameponywa sio kwa nguvy za Petro bali kwa imani katika jina la Yesu Kristo: "Enyi Waisraeli, mbona mnastaajabia haya, au mbona mnatukazia macho sisi, kana kwamba tumemfanya huyu aende kwa nguvu zetu sisi, au kwa utauwa wetu sisi? Mungu wa Ibrahimu na wa Isaka na wa Yakobo, Mungu wa baba zetu, amemtukuza mtumishi wake ... Na kwa imani katika jina lake, jina lake limemtia nguvu mtu huyu mnayemwona na kumjua; na imani ile iliyo kwake yeye imempatia huyu uzima huu mkamilifu mbele yenu ninyi nyote" (Matendo 3:12-16).

Nguvu ya Mkristo itokayo kwa Mungu humwezesha kustahimili mateso katiti kati mwa dhuluma: "Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Basi usiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, wala usinionee haya mimi mfungwa wake, bali uvumilie mabaya pamoja nami kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu" (2 Timotheo 1:7-8).

Nguvu ya Mkristo hudumishwa katika udhaifu: "Naye akaniambia, Neema yangu yakutosha; maana uweza wangu hutimilika katika udhaifu. Basi nitajisifia udhaifu wangu kwa furaha nyingi, ili uweza wa Kristo ukae juu yangu" (2Wakorintho 12:9).

Mkrisot hupata nguvu katika maombi: "Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidi" (Yakobo 5:16).

Mungu huwapa Kristo nguvu katika huduma kuonge akwa jina lake kwa ujaziri katika uwepo wake wa kudumu: "Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari" (Mathayo 28:18-20).

Waefeso 3:20 intuambia kwamba nguvu ya Mungu inapatia ufahamu wetu. Nguvu ya kiungu ii katika kazi ndani ya Mkristo na kutenda ziadi ya yale tunayoweza uliza au fikiria. Anatupa uwezo, nguvu, ujuzi, rasilimali na mamlaka ambayo zaidi yanapita kitu chochote tunaweza kuota au fikiria. Waefeso 1:19-20 inasema kwamba hakuna kitu kinawezea linganishwa na nguvu yake kuu kwetu sisi tunaomwamini. Kwa kweli, nguvu hii Mungu anawapa waumini ndio nguvu ile ile iliyomfufua Kristo Yesu kutoka kwa wafu an kumketisha mahali mbinguni.

Wakristo wana sababu kuu ya kufurahi. Biblia kuwa nguvy ya Mkristo hukirimia chochote kile tunachohitaji katika kuishi maisha matakatifu katika ulimwengu huu wa dhambi: "Kwa kuwa uweza wake wa Uungu umetukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa, kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe" (2Petro 1:3).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Biblia inasema nini kuhusu kiasi cha mamlaka Wakristo wako nayo?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries