settings icon
share icon
Swali

Je, akina mama wote wanapaswa kuwa mama wa kukaa nyumbani?

Jibu


Mjadala wa mama wa kukaa nyumbani umesababisha ugomvi mkubwa, hasa katika mataifa ya Magharibi ambapo wanawake wengi hufanya kazi mbali na nyumbani. Kuna tu mistari mbili ambayo huzungumzia moja kwa moja tu kuhusu mama anayekaa nyumbani na watoto wake. Tito 2: 3-5 inasema, " Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema;

li wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe." Mstari mwingine wa moja kwa moja ni 1 Timotheo 5:14, ambayo inasema, "Basi napenda wajane, ambao si wazee, waolewe, wazae watoto, wawe na madaraka ya nyumbani; ili wasimpe adui nafasi ya kulaumu." Tafsiri nyingine ya maneno "kuwajibika nyumbani" katika kifungu cha Tito 2 ni "kuwa watunza nyumba."

Pia fikiria mistari ambayo haizungumzii mada hii moja kwa moja. Mithali 14: 1 inasema kuwa ni busara kwa mwanamke kujenga nyumba yake. Ingawa si lazima kuwa mama wa kukaa nyumbani ili kujenga nyumbani yako, tunaona kipaumbele ambacho Mungu huweka nyumbani na ushiriki wa mwanamke. Kwa wazi, nyumba haipaswi kuachwa kwa ajili ya kazi ya nje. Kumbukumbu la Torati 6: 4-9 linafundisha umuhimu wa kufundisha watoto wetu daima. Bila shaka, hii inaelekezwa kwa baba na mama. Kukaa nyumbani na watoto hutoa nafasi zaidi ya kuwafundisha watoto njia za Mungu. Hivyo ni uwekezaji mzuri unaofanywa katika maisha ya watoto kwa kutumia kifungu hiki cha Maandiko halisi.

Hatimaye, Mithali 31 ni kifungu kinachojulikana kuhusu mke na mama wa ubora. Kutokana na maelezo yake, tunajifunza kuwa mama huyu alifanya kazi nje ya nyumba. Hata hivyo, familia yake haikukosa chochote. Aliakikisha kuna usawa sahihi, hivyo familia yake haijawahi kuteseka. Familia yake ilikuwa daima kipaumbele chake. Wakati Biblia inawaachia wanawake uchaguzi wa kukaa nyumbani na watoto au kwenda kufanya kazi nje ya nyumba, hakika ni jambo la kupendeza kwa mama kuwa nyumbani na watoto na kujijitolea kuwafundisha wakati wote. Wanawake wanashauriwa sana katika Tito 2 na 1 Timotheo 5 kukaa nyumbani na watoto wao wadogo. Chochote mwanamke anachochagua, lazima nyumba yake iwe kipaumbele na nyanja yake ya msingi ya ushawishi.

English



Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je, akina mama wote wanapaswa kuwa mama wa kukaa nyumbani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries