settings icon
share icon
Swali

Mungu anasema nini kwa kina mama ambao hawajaolewa?

Jibu


Biblia haitazungumzia moja kwa moja suala la mama ambaye hajaolewa, lakini kuna mifano mingi ya ushirikiano wa Mungu kwa upole na wanawake, akina mama, wajane na watoto wao. Mifano hizi, na upole wa Mungu, hutumika haijalishi kama mama hajaolewa au ameolewa au mjane au amepata talaka. Mungu anajua kila mtu kwa kina na anajua hali yake kabisa. Biblia inaonya kuwa ngono nje ya ndoa ni dhambi na ya hatari na italeta taabu, mojawapo ni kuwa kwamba kuna uwezekano wa mwanamke kumlea mtoto mwenyewe, ambayo bila shaka ni ngumu. Na ikiwa ni dhambi yake ambayo imesababisha uzazi wa pekee, Mungu wetu mwenye neema bado ni yuko tayari kutoa msaada na faraja. Na muhimu ni kwamba Yeye hutoa msamaha kwa dhambi hizo kwa njia ya Yesu Kristo na faraja ya milele ya mbinguni kwa mama ambaye anamkubali Yeye, watoto ambao wanamkubali, na hata baba aliyejitenga ambaye humkubali Mungu!

Lakini mara nyingi mwanamke hujikuta akiwa peke yake katika malezi ya watoto huwa sio kosa lake mwenyewe. Kwa kusikitisha, mara nyingi wanawake ni waathirika wasiokuwa na hatia wa ulimwengu ambao wameharibiwa na vita na ugaidi. Wanaume wanakwenda kwenye vita na kamwe hawarudi, wakijitolea maisha yao kwa nchi zao. Ikiwa kifo cha mume kimemwacha mwanamke na watoto, bila shaka Mungu atamsaidia na kumfariji mwanamke huyo.

Mungu anajali familia. Lakini anajali zaidi kwamba kila mtu, bila kujali familia yake inaonekanaje, kutubu dhambi na kuja katika uhusiano naye. Anataka tumjue Yeye, kwa sababu kama viumbe vyake, kumjua hutuletea furaha na kumletea utukufu. Tunazingatia mambo ya maisha yetu, tunashangaa kile watu wengine watafikiri kutuhusu na ikiwa kanisa litatukubali sisi na kama tumeharibu mambo kabisa. Lakini Mungu anamwita Mkristo kuwa na furaha ya kutokuwa na wasiwasi. Amesema kwamba tunapaswa kumtwika yeye fadhaa zetu zote, kwa maana yeye anajishughulisha sana kwa mambo yetu (1 Petro 5: 7). Anataka kubeba mizigo yetu na kutusamehe dhambi zetu na kisha kusahau dhambi zetu na kutusaidia kusonga mbele. Yote anayotutaka tufanye ni kumjua, kumfurahia Yeye, na kumtumainia. Mara nyingi mama/ mzazi wa pekee huwa amewajibika sana, na wakati mwingine inaweza kuwa vigumu tu "kuweka kando" wasiwasi. Mama amgaye hana mume anaweza kuhisi ni kama ana hatia kwa kifikiria tu kutojali! Lakini Mungu ametuamuru kufanya hivyo , kutumia muda kidogo kila siku kumtazama, na kuamini (wakati wa siku zote) kwamba attimiza mahitaji yetu, kimwili na kihisia tunapomtegemea.

Jinsi inavyoonekana kwa mama mzani –pekee ni kutenga wakati wakati wa kusoma Biblia na kuomba. Anaweza kufikiria, "Mimi sina muda wa kufanya hivyo katika harakati ya kufanya kazi na kumlea mtoto na kutunza nyumba na kila kitu kingine." Lakini kama hata kwa nusu saa wakati mtoto wake amelala au anaangaliwa na jamaa au rafiki, anaweza kutenga kando muda wa kuzungumza na Mungu kwa sala na kusikiliza sauti yake katika maandiko, hata kama inamaanisha kutosafisha vyombo hivyo, atapata nguvu kutoka kwa Mungu za kushangaza na kupata kutulia kwa uwepo wake siku nzima. Kutaadhimisha mistari za Biblia kama "Bwana ndiye msaidizi wangu, sitataogopa. Mtu anaweza kunifanya nini? "(Zaburi 118: 6) au" Naweza kufanya yote kwa njia ya Kristo anayeniimarisha "(Wafilipi 4:13) itasaidia kutoa vikumbusho vya upendo na ulinzi wake wakati mambo yanayokuwa magumu au kuleta vikwazo.

Kwa hiyo, Mungu anasema nini kwa akina mama wazazi wa pekee? Kile tu anachosema kwa kila mtu. Tubu dhambi, tumaini kwa Kristo kwa ajili ya msamaha, uwasiliane na Mungu kupitia sala, usikilize sauti Yake kwa njia ya Maandiko, tumaini kwa Mungu kwa ajili ya kupata nguvu katika majaribu, na kuweka tumaini lako katika maisha ya milele ya ajabu pamoja Naye aliyopanga. " lakini, kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia, (Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao." (1 Wakorintho 2: 9).

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu anasema nini kwa kina mama ambao hawajaolewa?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries