settings icon
share icon
Swali

Je! Malkia wa Mbinguni ni nani?

Jibu


Maneno "malkia wa mbinguni" yanaonekana katika Biblia mara mbili, mara yote mbili katika kitabu cha Yeremia. Tukio la kwanza ni kuhusiana na mambo ambayo Waisraeli walikuwa wakifanya yaliyomkasirisha Bwana. Familia zote zilihusika katika ibada ya sanamu. Watoto walikusanya kuni, na wanaume walizitumia kujenga madhabahu kuabudu miungu ya uwongo. Wanawake walihusika katika kukanda kinyunya na kuoka keki ya mikate kwa "Malkia wa Mbinguni" (Yeremia 7:18). Jina hili lilirejelea Ishtar, mungu wa Ashuru na Babeli pia aitwaye Ashtoreti au Astarte na vikundi vingine mbalimbali. Alifikiriwa kuwa mke wa mungu wa uongo Baal, ambaye pia anajulikana kama Molech. Msukumo wa wanawake kuabudu Ashtoreti ulikuja kutokana na sifa yake kama mungu mwenye uwezo wa kuzaa, na, kama kuzaa kwa watoto kulitamaniwa vikubwa kati ya wanawake wa enzi hizo, kuabudu huyu "malkia wa mbinguni" kulikuwa kumeenea kati ya ustaarabu wa kipagani. Kwa kusikitisha, ikawa maarufu kati ya Waisraeli pia.

Rejeleo la pili kwa malkia wa mbinguni hupatikana katika Yeremia 44:17-25, ambapo Yeremia anawapa watu neno la Bwana ambalo Mungu alikuwa amenena naye. Anawakumbusha watu kwamba uasi wao na ibada ya sanamu imesababisha Bwana kukasirika sana nao na kuwaadhibu kwa janga. Yeremia anawaonya kuwa adhabu kubwa inawasubiri wao ikiwa hawatatubu. Wanajibu kwamba hawana nia ya kuacha ibada zao za sanamu, wakiahidi kuendelea kumwaga sadaka za vinywaji kwa malkia wa mbinguni, Ashtoreth, na hata kwenda Zaidi kwa kumpa yeye amani na usitawi ambayo walifurahia wakati mmoja kwa sababu ya neema na huruma ya Mungu.

Haijulikani ambapo wazo kwamba Ashtoreth alikuwa "mke" aliyetokea kwa Yehova, lakini ni rahisi kuona jinsi mchanganyiko wa upagani ambao unamsifu mungu wa kike na ibada ya Mfalme wa kweli wa mbinguni, Yehova, anaweza kusababisha kuchanganya ka Mungu na Ashtoreth. Na kwa vile ibada ya Ashtoreth ilihusisha ngono (uzazi, kuzaa, ukahaba wa hekalu), uhusiano unaosababisha, kwa akili iliyoharibika, itakuwa kawaida asili ya ngono. Kwa wazi, wazo la "malkia wa mbinguni" kama mke au hawara wa Mfalme wa mbinguni ni kuabudu sanamu na sio kibiblia.

Hakuna malkia wa mbinguni. Kamwe hakujawahi kuwa na malkia wa mbinguni. Kwa hakika kuna Mfalme wa Mbinguni, Bwana wa majeshi, Yehova. Yeye pekee anayewalawala mbinguni. Yeye hashiriki utawala Wake au kiti Chake cha enzi au mamlaka Yake na mtu yeyote. Wazo kwamba Maria, mama wa Yesu, ni malkia wa mbinguni halina msingi wa maandiko kwa vyovyote vile, badala yake upinzani kutoka tangazo za makuhani na mapapa wa Kanisa Katoliki la Roma. Wakati Maria alikuwa mwanamke kijana mwenye kumcha Mungu kwa kweli aliyebarikiwa sana kwa kuwa alichaguliwa kumzaa Mwokozi wa ulimwengu, hakuwa kwa njia yoyote ya kiungu, wala hakuwa na dhambi, wala hangekuwa wa kuabudiwa, kuheshimiwa, kutukuzwa, au kuombwa. Wafuasi wote wa Bwana Mungu hukataa ibada. Petro na mitume walikataa kuabudiwa (Matendo 10:25-26; 14:13-14). Malaika watakatifu wanakataa kuabudiwa (Ufunuo 19:10; 22:9). Jibu ni lile lile kila wakati: "Mwabudu Mungu!" Kutoa ibada, heshima, au utukufu kwa mtu yeyote isipokuwa Mungu ni aina ya kuabudu sanamu. Maneno ya Maria mwenyewe katika "Utenzi" wake (Luka 1:46-55) inaonyesha kwamba yeye kamwe hakujifikiria mwenyewe kuwa "safi kabisa" na anastahili utukufu, lakini badala yake akategemea neema ya Mungu kwa ajili ya wokovu: "Na roho yangu hufurahia katika Mungu Mwokozi wangu." Wanye dhambi tu wanahitaji mwokozi, na Maria aligundua hilo kwake mwenyewe.

Zaidi ya hayo, Yesu Mwenyewe alimkemea kwa upole mwanamke aliyemlilia, "Heri tumbo lililokuzaa, na matiti uliyonyonya" (Luka 11:27), akamjibu, "Heri walisikiao neno la Mungu na kulishika." Kwa kufanya hivyo, alikatiza mwelekeo wowote wa kuinua Maria kama chombo cha ibada. Kwa hakika Angesema, "Naam, heri Malkia wa Mbinguni!" Lakini hakufanya hivyo. Alikuwa anathibitisha ukweli huo huo ambao Biblia inathibitisha-hakuna malkia wa mbinguni, na marejeleo tu ya kibiblia ya "malkia wa mbinguni" yanarejelea mungu wa kike wa kuabudu sanamu, dini ya uongo.

English


Rudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Je! Malkia wa Mbinguni ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries