settings icon
share icon
Swali

Mungu aliumba lini malaika?

Jibu


Kujaribu kuamua wakati Mungu aliumba malaika ni jambo lisilo la rahisi kwa sababu kitu chochote ambacho Mungu alifanya "kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu" huweka tukio nje ya wakati yenyewe. Muda na nafasi ni sifa za dunia yetu, si ya Mungu. Yeye hazuliwi kwa saa, siku, na miaka kama sisi. Kwa kweli, Biblia inatuambia kuwa " Kwake Bwana, siku ni kama miaka elfu, na miaka elfu ni kama siku" (2 Petro 3: 8).

Tunajua kwamba Mungu aliumba malaika kabla ya kuumba ulimwengu. Kitabu cha Ayubu kinaelezea malaika wakimwabudu Mungu kama alivyokuwa akiumba ulimwengu: " Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha? " (Ayubu 38: 4-7).

Ikiwa tunazingatia kazi ya malaika, tunaweza kuhitimisha kwamba Mungu aliwaumba malaika tu kabla ya kuumbwa kwa wanadamu kwa sababu moja ya wajibu wao ni kuwa " roho watumikao, wakitumwa kuwahudumu wale watakaourithi wokovu?" (Waebrania 1:14). Pia tunajua kuwa walikuwapo kabla ya bustani ya Edeni, kwa sababu Shetani, aliyekuwa malaika Lucifer, alikuwa tayari katika bustani katika hali yake ya kuanguka. Hata hivyo, kwa sababu kazi nyingine ya malaika ni kumwabudu Mungu kando cha kiti chake cha Ufalme (Ufunuo 5: 11-14), wangeweza kuwepo mamilioni ya miaka-kama tunavyoona wakati-kabla Mungu hajaumba ulimwengu, kumwabudu na kumtumikia.

Kwa hiyo, ingawa Biblia hajasema kwa uwazi wakati Mungu aliwaumba malaika, ilikuwa wakati fulani kabla ya ulimwengu kuumbwa. Iwapo hii ilikuwa siku moja kabla, au mabilioni ya miaka kabla — tena, tunapohesabu wakati-hatuwezi kuwa na uhakika.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Mungu aliumba lini malaika?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries