settings icon
share icon
Swali

Malaika wa uangamizi ni nani?

Jibu


Malaika wa uangamizi pia anajulikana kama malaika wa kifo. Mara nyingi, Mungu alitumia malaika- wajumbe wa mbinguni wa aina fulani- ili kuleta hukumu kwa wenye dhambi duniani. Tafsiri mbalimbali za Biblia zinamtaja mtu huyu kuwa “malaika anayeangamiza.” Katika Biblia, hakuna ishara kwamba malaika yeyote alipewa jina hilo “malaika wa uangamizi” au malaika wa kifo.” Jambo kuu tunaloweza kusema ni kwamba Biblia hutaja kuhusu “malaika anayeangamiza” kurejelea kiumbe au viumbe wa mbinguni ambao walikuja uangamizi walio chini ya hukumu ya Mungu.

Kutembelewa kunaojulikana sana kwa malaika wa uangamizi kulikuwa katika wakati wa pasaka ya kwanza. Misri ilikuwa karibu kupata pigo la kumi na la mwisho ambalo ni kifo cha kifungua mimba. Maagizo ya Musa kwa Waebrania yalikuwa na onyo hili: “Bwana apitapo katika nchi yote kuwapiga Wamisri, ataiona damu juu ya vizingiti na kwenye miimo ya milango, naye atapita juu, wala hatamruhusu mwangamizi kuingia katika nyumba zenu na kuwapiga ninyi” (Kutoka 12:23). Kiumbe hiki kinaitwa “mwangamizi wa kifungua mimba” katika Waebrania 11:28.

Cha kuvutia ni kuwa maandishi ya awali ya Waebrania 12:23 hayataji “malaika” hata kamwe. Inasema tu “mwangamizi” au “mharibifu” au “mwenye kuharibu” angewaua vifungua mimba wa Misri. Inaweza kuwa ni Bwana mwenyewe aliyekuwa mwangamizi, ingawa kuna uwezekano kuwa Mungu alimtuma malaika kufanya tendo hilo. Zaburi 78 inasimulia mapigo ya Misri na kuyajumlisha kama kuwachilia kwa Mungu kwa “kundi la malaika waangamizao” (aya ya 49). Neno la Kiebrania linalotafsiriwa “malaika” limetumiwa hapa, lakini halihusu malaika mmoja pekee.

Malaika anayeangamiza-mjumbe wa mbinguni aliyeleta uharibifu- pia alitumwa na Mungu kuhukumu Waisraeli kwa sabau ya dhambi ya Daudi ya kuwahesabu watu: “Basi Bwana akatuma tauni katika Israeli kuanzia asubuhi mpaka mwisho wa muda ulioamriwa, wakafa watu 70,000 kuanzia Dani hadi Beer-Sheba. Malaika aliponyoosha mkono wake ili uangamizi Yerusalemu,Bwana akahuzunika kwa sababu ya maafa, akamwambia yule malaika aliyekuwa anawadhuru watu, “Yatosha! Rudisha mkono wako.” Wakati huo malaika wa Bwana alikuwa kwenye sakafu ya kupuria ya Arauna, Myebusi. Ikawa Daudi alipomwona huyo malaika aliyekuwa akiwaua watu, akamwambia Bwana, “Mimi ndiye niliyetenda dhambi na kukosa” (2 Samweli 24:15–17).

Waashuri walioshambulia Yerusalemu wakati wa utawala wa Mfalme Hezekia pia walikutana kile kingengeitwa malaika wa kifo au malaika wa uangamizi: “Usiku ule, malaika wa Bwana akaenda, akawaua wanajeshi mia moja themanini na tano elfu katika kambi ya Waashuru. Wenzao walipoamka asubuhi yake, walikuta maiti kila mahali!” (Wafalme 19:32–35). Katika kifungu hiki cha 2 Samweli 24, malaika wa kuagamiza kwa kweli anaitwa “malaika wa Bwana,” ambao wasomi wengi huichukulia hii kurejelea Kristo katika kuonekana kwake kabla autwae mwili.

Malaika mwingine ambaye alileta kifo na uharibifu anatajwa katika hukumu ya Mfalme Herode (Matendo 12:23). Malaika mwenye nia ya kuua, aliyejulikana kama “malaika wa Mungu,”akiwa na upanga alitoa anatoa ilani kwa Balaamu (Hesabu 22:31–33). Na Yesu anataja kwamba malaika watahusika katika hukumu ya waovu wakati wa mwisho (Mathayo 13:49-50). Katika visa hivi hamna malaika amabao wanaitwa “malaika wa uangamizi” au “malaika wa kifo.” Tunaweza kurejelea malaika anayetimiza hukumu ya Mungu kuwa “malaika wa uangamizi,” lakini sio neno la Biblia lililo dhahiri.

EnglishRudi kwa ukurasa wa nyumbani wa Kiswahili

Malaika wa uangamizi ni nani?
Shiriki ukurasa huu: Facebook icon Twitter icon Pinterest icon Email icon
© Copyright Got Questions Ministries